Dizasta Vina - Hatia V

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 ต.ค. 2024

ความคิดเห็น • 831

  • @kilingechasimulizi2072
    @kilingechasimulizi2072 ปีที่แล้ว +50

    Hakuna, narudia tena hakuna kwa wasanii wote wa tz anayefikia kichwa..hakuna

    • @kilingechasimulizi2072
      @kilingechasimulizi2072 ปีที่แล้ว +3

      Nilikuwa namaanisha hakuna wa kufikia hiki kichwa

    • @kyataonline5262
      @kyataonline5262 ปีที่แล้ว +2

      hakuna ! kwa nini hapati promo akaskika !

    • @emanuelmasanja8312
      @emanuelmasanja8312 ปีที่แล้ว +4

      Hapati promo wapi nani wapi hajasikika huyu kwa hapa hongo hayupo kama yupo mtaje jina

    • @emanuelmasanja8312
      @emanuelmasanja8312 ปีที่แล้ว +2

      Kyata! unajua misingi ya hip hop ama ndo whuzu na bonge la nyau

    • @kyataonline5262
      @kyataonline5262 ปีที่แล้ว

      @@emanuelmasanja8312 hapana siijui buda

  • @mtasma1994
    @mtasma1994 ปีที่แล้ว +7

    Mimi huwa simfananishi Dizasta na Rapper yeyote

  • @dizastavinafanaccount
    @dizastavinafanaccount ปีที่แล้ว +4

    Sanaa yenye usanii.
    Mwendazake Mr Magufuli. Akitenda kosa lakini upendo na uzalendo wake kwa hili taifa ulikuwa juu ya maelezo. Dizasta amesymbolise kupenda na kujali ni kama kujiua mwenyewe.
    Kalamu ya Dizasta si ya kawaida

  • @stevenjohn7816
    @stevenjohn7816 ปีที่แล้ว +5

    Hii ni film iliyokamilika kabisa bongo muvie karibuni

  • @timothykaiza327
    @timothykaiza327 ปีที่แล้ว +65

    Iko Auto playing saa mbili sasa, ni ngoma yangu ya leo kutwa mzee. Tunaozidi irudia HATIA V tukutane hapa. Nitumie mimi kama kitufe cha kukubali ujumbe huu.

  • @mtunda_thegreat_thinker
    @mtunda_thegreat_thinker ปีที่แล้ว +34

    Daaaah broh wewe ninomaaaa sanaaa 👊👊🔥🔥🙏🙏 tunao mkubali dzstvn tujuane kwa likeee hapaaa

  • @revocatusnzungu6580
    @revocatusnzungu6580 ปีที่แล้ว +11

    huwa natamani kila mwezi jamaa atoe ngoma dah ... kuna watu tuna arosto na ngoma zako broo dizasta

  • @jolamboi8842
    @jolamboi8842 ปีที่แล้ว +76

    Dah dizasta ndio my favorite rapper ebu tupia like kama una mkubali mwamba 🔭

  • @millardmbaraka6114
    @millardmbaraka6114 ปีที่แล้ว +7

    Alafu anatokea muhuni mmoja anamlinganisha D vina na makinda dah! Umejua kutufungia mwaka na tafakuri murua kabisa

  • @dizastavina
    @dizastavina  ปีที่แล้ว +293

    LYRICS
    Yeah
    Nilimfahamu baba alikuwa jasiri
    Aliondoa utando ulipodandia kuta
    Alitoa nyoka makatili alipambana na
    Majangiri walipovamia nyumba
    Aliweka paa juu vichwa
    Hatukuogopa baa la njaa tulishiba
    Niliona wengine nguo za kuvaa zimechanika
    Wakati kwetu nyuso ziling’aa migongo ilifunikwa
    Radi ilipiga wala sikujali
    Maana baba alikuwa Simba kwenye msitu mkali
    Wapo waliozijua sifa zake japo
    Mtaani halikuwika jina lake
    Halikuandikwa bali
    Waliona poa ilikuwa jukumu lake
    Mwanaume jasho kutoa ndio hukumu yake
    Ajali ya kisu iliondoa ngozi
    Sikumwona akitoa machozi
    Nilimwona kama Role model
    Alikuwa shupavu hakuwa na roho ndogo
    Mara chache alianguka ali-score zero
    Alipambana upya kama war Hero mdogo mdogo.
    Maisha yake yalikuwa ni adventure
    Alikuwa ni Handyman Carpenter Painter
    Alinijuza aliyoshuhudia kwa macho
    Maana Aliisafiri dunia enzi zake kama Vasco
    Alikuwa so gentle
    Alimpenda mama kupita maelezo
    Watu walijadili nini maana ya upendo
    Waliunda dhana mi niliiona maana kwa vitendo
    Huh
    Ugonjwa uliingia mama aliugua maradhi
    Homa ilivamia ghafla kupumua kazi
    Baba ali-suffer Hospitali kadha wa kadha
    Changamoto afya kupigania zikafungua jamvi huh
    Hali ilileta mtiti
    Hakuipata nafuu ugonjwa ulimweka kingi
    Baba aliwapa Waganga wakuu pesa nyingi
    Mixer kupelekwa majuu zinakoendeshwa ligi
    Mama alilala hospitali miezi kumi na nane
    Nyumbani miezi ilikuwa ni kama karne
    Tulimzoea mama baba hakupagawa
    Alisimama imara japo mambo hayakuwa sawa kamwe
    Maisha yalibadilika tukabadilika pia
    Familia ilipata shida ila baba aliisimamia
    Ukubwa ulimshika majukumu yalishika njia
    Yalimkaba shingo ila sikuwahi kusikia analia
    Bahari ikichafuka inampima nahodha wa meli
    Kama ataogopa kufa au ataongoza Kweli
    Lakini si mawimbi samaki waliododosha meli
    Bali ni rafiki wa karibu wa mama anaitwa Mary
    Mary alimjali baba alimzidi Rose
    Alimzidi Rahma alimzidi Shosi
    Alimletea baba kadi aliniletea chopstick
    Alifua nguo aliosha vyombo na alipika msosi
    Aliingia mpaka chumbani kwa mdingi
    Na udhaifu ukaanza yumbisha misingi
    Mary alimshawishi baba baba akaingia kingi,
    Kwa muda akamsahau mama akapitiwa akamsaliti ah
    Hamu ya tendo ikawazidi maarifa
    Kijakazi akazibeba taarifa
    Miezi kadhaa baada ya mama kupona
    Akasimulia yote aliyoyaona kama picha
    Mama akatokwa na machozi
    Baba akasota kwa magoti
    Mbele yangu mi mwanae mbele ya wazee
    Wakunga wa ndoa wenye busara waliobeba koki
    Huh
    Mama akapata mashoga wakali
    Walitoka jangwa la Sahara na Kalahari
    Wenye elimu za kutosha na ajenda kali
    Wakamwambia talaka ukiomba utazipata mali
    Mama akiwa na chembechembe za hasira
    Akashawishiwa na wasomi wenye hira
    kwa mbali wamezongwa na tamaa za ngawira
    Akasahau kumsamehe kama ilivyosemwa mila
    Mama akafungua jarada la talaka
    Akaandaliwa Majeshi waliojipanga kwa karata
    Baba aligoma kutoa talaka akiomba wamalizie nyumbani sio mahakamani na mama hakutaka
    Mji ulifahamu kesi iling’ara
    Yalipambwa magazeti mengi kwa nakala
    Wanaume washenzi waliongea wapambe
    Vijiwe vya uswazi waligawana pande ka masihara
    Mzee hakukataa mwisho akakili kosa
    Talaka ikaidhinishwa ndoa ikadondoka
    Baba akapata uchungu likamshukia rungu
    Kisha mama akaonyeshwa fungu akachota
    Afya ya mama ya uchumi na mwili vikanawiri
    Akawa Malkia mji ukatabiri
    Baba akawa kama kifaranga kwenye mvua
    Bado alimpenda mama na mama hakujua
    Mama aliitwa Superwoman ama soja
    Aliushinda usaliti aliushinda ugonjwa
    Baba alimkosa mama kwa starehe ya usiku mmoja
    Alimpenda mama hivyo kumpoteza maumivu tosha
    Washiriki wa biashara walimweka kapuni
    Akafukuzwa kazi asiharibu sura ya kampuni
    Vikundi vya kina mama walisherekea kombe
    Dingi aliipoteza kazi akaisogelea pombe
    Hakuwa sawa kichwani aliishiwa Energy
    Hakukuwa na counseling hakukuwa na Remedy
    Zaidi Makala zilizoandikwa na Mafeminist
    Pesa zilimwisha mtaani alifuga Enemies
    Magazeti hayakuandika alivyokuwa hero
    Yaliandika matusi yaliyomzidi kilo
    Aliitwa Malaya shenzi katili
    Mwanahizaya mwenye cheti cha ujangili
    Na yakapiga millions
    Hakukuwa na vyama vya wanaume kumtetea baba wakasema ana pepo la uzinzi
    Ustawi wa maisha yetu ulipotea ghafla
    Wanasheria wakala na pesa za ushindi
    Aliumia peke yake Dunia ilimweka peku
    Dhambi ilimwacha uchi hadharani
    Alifanya mema zaidi ya kumi hayakutosha awe Yesu
    Ila baya moja aliitwa Shetani Alizubaa
    Alizubaa na akashikwa na madoa
    Alikuwa shujaa ila alishindwa kujiokoa
    Mwamba wa nyenzo ya katikati ulipoondoka
    Ilimaanisha ni muda wa Safina kudondoka huh
    Hazikusikika sifa zake njema
    Machozi hayakusafisha jina lake tena
    Haiba alizokuwa nazo hazikuvutia kamwe
    msongo nao wa mawazo ukamvamia Mfalme
    Aliandika barua ya hadithi yake
    Akisema kilichomtesa sio dhiki yake
    Bali ni uzito wa alichokifanya
    Alijiua kando ya bahari uliokotwa mwili wake

    • @umodernize4142
      @umodernize4142 ปีที่แล้ว +5

      You

    • @alphanlukombe3774
      @alphanlukombe3774 ปีที่แล้ว +11

      Hii kali sana hili ni fumbo tuliolielewa watu wachache sana nakubali sana dizasta vina katika uandishi wako mtu akisikiliza juu juu anaweza akaona kawaida lakini hii Ngoma umeimba mambo makubwa sana kwa sisi waelewa dizasta vina on top

    • @reganmmasi1246
      @reganmmasi1246 ปีที่แล้ว +10

      Sasa mkuu mbona pale spotify kama umetutenga hiv...😕😕

    • @jebajr
      @jebajr ปีที่แล้ว +6

      Always upo tofauti sana na hawa wasanii wetu, wewe ni sanaa.

    • @dizastavina
      @dizastavina  ปีที่แล้ว +8

      @@reganmmasi1246 ipo njiani

  • @braintease1o6
    @braintease1o6 ปีที่แล้ว +18

    Wimbo wa dakika 8, hauongelei siasa wala mapenzi... Story fulani iliyotilia kuhusu familia. Dizasta Vina is the Legend🔥

  • @stonestz8815
    @stonestz8815 ปีที่แล้ว +11

    Dizasta dizasta dizasta ndo toleo la mwisho la viumbe aina ykooo

  • @nillyjos1203
    @nillyjos1203 ปีที่แล้ว +9

    Daah kaka Tanzania nsima wew Ndo msani Bora Tanzania nzima

    • @allysaleh2220
      @allysaleh2220 2 หลายเดือนก่อน

      Huyu ni msanii wa dunia sio tanzania2 jamaa ubongo wake sio wakawaida

  • @reeckstar931
    @reeckstar931 ปีที่แล้ว +10

    😭😭 kwanini wa bongo hawaamki kumpa sikio dizasta

  • @rogathpanga
    @rogathpanga ปีที่แล้ว +4

    Yaah Nilimfahamu baba alikuwa jasiri

  • @shehakudura3243
    @shehakudura3243 ปีที่แล้ว +4

    Aisee kwenye taswira ya kifamilia,,,, W,ume tujipe Poole,,, coz hakuna mafanikio ya watoto na family kiujumla bila Baba kusmama vyema,,,
    Ila aisee shiida ya UMUHIMU WETU kutoonekanwa na kuthaminiwa na KUTENGWA kwa KOSA Moja aisee,,,
    INAUMAA SANA....

  • @renatusmsakula4746
    @renatusmsakula4746 ปีที่แล้ว +3

    Anaetaka kujipima na wewe hatokua SAFE yaani no body is safe!!!

  • @kaissalum7364
    @kaissalum7364 ปีที่แล้ว +6

    Duh bro sina mengi ebu weka namba Nikutumie chochote kitu nakukubali sana

  • @joshmangi
    @joshmangi ปีที่แล้ว +4

    Hizi juhudi zinahitaji malipo, weka lipa namba watu wachangie hizi juhudi.

  • @reeckstar931
    @reeckstar931 ปีที่แล้ว +9

    All way from Switzerland 🇨🇭🇨🇭🇨🇭 nnasubili chakula Cha ubongo

  • @Mr.Kibabu
    @Mr.Kibabu ปีที่แล้ว +16

    Dizasta hajawahi niangusha, Kichwa kweli kweli, Huwa na Like kwanza ndio naanza kusikiliza, Msanii wangu Bora wa HIP HOP

  • @shariffahmad8705
    @shariffahmad8705 ปีที่แล้ว +7

    Kama messi alipata alichostahili kwa miaka yote hiyo amini ndugu yangu utapata unachostahili one day keep it on unajua mpaka unajua tena akili mingi mtu wangu

  • @johannesjoseph7496
    @johannesjoseph7496 ปีที่แล้ว +6

    Hakika unadhihirisha kwamba unaishi kwenye dimensions ambazo miungu ndo inasettle.....
    Hatia 1-5 zote mwisho wa siku lazima ujiulize nani alikosea zaidi..kila muhusika anakua na excuse ya kutenda makosa ijapokua uwezo wa kuyaipuka unakuepo japo mdogo kulingana na mazingira,
    I salute you our best storyteller the verteller

  • @selemaniselemani591
    @selemaniselemani591 ปีที่แล้ว +2

    Haichoshi kusikiliza Leo hii ni mara ya 16 bado Radha ni ile ile Kama ile Ngoma ya tattoo ya asili bro wewe ni nyoko naomba nikusifie kabla hijafa wewe ni nyokooooooo🔥🔥🔥🔥

  • @alimkumba9459
    @alimkumba9459 ปีที่แล้ว +3

    mtu yeyote anamsikiliza dizastar naamini hatoweza kuupoteza mziki wa huyu mwamba kwenye kuta za sikio zake nahisi huyu sio mtu wa sayari hii

  • @richardmloha1762
    @richardmloha1762 ปีที่แล้ว +5

    Jamaa n anaumiza ndongaa wazee kwanin lakin ngoma Kama hizi watu wake wanashindwa kuwa na maslahi yanayoendana na hustles zaoo daaah 😓 em sisi mashabiki tuanze na hii ngoma iangalie ata Mara 5 utatisha sanna let's go

  • @ablemuxic7334
    @ablemuxic7334 ปีที่แล้ว +15

    Kwa mwaka huu hii ndo nyimbo yangu bora ahsante Sana D 🔥🔥

  • @valencepaul4604
    @valencepaul4604 ปีที่แล้ว +2

    Uliletwa kwa ajili ya HIP HOP wengi wamefichwa wewe ni nani ila ni zaid ya rapper zaidi ya mwalimuu wa jamii,,,,napo play ngoma zako hadi wazee wanauliza huyu ni nani😀💥💥UNAJUA SANA MIMI NI MFUASI

  • @mtaaruma
    @mtaaruma ปีที่แล้ว +2

    Kweli mazuri kumi hayawezi kufanya uitwe Yesu but baya moja utaitwa shetan
    The game is in yourself hands prf tungo

  • @petercharles8572
    @petercharles8572 ปีที่แล้ว +5

    Kwenye harakati za kumpandisha mwanamke kuwa sawa na mwanaume zimekuwa harakati za kumkandamiza sana mwanaume na sio tena kumuweka mwanamke awe sawa na mwanaume...
    Dizasta ametuonyesha jinsi mama alistawi kutokana na dunia nzima kuwa upande wake na baba hakusikilizwa.
    This man deserve 01, Ni jambo la kujivunia kuwa wakati mmoja na dizasta vina... Bahati mbaya kwa wote waliotamani kumsikiliza msanii kama huyu ila hawakufanikiwa kwasababu waliku past na records hizi mustakabari mzuri kwa kizazi kijacho.
    We love you Dizasta Vina

    • @dizastavina
      @dizastavina  ปีที่แล้ว +1

      Feeling is mutual, cheers

  • @erastompongo8400
    @erastompongo8400 ปีที่แล้ว +3

    Duuuh we jama ni mnoma sana wangapi wanailudia rudia

  • @idmpros
    @idmpros ปีที่แล้ว +1

    nomaaaa sasa @dizastavina wewe upo mbeleeee sanaaaaa ya Muda Trust me watu ni kama hawakuoni BUT I BELEAVE IN GOD TIME WATU WATAKUZINGATIA KWA KISHINDO

  • @isdoryemily5029
    @isdoryemily5029 11 หลายเดือนก่อน +2

    Uyu mwamba amejua kunibadirisha sinaga mshauri nyimbo zake nikisikia najifunza na mtaani naitwa Hip Hop culture

  • @sabagumasanja8001
    @sabagumasanja8001 ปีที่แล้ว +2

    Mm namlaumu sana dada wa kazi😥😥😣

  • @MoreWarzone
    @MoreWarzone ปีที่แล้ว +2

    Kaka we tukujengee sanamu tuu … unajua kuandika

  • @Makavelithedon2086
    @Makavelithedon2086 ปีที่แล้ว +10

    *Dizasta Vina ni moja kati ya best lyrical rapper kuwaikutokea Tanzania*

  • @morganmwaikusa8194
    @morganmwaikusa8194 ปีที่แล้ว +3

    Genius.... Huyu Edgar anajua mpk anakela yan....

  • @odiloodilo
    @odiloodilo ปีที่แล้ว +2

    Me nishabiki yako sik zote, kaka upo vizuri sana 👍💯💯💯💯🙌

  • @erickpaschaljr8667
    @erickpaschaljr8667 ปีที่แล้ว +3

    Ninamshukuru Mungu kwa zawadi ya mziki mzuri wa Dizasta vina yawezekana sisi ni watu wenye bahati sana ila bado hatujatambua thamani ya utunzi usio wa kawaida.

  • @Jumajing
    @Jumajing ปีที่แล้ว +8

    Hii ni zaid ya Wimbo bora wa Mwaka kaka, Funzo,Vina na 🔥🥂

  • @mkanganails5839
    @mkanganails5839 ปีที่แล้ว +1

    Daaa aisee unabalaa zito wewe una hatareeee mwamba

  • @mr.theory5871
    @mr.theory5871 ปีที่แล้ว +1

    Oyaaaaa mwamba anaandika hadi anaandika tena,cha ajabu tuzo kwa wanaosifia ngono!

  • @AmisiHassaniTygo
    @AmisiHassaniTygo ปีที่แล้ว +2

    Daahh, kuna watu wana Chana nyie

  • @jacksonkitosi6504
    @jacksonkitosi6504 ปีที่แล้ว +2

    Kwann nilichelewa kumjua huyu mwambaa brother be blessed 🙏
    🔥 🔥 Unajua sanaaa

  • @jaymbawal249
    @jaymbawal249 ปีที่แล้ว +2

    Dizasta vina mkali san kam una mfatilia 🔥🔥🔥🔥 sikuping broo

  • @braytonedaniely7977
    @braytonedaniely7977 ปีที่แล้ว +2

    Tym yako ndo hii mwanetu utaeleweka tu siku moja✌

  • @bennyblac0621
    @bennyblac0621 ปีที่แล้ว +1

    Daaah ww dizasta ni mtu wa aina gn na unafikira gn aiseee daaah napata ile ladha ya mziki na fikra ambazo havizungumziwi kwenye mziki huuuu aisee

  • @g_eazmusic1329
    @g_eazmusic1329 ปีที่แล้ว +4

    Kosa moja mtu anasaau wema wote

  • @ibrahimukasimu3386
    @ibrahimukasimu3386 ปีที่แล้ว +1

    Kaka shikamoo we unajua mpaka nawaza kuwa haujatoka latina hii planet dah uno amor amigo god bless u on ur evry step of ur lyfe

  • @abdulkara2327
    @abdulkara2327 ปีที่แล้ว +2

    Kutoka Zanzibar kama unamkubali dizasta gonga like mwanangu kumaanisha huyu jamaa ni mwamba

  • @dedeayew9650
    @dedeayew9650 ปีที่แล้ว +1

    Ambae hatapenda hizi lyrical aisee huyo hajui music

  • @sayedkhamis5204
    @sayedkhamis5204 ปีที่แล้ว +7

    Bro una akili Kubwa wewe sio msanii wewe sio Mwana Muziki wewe Ni Legendary wa Maandishi, sauti na Midundo The Story Teller Never Seen Before Keep Pushing Vinna

  • @mansourabdul3902
    @mansourabdul3902 ปีที่แล้ว +2

    Keep it up aisee unaandika leo ndio mara yangu ya kwanza kuusikiliza na kukujua ila sasa nihesabu kama shabiki yako sasa

  • @Lukona639
    @Lukona639 ปีที่แล้ว +1

    Dah sijui kwanini nimeusikiza...Nimeishi katika hyo mistari kama natazama movie...Umeniacha na Majonzi mjomba but...Yeah Nilimfahamu baba alikua jasiri....Wapo waliozijua sifa zake....Mtaani halikuanzikwa jina lake.....Alifanya mema zaidi ya kumi hayakutosha awe Yesu...Ila baya moja aliitwa Shetani Alizubaa...WOW

  • @mbarakamngayunga9558
    @mbarakamngayunga9558 ปีที่แล้ว +64

    Daaaah,aisee sikutegemea kama ningekutana na idea kali kama hii...wewe brother dizasta ubarikiwe sana...Nyimbo zako zinanifunza sana❤

    • @octavian54
      @octavian54 ปีที่แล้ว +4

      Unafelii wapi huyo ndio Mwenye mziki wa hip hop

    • @amalillahasante6693
      @amalillahasante6693 ปีที่แล้ว +1

      Kweli mwanangu.

    • @babamasakalanga5687
      @babamasakalanga5687 ปีที่แล้ว +4

      Daaah hii ngoma imenitoa chozi nimekumbumbuka mbal sana😭😭😭😭😭

    • @idrissachisigwa5360
      @idrissachisigwa5360 ปีที่แล้ว +2

      Noma sana

    • @shehakudura3243
      @shehakudura3243 ปีที่แล้ว

      @@babamasakalanga5687 for real Yani inaniumiza sana hii ngoma aisee,,,,
      W,ume thamani yetu mbinguni ila tunavuja Jasho hatari lakin mwishoe tunaambulia kisukari na presha

  • @rahimtz6794
    @rahimtz6794 ปีที่แล้ว +2

    Bro unajua sana hii ndo maana halisi ya kipaji

  • @saadatmsuya293
    @saadatmsuya293 ปีที่แล้ว +2

    Kaka unajua🙌🙌🙌🙌🤝🤝😭

  • @filbetdaud4597
    @filbetdaud4597 ปีที่แล้ว +2

    mamaeh aisee iki n kichwa na nusu aiseee Mzee D unaandika sana unaandika sanaaa kaka unaandikaaaa nasemaaa unajuaaa sanaaa D ish sana mflame D

  • @hassanmakweto6299
    @hassanmakweto6299 ปีที่แล้ว +1

    Yeah hii ndio mind food💪💪💪 afu kweli rapcha abishana na kaka zake kama hawa?

  • @danielmbilinyi4025
    @danielmbilinyi4025 ปีที่แล้ว +2

    Huaga najaribu kuandika mistari ila nikimsikiliza Dizasta vina najiona siandiki kabisaaa

  • @Amisa8899
    @Amisa8899 ปีที่แล้ว +1

    Uyu dah mtu mbadi

  • @dickmlawa8843
    @dickmlawa8843 ปีที่แล้ว +1

    Asante kwa kunipa jibu D ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

  • @MasasiVisionTv
    @MasasiVisionTv ปีที่แล้ว +3

    DIZASTA VINA 🙌🏿 usiku mmoja umebadili fomat yoot y maisha duh 😔

  • @openmindtz
    @openmindtz ปีที่แล้ว +1

    Too pain nais kama ni mm ndo baba... life is so complicated aliitaj faraja pale penye uzito ubinadam ukampoza sasa ana onekana zito... rest in peace baba na ukiangalia in really life ma baba weng wana fight sana bt they would never let a sight on us

  • @yusufuselemani6339
    @yusufuselemani6339 ปีที่แล้ว +2

    Good work kutoka kwa narrator bora wa mda wote,
    Sema D humu na muona hayati kabisa kazungumziwa 😀😀

  • @hurumamwankuga6663
    @hurumamwankuga6663 ปีที่แล้ว +2

    Style yako Ime inspire rappers wengi but hiyo hiyo style Iko tofauti na wao bcz unavyotema na wanavyotema there are so different 👐👐

  • @kennethmbilinyi4171
    @kennethmbilinyi4171 ปีที่แล้ว +1

    Sinachakusemaa Mzee niutamuu tuu great

  • @ShabaniAbdi-q1w
    @ShabaniAbdi-q1w 3 หลายเดือนก่อน +1

    Nomaaa sanaa

  • @braytonemmanuel4915
    @braytonemmanuel4915 ปีที่แล้ว +1

    we dizasta mtu mbaya

  • @eliamhiro4737
    @eliamhiro4737 ปีที่แล้ว +1

    Huyu jamaa nilikua simjui asee

  • @ahmedramadhani1264
    @ahmedramadhani1264 ปีที่แล้ว +6

    Binafsi nimeisikiliza zaidi ya mara tano kwenye simu na bado naendelea kuisikiliza. Noma sana hii kitu.

  • @jumazinga941
    @jumazinga941 ปีที่แล้ว +2

    Ama kweli baba atabaki kuwa hero

  • @kioochafasihi
    @kioochafasihi ปีที่แล้ว +1

    Dizasta na mimi ni miongoni mwa madini adhimu kabisa kwenye kiwanda cha Hiphop ya Afrika (swahili rap)

  • @GladMzava-y7v
    @GladMzava-y7v ปีที่แล้ว

    Huyu ni kiumbe alietokea sayari nyingine naeza Sema vinus au jupiter au Mars Mr dizasta ni genius by nature sio tu kipaji ulicho nacho umebalikiwa hekima na bahati

  • @brainfigure94
    @brainfigure94 ปีที่แล้ว

    Noma sana hatusemi sana kazi nzuri inaonekana pongezi kwa mchora kartoon

  • @ausiissa7155
    @ausiissa7155 ปีที่แล้ว +1

    Kuna mda uwa nikisikiliza nyimbo zako nikisema unajua naona Haitoshi inabidi tu niwambie wasio kujua kwamba unajua ili wao pia wakatoe ushuhuda ✨✨Mungu akuweke sana kaka✨✨

  • @yohanidimoso3711
    @yohanidimoso3711 ปีที่แล้ว +2

    Mpeni Dizasta crown yake ya story telling

  • @originalnchimbi7360
    @originalnchimbi7360 ปีที่แล้ว +1

    Daaah nyimbo nzuri

  • @raphaelmwangosi9295
    @raphaelmwangosi9295 ปีที่แล้ว +2

    Kak daaaaaaaa cjui tusemeje mwanang ila bc wameweka tasnia chino ila tunakuexhmu 💪💪💪🥰😍🥰🥰🔥🔥🔥💥💥💥

  • @GeofreyGeorge-ii8cm
    @GeofreyGeorge-ii8cm ปีที่แล้ว +1

    Naisikiliza kila saa... Hii ni ngoma na nusu aiseeee

  • @vianneysospeter2235
    @vianneysospeter2235 ปีที่แล้ว +1

    Mwenyewe hip hop yake huyu hapa

  • @octavianmushi928
    @octavianmushi928 ปีที่แล้ว +2

    Bro Mungu akubariki kwaelimu ya bure uliyotupatia... Mungu akulinde sana...🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻

  • @mosesshayo1733
    @mosesshayo1733 ปีที่แล้ว +1

    Sina uwakika na ao unaobato nao dizasta Bato na mm utawaua wee wa az zangu

  • @worldhappiness1181
    @worldhappiness1181 ปีที่แล้ว +1

    Mwandishi Bora wa Muda wote Tanzania

  • @amanikito6252
    @amanikito6252 ปีที่แล้ว +1

    Asee huyu jamaa ni hatari sana

  • @kiondosaimon6149
    @kiondosaimon6149 ปีที่แล้ว +1

    Always de Best unajua sanaaa mzeee hakuna wa kushindana na ww Bongo hapa 👊👊👊

  • @xylomyxdisophie2011
    @xylomyxdisophie2011 ปีที่แล้ว +2

    broo surely ww n msanii ulienitoa kwa life moja kwenda step nyingin......

  • @StimaOfficial
    @StimaOfficial ปีที่แล้ว +1

    Sijawah kuchoka kuzipakua na kuskilz hizi punch
    mzee wa Panorama
    Professor Tungo💪💪💪

  • @derrikdesertman4564
    @derrikdesertman4564 ปีที่แล้ว +1

    Aiseee hii akili nyingi ya huyu jamaa ni noma sana..
    Trakii kalii sana Dizasta Vina.

  • @obbyentertainment4303
    @obbyentertainment4303 ปีที่แล้ว +1

    Huyu jamaa ni hatari sana

  • @imanyjohn1755
    @imanyjohn1755 ปีที่แล้ว +1

    We si Mbuzi (g.o.a.t)tena,We ni Simba.

  • @johnngowi8334
    @johnngowi8334 ปีที่แล้ว +1

    Noooma sana aisee , wew ni mkali saaana hapa bongo unandika sanaaaa⭐⭐⭐⭐💥

  • @rajabmpamwa9051
    @rajabmpamwa9051 ปีที่แล้ว +1

    Sasa naelewa kwann kwenye jina lako umemalizia neno vina ...

  • @FUNNYVIDEOS-ek1cm
    @FUNNYVIDEOS-ek1cm ปีที่แล้ว +1

    Dizasta Hakuna nyimbo yako ambayo sina kaka God bless your Talent

  • @revocatusnzungu6580
    @revocatusnzungu6580 ปีที่แล้ว +3

    Ningekua mwalimu wa kiswahili nyimbo za Dizasta zinastahili kufundishia kabisaaa ......na kama nikija kuwa waziri wa elimu nyimbo za Dizasta zitatumika shule za sekondari na elimu ya juu kufundishia

  • @kiuyl0
    @kiuyl0 ปีที่แล้ว +1

    Binafis naomba hii hatia tupewe Ep Au albam kiukwel ni bonge LA idia

  • @jovinj7888
    @jovinj7888 ปีที่แล้ว +1

    Moto ushawaka tuote sasa.

  • @ngomesaidi1754
    @ngomesaidi1754 ปีที่แล้ว +1

    Unafaa kuitwa teacher dizasta,,,,tunangoja mwendekezo wa sehem ya 6

  • @hajimaster7624
    @hajimaster7624 ปีที่แล้ว +2

    Kichwa chenye madini makini kila ninapoona umerelease kitu najua ninacho chakujifunza✍

  • @bbooster06
    @bbooster06 ปีที่แล้ว +1

    Dah much respect broo nii story kalii kinoma sanaa imepenyaa hiii