Tanzania Ilipowafukuza Maofisa wa Marekani Kwa Tuhuma za Ujasusi

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 25 ส.ค. 2024
  • Katika nyakati za vita baridi, ujasusi, uhasama na hujuma zilikua ni sehemu ya mchezo. Mafahali wawili wa dunia yaani Marekani na Shirikisho la Sovieti walihasimiana na uhasama huu ulisambaa na kuigawa dunia katikati.
    Nchi nyingi ikiwemo Tanzania ziliamua kutofungamana na yeyote. Hii haikua kinga, bali uhasama uliendelea mpaka ndani ya nchi hizo.
    Tanzania kuwa makao makuu ya ukombozi Afrika pamoja na ushawishi alioujenga Nyerere, ilifanya viunga vyake kuwa uwanja wa mapambano ya vita baridi.
    Mashirika ya kijasusi yalipambana kushawishi, kutafuta taarifa na kusajili vijumbe. Mashaka na kutoaminiana ilikua ni maisha ya kila siku.
    Mwaka 1965 lilitokea tukio Tanzania, tukio liloleta mvutano wa kidiplomasia, ilikuwa ni sehemu ndogo ya matukio yaliyosababishwa na uhasama wa vita baridi. Fuatilia Makala hii:

ความคิดเห็น • 6

  • @iviejustified8109
    @iviejustified8109 6 หลายเดือนก่อน +4

    Kwanini waongee lugha tata...
    Nyerere hakuwa na muda wa kuchezea alifanya vyema saaana mzee wetu Nyerere. Rest in power Mzee wetu

  • @Mapenzi2635
    @Mapenzi2635 หลายเดือนก่อน +1

    Asante sana, Shafii.

  • @KisimaTv99
    @KisimaTv99 6 หลายเดือนก่อน +1

    Ahsante sana Shafii Hamis

  • @surusuru1994
    @surusuru1994 2 หลายเดือนก่อน

    Nyerere❤ Allah akurehem makufuli❤ pia

  • @prince.eric_msemwa9732
    @prince.eric_msemwa9732 6 หลายเดือนก่อน +1

    Siku hzi hali mbaya zaidi, wapelelezi wa magharibi ni weusi kwa ngozi na wateja wao wakubwa ni watu weusi pia. Je hilo linawaacha wapi viongozi wa bara hili

  • @moxasaidi3398
    @moxasaidi3398 26 วันที่ผ่านมา

    Hapo nimesoma kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 ni hao majajusi wawili ndio walio tumwa na kumuezesha mwalimu nyerere kuyafanya kisiwani zanzibar bila ya hao majajusi kwa msaada wao kusingelikuwa na mapinduzi zanzibar wala muungano ni vitu vilipangwa kwa maslahi ya majasusi mbeleni