Salama Na WALTER CHILAMBO SE6 EP59 | HABA NA HABA PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 ต.ค. 2024
  • #SalamaNa #SendTip MPESA #5578460
    Pengine jina la episode hii linaweza likakupa muangaza kidogo wa story fupi ya maisha ya mgeni wetu wa wiki hii kwenye kiti chetu chakavu na meza ya kigae ambaye leo hii tayari kashaona, tochi ya maisha kwake inamulika tu vizuri na mbele anapaona. Huyu ni Walter Chilambo ambaye miaka tuseme 14 iliyopita alikua hana uhakika wa chakula chake cha siku tu achana na sehemu gani atalala. Ruka ruka ya kule na huku na bahati ya kupendwa alonayo na ambayo inaendelea mpaka leo naamini inakuja kwasababu ya ukarimu wake na hii ndo silaha yake yenye makali ambayo inampeleka mbali mpaka leo hii
    Kama mtoto wa kiume ambaye unatakiwa kwenda kujitafuta ki maisha Walter nae ilibidi afanye yale yale ambayo si watoto wa kiume tu ila wengi wetu tumefanya ya kutaka kwenda kutafuta chako, na yeye aliona basi bora afanye hivyo. Safari ya kuja town kutoka mkoani anatuhadithia kwa upana kwenye episode hii. Mtu ambaye alimpokea ni mwana tu ambaye alienda nae shule moja, stop ya kwanza? Keko Magurumbasi. Na si kwamba alikua hana Ndugu hapa Dar es Salaam yeye alijiamulia isiwe hivyo, ilikua ngumu kumshashiwi Mama yake ambaye alitaka kujua ramani nzima ya mwanae ambaye alikua anakuja mjini kwa mara ya kwanza. Baada ya kufanikiwa kushawishi Mama Walter, kijana alipewa nauli na ananiambia by the time anafika Dar alikua na shilingi ELFU MOJA TU kwenye mfuko wake, hapo ni Ubungo kwenye stendi ya mkoa
    Imani yake kwa Mungu wake pia ni silaha ya pili ya Ndugu Walter Chilambo. Hii ndo ambayo kwa mujibu wake imemsaidia kumvusha na mengi, maisha huko Keko hayakua mazuri, sikutaka kutumia neno si kama alivyo yatarajia maana hata yeye hakua na matarajio yoyote kwasababu alikua hajui anakutana na mazingira gani wakati anaenda kwa mwanae huyu aliyesoma nae Sekondari ambaye walikua na majina ya Baba yanayofanana. Mwenzetu anaitwa Michael. Alikaa pale huku akiwa anajaribu kuji tafuta ila kila anachogusa kilikua cha moto. Ananihadithia jinsi alivyoanza kufanya kazi za kila siku ili angalau apate hela ya kula, kule kwa Mama alikua anajifanya kama kila kitu kinaenda vizuri kwahiyo hata vimzinga vidogo vidogo vilikua haviendi. Ulipofika wakati wa yeye na mwanae Michael kufunguana mashati maana alikua ashakaa saana na hana dira nzuri hapo sasa ndo kila kitu kilianzia.
    Unadhani mmoja anaweza kuwa na bahati kiasi gani kwamba mtu ambaye aliombwa amhifadhi kwenye ghetto lake wakati yeye anatafuta ustaarabu mwengine kuwa ni Ndugu yake? Pengine hii hutokea kwa wenye BAHATI TU, pengine Walter ni mmoja ya watu hao maana baada ya kujulikana hilo ndo angalau kukawa na ahueni ya kuwa na uhakika wa sehemu ya kuegesha mbavu, hii ni moja ya sehemu ilonisisimua kwenye simulizi yake, imagine mtu anavyokua kapigika alafu kutoka ambako hakujulikani mtu ambaye ameombwa akuhifadhi kwa muda anatokea kuwa ni Ndugu yako, hii ni Mwenyezi Mungu pekee ndo ambaye anaweza KUTENDA na kama utakua ushawahi kuishi kama ndege ambaye hajui analala wapi basi wewe utaweza kuelewa zaidi hapa.
    Walter Chilambo ni mshindi wa Bongo Star Search wa mwaka 2012 na baada ya kushinda alianza safari yake ya muziki rasmi. Safari yake haikua ya urahisi kama ambavyo naamini alitarajia au sote tulidhani. Kiwanda cha Bongo Flava ki usalama tunaweza kusema kina wenyewe na ukiwa mpya kabla hujajua fagio lipi ndo linafaa kusafishia wapi basi kazi utakua nayo. Kwa Bwana Chilambo ambaye alishinda taji na pesa hakukua na tofauti kabisa. Neema kwa upande wake ilianza kuonekana baada ya yeye kuamua kufanya mziki wa kumtukuza Mungu na baada ya hapo mengine ni story tu.
    Kwahiyo NINI hasa kilimfanya afanye maamuzi hayo? Kwenye kipindi ambacho kila mmoja ameamua kuimba nyimbo za mambo ya kitandani na mambo ya ndani je yeye kwanini aliamua kubadilisha gea? Maana Kama sauti anayo na kuandika anajua sasa sababu ni nini? Na pia wasiwasi wangu uko kwenye baada ya ‘kutoboa’ huko aliko na kupata umaarufu na sifa tele hatorudi tena huku kwenye kuimba nyimbo za kuachwa na kupendwa na kutendwa? Ana uhakika kiasi gani? Ukichukulia kama kuyaona na kuyafanya basi ashafanya mengi?
    Nataka nikuachie hapa kwa leo ili uweze kwenda kuskiliza na kuya enjoy maongezi haya na mwanangu huyu ambaye hajabadilika, bado mcheshi, mwenye heshima na anayejitambua. Natumai hadithi yake itaku inspire kwa vile ambavyo ningependa iwe.
    Amina.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

ความคิดเห็น • 36

  • @blandinamyinga9489
    @blandinamyinga9489 ปีที่แล้ว +4

    Salama sitakaa niisahau cku uliyomwambia Walter kwamba ungekuwa na uwezo ungemtia mfukoni watu wakakutunza hela ♥️daaah long time.

  • @imasigaro2968
    @imasigaro2968 ปีที่แล้ว +7

    Maisha yakukua bila upendo wa baba zetu yanatugusa wengi ,Mungu awabariki wakina mama wote dunia ,endless love from them ❤️

  • @newtonmnyack9729
    @newtonmnyack9729 ปีที่แล้ว +1

    Nakukubali Sana mdogo wangu ila nilifurahi Sana kwa Mara ya kwanza nisikia ukiimba Asante kwa ajili ya kumshukuru MUNGU nikaona hapo ndio mahali sahihi MUNGU akubariki Sana kwa Hilo nakutakia mafanikio mema. #andazi maji ya kandolo,.

  • @Bob-kz2ql
    @Bob-kz2ql ปีที่แล้ว +2

    😅😅😅Salama never stop to amuse us na intro zake asee this is powerfull…Walter keep going,kuimba gospel inataka moyo in terms of payment shows nn ila uko vizuri God bless you mpendwa

  • @zebedayomshani
    @zebedayomshani ปีที่แล้ว +4

    Watu wa mungu ni wa kweri mno hongera brother 💪

  • @blandinamyinga9489
    @blandinamyinga9489 ปีที่แล้ว +2

    ""Umenitoa mbaali kusikojulikanaa"""I loooove this"kama wewe ulifuatilia BSS ya Walter utaelewa maana ya huo mstari wa huo wimbo hapo mwanzo"meeeen these 2🤣🤣🤣🤣

  • @blandinamyinga9489
    @blandinamyinga9489 ปีที่แล้ว +1

    Preach Walter preach""we forgive for our own healing n not for their wrong doing.

  • @elia5475
    @elia5475 5 หลายเดือนก่อน

    Ubarikiwe sana blaza

  • @Heavyweight1111
    @Heavyweight1111 ปีที่แล้ว +6

    Wa5 leo Nipeni like zangu

  • @ArexIsack-ex9pt
    @ArexIsack-ex9pt ปีที่แล้ว

    God bless you salama

  • @mountaincoffee7
    @mountaincoffee7 ปีที่แล้ว +1

    Golden voice

  • @namelockmaasailady8002
    @namelockmaasailady8002 ปีที่แล้ว

    I love you my lovely sisy salama💞💞💞you are doing great.

  • @doreen9516
    @doreen9516 ปีที่แล้ว

    Ubarikiwe sana Walter! 🙏🏾

  • @musambaruku6661
    @musambaruku6661 ปีที่แล้ว

    Salama Na ❤❤❤

  • @isayamandevu833
    @isayamandevu833 ปีที่แล้ว

    Aisee mimi ni shabiki yako, napenda namna unavoeka page zako za mitandao ya kijamii kwa upekee , na napenda mengi ambayo mengi SIWEZ sema APA
    But ninakuomba umlete na pastor Myamba

  • @lowkeybongo
    @lowkeybongo ปีที่แล้ว

    Bomang’ombe ❤️🔥

  • @amoogaza6825
    @amoogaza6825 หลายเดือนก่อน

    Nipo hapa 26.8.24 😊

  • @marrymchaki9025
    @marrymchaki9025 ปีที่แล้ว +4

    Nani anakikubali salama ....anipe like zangu apa

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว

    🙌🏿

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    🙄🙄😳😲😲😲2019 au nime sikia vibaya??????????

  • @ibrahimzuberi1029
    @ibrahimzuberi1029 ปีที่แล้ว

    Wakwanza

  • @emmanuelywambura2006
    @emmanuelywambura2006 ปีที่แล้ว

    Mshikaji wake na reivani wanatoka mtahaaaa mmoja na Mimi ndio mtu wa kwanza kurekodi kazi zao dar most record pumbavu

  • @emmanuelywambura2006
    @emmanuelywambura2006 ปีที่แล้ว

    Pumbavu namjuwa huyooooo muongoooo mpumbavu Sana uyu dad's salama sio mlokole no Kiki mpumbavu Sana namjuwa mungu wangu Mimi namjuwa toka anamiaka 0

    • @josephk90
      @josephk90 ปีที่แล้ว +1

      Alikukosea nini mkuu mbona unamchukia mno?

    • @luogafrank3205
      @luogafrank3205 ปีที่แล้ว

      Jamaa kashaokoko na demu wako alikuachia mbona kitambo tu move on jamaa

  • @emmanuelywambura2006
    @emmanuelywambura2006 ปีที่แล้ว +1

    Pumbavu namjuwa huyooooo muongoooo mpumbavu Sana uyu dad's salama sio mlokole no Kiki mpumbavu Sana namjuwa mungu wangu Mimi namjuwa toka anamiaka 0

    • @veronikabaraka3315
      @veronikabaraka3315 ปีที่แล้ว

      Nan muongo Sasa hapo

    • @mariajoseph9735
      @mariajoseph9735 ปีที่แล้ว +1

      Si ameshakwambia aliamua kubadili mwenendo wa maisha yake

    • @miriamumbwilo164
      @miriamumbwilo164 ปีที่แล้ว +1

      Annoying comment🚮😏😏
      Et sio mlokole bro..are you God? Who are you to judge...eniwei akili🤌

    • @liducakes2803
      @liducakes2803 ปีที่แล้ว

      ​@@miriamumbwilo164 100%

    • @luogafrank3205
      @luogafrank3205 ปีที่แล้ว

      Namjua huyu jamaa kabda ajaokoka alimchukua demu wa emanuely wambura lakin sasa hivi kaokoko