Kilichojiri kesi ya padri na wenzake wanane tuhuma za mauaji ya Asimwe

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 27 มิ.ย. 2024
  • Watuhumiwa wanane wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath (2) wamefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba akiwapo Paroko Msaidizi Elipidius Rwegashora wa Parokia ya Bagandika wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera.
    Mtoto Asimwe alichukuliwa Mei 30, 2024 na watu wawili wasiyojulikana akiwa nyumbani na mama yake, saa 2:30 asubuhi katika Kitongoji cha Mbale kilichopo katika Kijiji cha Bulamula, Wilaya Muleba mkoani Kagera.
    Mabaki ya mwili wa marehemu Asimwe yalikutwa yametelekezwa kwenye mfuko wa sandarusi chini ya karavati katika Barabara ya Ruhanga Makongora, katika Kitongoji cha Malele, Kata Ruhanga, Juni 17, 2024 na kuzikwa siku iliyofuata Juni 18, 2024, nyumbani kwao.
    Washtakiwa wote tisa, leo Ijumaa Juni 28, 2024 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba na kusomewa shitaka moja la mauaji ya kusudiwa ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe, ambalo ni shauri namba 17740.
    Awali, Mkuu wa Mashtaka Mkoa Kagera, Waziri Magumbo amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, hivyo washtakiwa wote hawatakiwi kujibu chochote hadi watakapofikishwa Mahakama Kuu.
    Jamhuri imefungua shauri hilo la mauaji ya kukusudia namba 17740 la mwaka 2024 ambalo limesomwa na Mkuu wa Mashtaka Mkoa Kagera, Waziri Magumbo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Bukoba, Eliapokea Wilsoni, aliyesikiliza shauri hilo.
    Baada ya kutajwa kwa shauri hilo na kusikiliza na Hakimu Mkazi Bukoba, Eliapokea Wilson amehairisha kesi hiyo hadi Julai 12, 2024, shauri litakapotajwa tena na washtakiwa wote tisa wamepelekwa rumande, gereza la Bukoba.

ความคิดเห็น • 24

  • @user-jx9xc6vo9x
    @user-jx9xc6vo9x 10 วันที่ผ่านมา

    Pole

  • @user-gh4mg2wn8y
    @user-gh4mg2wn8y 13 วันที่ผ่านมา +2

    Wanyongwe hao kenge..

  • @righitkileo
    @righitkileo 13 วันที่ผ่านมา +1

    Padre tunamalizana nae kwenye Novena kwisha habari yako

  • @Akymedia007
    @Akymedia007 13 วันที่ผ่านมา +1

    Wanyongwe

  • @rhodamwakaje778
    @rhodamwakaje778 12 วันที่ผ่านมา

    Aibu kwa paroko na mzazi wa mtoto hao wamefunga kazi

  • @ndukulusudikucho_
    @ndukulusudikucho_ 11 วันที่ผ่านมา

    Inasikitisha

  • @MustafaabdullaIssa-zl8mp
    @MustafaabdullaIssa-zl8mp 13 วันที่ผ่านมา

    Hatar mpaka mkuu wa kanisa ameshiriki!

  • @efatauroki867
    @efatauroki867 13 วันที่ผ่านมา

    Na wale walio muhwa kamanda mawaza mbona kwann wameachiwa?

  • @YusuphMwangobola
    @YusuphMwangobola 13 วันที่ผ่านมา

    Pingu Moja watu 3

  • @RoseMziray
    @RoseMziray 13 วันที่ผ่านมา

    Wèwe mtangazaji kuwa makini wanne wapi ujui kitu

  • @GaudiosFilbert-fy7bq
    @GaudiosFilbert-fy7bq 13 วันที่ผ่านมา

    Maandiko yalishasema aliyeua kwa upanga auawe kwa upanga sioni kwenda mahakamani wakati kila kitu kipo wazi nikupoteza makaratasi na kusumbua majaji tu

  • @asteriashios1852
    @asteriashios1852 6 วันที่ผ่านมา

    Padre? Makubwa duh

  • @BernadetteSendama
    @BernadetteSendama 9 วันที่ผ่านมา

    Uyo anajifanya kavaa suti alafu muaji wanyongwe kabisa

  • @user-fp5to3bu4s
    @user-fp5to3bu4s 13 วันที่ผ่านมา

    Sidhan kama waliitaji ulinz wowote mngewaachia2 wananchi wakawachoma moto

  • @DevotaIjumba
    @DevotaIjumba 13 วันที่ผ่านมา

    Msipoteze mda nao please please nyongeni kabisa

  • @margarethpolepole7438
    @margarethpolepole7438 13 วันที่ผ่านมา

    Mnaua mtoto kweli kwanini na nyie msiuwawe

  • @revocatusclavery3562
    @revocatusclavery3562 13 วันที่ผ่านมา +1

    Police nimewaheshimu Tena Kwa wale asikali wapelelezi alivyotengeneza nywele kama mchezaji wa mpira au muuingizaji fulani hivi kumbe askari

    • @shaurimtanda8285
      @shaurimtanda8285 10 วันที่ผ่านมา

      alikuwa ni kibu Denis kabla hajawa staa

  • @wadantz123
    @wadantz123 13 วันที่ผ่านมา

    Mbwa hao ni kunyonga ty

  • @NdevuKamdini
    @NdevuKamdini 13 วันที่ผ่านมา

    Wewe mbomba wa nne vip na tisa

  • @user-ml5tq8hj2x
    @user-ml5tq8hj2x 13 วันที่ผ่านมา

    Msipoteze muda nao wale ugali wa bure magereza hao pigeni chuma wana faida gani sasa napata uchungu nikimkumbuka asimwe jamani alivibebwa hana tumaini lolote yuko mikononi mwa wanyanganyi hapana wauwawe tu

  • @mfalmekaitaba2425
    @mfalmekaitaba2425 13 วันที่ผ่านมา

    Ndani ya police kuna vitengo aisee yaani kuna jamaa wawili hapo wamesokota nywele utadhani ni wavuta bangi ukiwakuta mtaani kumbe ni maaskari aisee.

    • @VeronicaAdam-lx8yd
      @VeronicaAdam-lx8yd 13 วันที่ผ่านมา

      Hao wapelelez wanafung ndevu

    • @mfalmekaitaba2425
      @mfalmekaitaba2425 13 วันที่ผ่านมา

      @@VeronicaAdam-lx8yd wanafuga ndevu na kusokota nywele,ndo maana sipendagi kuropoka kwa watu nisiyo wajuwa