MJUE MAHARAGE CHANDE NA ALICHOWAI KUAMBIWA NA RAIS ALIVYOTEULIWA TTCL NAKUPELEKWA SHIRIKA LA POSTA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 ต.ค. 2024
  • Licha ya historia nzuri na sifa lukuki za utendaji, alipokuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), katika wadhifa wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania hali imekuwa tofauti.
    Huu ndiyo uhalisia wa historia ya Maharage Chande katika kuzitumikia taasisi za umma tangu Septemba 2021 alipotoka sekta binafsi.
    Safari ya Chande katika mashirika ya umma ilianza Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alipomteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco.
    Kuingia kwake Tanesco, kulimfanya awe mmoja wa wakurugenzi waliopata kusifiwa na mkuu huyo wa nchi, hasa kwa kile kilichoitwa mageuzi ya kidigitali ndani ya shirika hilo.
    “Mwezi uliopita nilishiriki mkutano wa Posta pale Arusha nikakuta maendeleo makubwa kwa upande wa Posta yetu wanakwenda kidigitali na nikajua hayo ndiyo maeneo yako (Chande).
    “Kwa hiyo kwa sababu ni maeneo yako na nimemkuta kijana mzuri wa Posta ya kidigitali nikaona ninyi mkiwa pamoja mtafanya kazi nzuri, kwa hiyo nenda kamsaidie mkuze Posta yetu iende kidigitali,” alieleza Rais Samia baada ya kumwapisha Chande katika wadhifa wa Posta Masta Mkuu.
    Sifa na matarajio hayo yamefifia Julai 23, 2024, baada ya taarifa ya utenguzi wa Chande katika wadhifa wake pamoja na watendaji wengine katika taasisi mbalimbali.
    Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, waliotenguliwa ni Chande, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ulanga na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba.

ความคิดเห็น • 3

  • @zefamange7281
    @zefamange7281 2 หลายเดือนก่อน

    MAMA MBONA ULISHA KATAZWA NA MAGUFULI KUHAMISHA MAJIZ?

  • @ilynpayne7491
    @ilynpayne7491 2 หลายเดือนก่อน

    Huyu ndo alifanya mgao wa umeme ukawa balaa😅