TSH. BILIONI 101 KUANZA UJENZI WA KM 73 ZA LAMI BARABARA YA KAHAMA-BULYANHULU JCT - KAKOLA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 30 มิ.ย. 2024
  • Baada ya tarehe 16 Machi 2024 Serikali kusaini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama-Bulyanhulu Jct - Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 kwa kiwango cha lami, tayari Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation imeanza utekelezaji wake.
    Pamoja na Barabara hiyo kufungua fursa za kiuchumi za madini, kilimo, misitu na utalii katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Tabora, Kagera na Kigoma mara baada ya kukamilika pia Barabara hiyo ni muhimu katika shughuli za kiuchumi na kijamii kwa Mkoa wa Shinyanga hususani Manispaa ya Kahama ambako kuna mkusanyiko mkubwa wa Wasafirishaji wa mizigo kutoka bandari kuu ya Tanzania kwenda nchi za jirani za Rwanda na Uganda.
    Akizungumza mara baada ya kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joel Samwel Mwambungu amesema kuwa barabara hiyo inajengwa na serikali kwa gharama ya Shilingi Bilioni 101.2 kwa ufadhili wa Kampuni ya Madini ya Barrick Tanzania Mining Companies (BTMCs).

ความคิดเห็น • 2

  • @chumamasunga8855
    @chumamasunga8855 5 วันที่ผ่านมา +2

    Rasta na vumbi by by🎉🎉👏👏👏👏💪💪🇹🇿🇹🇿

  • @chumamasunga8855
    @chumamasunga8855 5 วันที่ผ่านมา +1

    Bora muanze maana kama nimbi tumekula sana