MAJALIWA "Haiwezekani Mfanyabiashara wa Kariakoo unadai barua ya Rais Samia kupeleka TRA hii dharau"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 14 พ.ค. 2023
  • Mheshimiwa ameiagiza TRA kusitisha matumizi ya kikosi kazi ambacho kilikuwa kinafanya kazi ya ukusanyaji wa kodi katika eneo hilo “Task force hii ndiyo inaendesha kamatakamata kila siku, Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA naagiza isitishwe, kanuni zipo, sheria zipo zinatuelekeza namna ya kulipa kodi, kamatakamata hii inafukuza wafanyabiashara Kariakoo na mbaya zaidi mnawakata hadi wageni kutoka nje”
    Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa TRA wanaosimamia ukusanyaji wa kodi katika eneo hilo na nchini kote kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya namna bora ya ukusanyaji wa mapato na kuacha kutumia nguvu wanapo tekeleza majukumu yao.
    Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameahidi kukutana na wafanyabiashara hao Mei 17, 2023 kuwasikiliza na kutatua changamoto zao ili kuwa na suluhisho la kudumu.

ความคิดเห็น • 4