Sativa kupatiwa matibabu Dar, ndege yapata dharura

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 28 มิ.ย. 2024
  • Wakati wowote kuanzia sasa Edgar Mwakabela maarufu Sativa anayedaiwa kutoweka Juni 23 na kupatikana mkoani Katavi, atawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
    Sativa alitakiwa kuwasili Dar es Salaam leo saa tisa alasiri kwa ndege maalumu ya kukodi, lakini kutokana na dharura iliyojitokeza, amelazimika kusafirishwa kwa gari la wagonjwa akitokea mkoani Dodoma kuletwa jijini hapa.
    Sativa mkazi wa Mbezi wilayani Ubungo alipatikana Alhamisi Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na majeraha mwilini, akiomba msaada wa kupelekwa hospitalini.
    Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi, Juni 29, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, mratibu wa matibabu na safari ya Sativa, Martin Masese maarufu ‘MMM’ alisema Mwakabela anaendelea vema na hali yake inazidi kuimarika, ndiyo maana madaktari wametoa ruhusa asafirishwe.
    Masese amesema Sativa alikuwa asafiri na Shirika la Ndege la Tanzania, tangu Juni 28 kutoka Katavi kupitia Tabora hadi Dar es Salaam, lakini kwa bahati mbaya usafiri huo ulishajaa.
    Kutokana na hali hiyo, Masese amesema walishauriana na ndugu wa Sativa na madaktari na kuazimia mgonjwa huyo aletwe Dar es Salaam na gari la wagonjwa badala ya kusubiria ndege iliyopangwa kufika Dodoma usiku.

ความคิดเห็น • 35

  • @user-lo8ef9qn2r
    @user-lo8ef9qn2r 7 วันที่ผ่านมา +4

    Mnajua kutufunga kamba kumbe Kwa Gari angeweza kufika vp mkae kusubili ndege?

  • @samsonsamwel8782
    @samsonsamwel8782 6 วันที่ผ่านมา +3

    Na mchunge kutoa taarifa kamil na ikiwezekana mpeleken hata Kenya hapo watamvzia kumalizia

  • @LaurentMpilu-qe6lq
    @LaurentMpilu-qe6lq 7 วันที่ผ่านมา +3

    Danadana Mpira wenye chenga nyingi

  • @IMANWILLIAM-bl2ui
    @IMANWILLIAM-bl2ui 5 วันที่ผ่านมา +2

    mbona umbali wa dom-dar ni mdogo kuliko umbali wa katavi-dom, c mngemleta dar kwa gari tu

  • @swaibushemdoe2143
    @swaibushemdoe2143 7 วันที่ผ่านมา +5

    Kwanini msichukue V8

  • @InjiliyaUfalmetv
    @InjiliyaUfalmetv 4 วันที่ผ่านมา

    Mungu aliyemlinda uhai wake usipotee ndo Mungu atamponya Ameen

  • @YangaNews
    @YangaNews 6 วันที่ผ่านมา +2

    Nyie akili ndogo sana 😢

  • @user-mb2ln1et5w
    @user-mb2ln1et5w 7 วันที่ผ่านมา +3

    Huyo rpc ni WA serekali hii mnayoishbulia Kila siku au??

  • @cheiknamouna2058
    @cheiknamouna2058 2 วันที่ผ่านมา

    Mnakaa kungoja ndege wakati kuna luxury bus mngechukua hata private ila yote kwa yote apewe ulinzi hata ikiwezakana apelekwe nje ya nchi sina iman na serekali yetu imebeba watekaji kukilinda chama tu😭😭

  • @user-mb2ln1et5w
    @user-mb2ln1et5w 7 วันที่ผ่านมา +1

    Poleni sana

  • @prospersteven4564
    @prospersteven4564 7 วันที่ผ่านมา +1

    Poleni saana

  • @deborahmchona5584
    @deborahmchona5584 7 วันที่ผ่านมา +1

    SASA Dodoma mgeendaoja Kwa moja mpka dar

  • @KilingohJuma
    @KilingohJuma 3 วันที่ผ่านมา +1

    Unaongea sana bila vtendo , katavi to Dar usafl upo na Kuna mabas mazur sana, ninyi mnasubili ndege , are you serious ,acheni uzembe

  • @fridayjkajange1247
    @fridayjkajange1247 6 วันที่ผ่านมา +1

    Chukua visa ninda nje ya nchi utanishukuru badae

  • @davidmalisa8043
    @davidmalisa8043 2 วันที่ผ่านมา

    Hawawez uma tumeshajua

  • @HijaSaid-xd7fg
    @HijaSaid-xd7fg 4 วันที่ผ่านมา

    Mpelekeni Kenya, wasije wakammalizia

  • @ndukulusudikucho_
    @ndukulusudikucho_ 6 วันที่ผ่านมา +1

    Tanzania ni Nchi ya Amani saaana ila kwa wanao funga midomo, watekaji hawakuwa na lengo la kumuua yaelekea lengo ni kufikisha ujumbe au walivyoona media zimeanza kurusha wakaona Isiwe tabu , hizi taarifa siku hizi zinafika Dunia nzima na ndio mambo yanayo ichafulia Nchi , kwenye ripoti ya haki za Binam kwa Tz sio nzuri saana , huwa wanatahadharisha saana watu wao wakija kufanya utalii

  • @beinafuu6219
    @beinafuu6219 2 วันที่ผ่านมา

    Watekaji hinaonyesha bado watu hawatak kuua ndo maana kila mbombo yanagoma lisu na huyu vinagoma mama samia saidia hawa watu mama wanakutis ubaya

  • @HijaSaid-xd7fg
    @HijaSaid-xd7fg 4 วันที่ผ่านมา

    Kwa hiyo uma wasipojua alike ndio usalama wake, au wasiojulikana ndio hawatakiwi kujua,

  • @danielndam5997
    @danielndam5997 6 วันที่ผ่านมา

    Askali wanalinda nn eneo la tukio?

  • @MusaJuma-jr7wb
    @MusaJuma-jr7wb 6 วันที่ผ่านมา +1

    Ingekua mbunge maeezezo yotehayo yangekuepo

  • @davidmalisa8043
    @davidmalisa8043 2 วันที่ผ่านมา

    Kwan alionywa ache matus au harakati utakufa brazer acha watu wafanye yao wewe raia tu wako wanene wahii nchi

  • @user-ze6lx9ng6s
    @user-ze6lx9ng6s 3 วันที่ผ่านมา

    Hivi hawa watekaji ni dini gani? Mbona hawana huruma? Pole sana,