Panga lamfyeka Mwenyekiti UVCCM Shinyanga avuliwa uenyekiti

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 12 มิ.ย. 2024
  • Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanya imemvua uenyekiti, Jonathan Madete aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho ( UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini.
    Akizungumza ofisini kwake Juni 13, 2024 Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Shinyanga, Richard Masele amesema maamuzi hayo ni ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa huo baada ya Madete kubainika na kosa la utovu wa nidhamu.
    Katibu huyo amesema halmashauri hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Mabala Mlolwa haitamfumbia macho wala kumvumilia kiongozi yeyote au mwanachama wa chama hicho atakayevunja kanuni, taratibu na katiba.
    Amesema hatua hiyo ni kulinda heshima ya chama hicho na jumuiya zake pamoja na kuhakikisha misingi na miongozo yake inaendelea kuheshimwa chini ya Mwenyekiti wao, Dk Samia Suluhu Hassan.
    Kabla ya kuvuliwa uenyekiti, Madete alikuwa anatuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwemo ya kufanya vurugu ofisi ya CCM wilayani humo.

ความคิดเห็น •