Salama Na GARA B SE6 EP63 | BABA SHUGHULI PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 เม.ย. 2023
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Jina MC Gara B ni miungoni mwa majina makubwa sana kwenye ulimwengu wa kazi ambayo mwenzetu huyu amechagua kuifanya. Familia yake, mke na watoto, wazazi wake na wa mkewe pengine, Ndugu jamaa na marafiki na waajiriwa wake wanakula vizuri kwasababu ya kipaji chake Ndugu yetu huyu. Ni mwanaume ambaye akiwa kazini kwake furaha na burudani ambayo huwapa wateja wake ndo inayomfanya azidi kuenda mbali kwenye tasnia hiyo ya ushereheshaji. Again, yeye ni mmoja ya BORA kadhaa ambao wanafanya kazi kama yake.
    Mtandao wa kijamii ni kitu kimoja chenye nguvu sana kwenye miaka ya hivi karibuni, kwa ushahidi tulonao tushawaona wengi ‘wakitoboa’ kwasababu ya Instagram au sehemu nyengine. Mitandao iko mingi na kila mmoja na tobo lake la kufikia mjini. Kazi ambayo MC huyu huifanya yeye huenda na team yake kuiweka vizuri kisha ana post kwenye page yake yenye watu karibia MILIONI MOJA NA NUSU. Akizifikisha mjini kazi hizo wengi huvutiwa nazo na ambao wanakua wana shughuli nao bila ya shaka watamtafuta na kutaka kufanya nae kazi. Ubunifu wake ni wa kipekee kutokana na vingi na wengi ambao tumekua tukiwaona kwa miaka mingi sasa. Mtandao wa kijamii umemsaidia na unaendelea kumfanya awe bora zaidi ya jana.
    Sasa, shughuli hii anayo ifanya ndo ambayo ilikua ndoto zake? Pengine alikua huku anamuona mtu fulani akiwa anaifanya hii kazi kwa ufanisi na ikamvutia? Ilikuaje mpaka akaingia huko? Kwa kumtizama haraka haraka tu utagundua Ndugu yetu ni MCHESHI, yeye anapenda kucheka na kuongea, ingawa hapo kwenye kuongea nako sio kiviiiile ila ni mtafutaji ambaye AMETIMIA. Story yake alotupa kwenye episode hii inajumuisha yeye kufanya kazi zaidi ya mbili kwenye kipindi flani hivi cha maisha yake ili aweze kuishi vizuri. Ki professional mwenzetu ni MWALIMU, ambaye hiyo kazi aliifanya hasa, na akaijumlisha na kazi ya huduma kwa wateja pale Tigo na wakati huo huo akawa anafanya kazi kwenye kiwanda kimoja hivi huko Pugu Road, hakua na wa kumdekea wala kumsubiria na hustle yake hiyo ndo ambayo anaenda nayo mpaka leo kwenye maisha yake.
    Sasa kama Baba na mume kwa mkewe kipenzi ambaye naye alikutana nae sehemu ya kazi yake, Gara B ananijibu kuhusu uaminifu ambao anao kwa mkewe ambaye kwa mujibu wangu kama amekutana nae kwenye mazingira hayo, vipi hujiskia kila mara anapokua kazini mumewe ukichukulia huko ndipo walipo kutana na ndo ambapo wanawake wengi wazuri huwepo? Jibu lake lilikua na kuukonga moyo.
    Alituhadhia pia kuhusu wazazi wake na jinsi ambayo ameweza kujitengenezea jina, siku ya kwanza alipopata kimeo cha ku host harusi ya watu ambayo kwa mujibu wake aliibembeleza sana na hakua amepewa nafasi, ila nafasi ilipojileta akanyoosha kwa umbali mrefu mpaka mengine yamebaki story tu. Na hii ndo ilikua simulizi yangu bora kabisa kuhusu kupata nafasi na kuzitumia vyema.
    Yangu matumaini utaskiliza na kuangalia kwa makini maana humu anatupa simulizi zote za kutokata tamaa na jinsi ya kuchukua nafasi, ila pia anatuhadithia baadhi ya mitihani ambayo huja na umaarufu pia na jinsi ya kupambana nayo. Mimi nili enjoy na natumai itakua hivyo kwako pia.
    Happy Holidays.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camSalamaNa
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • บันเทิง

ความคิดเห็น • 36

  • @emmanuelwilson8191
    @emmanuelwilson8191 ปีที่แล้ว +9

    Salama yani katika kipindi chako nimejifunza kuwa ilikutimiza ndoto kubwa yeyote mtu unayoiona ni lazima kujianda vzuri na kukubali kujifunza ili kufanya kiufasaha ile ndoto yako muda ukifika. ulikubali kufanya vipindi vya interview (Mkasi) and hata kuwa judge and now unafanya vzuri kazi yako. hii formula ni ya kuitumia kwenye maisha yangu. Best of luck Salama. Positive vibes

  • @marianajohn5415
    @marianajohn5415 ปีที่แล้ว +4

    Dah nimesikitika sana na ile story! Aisee una mke na nusu❤❤

  • @mbwanamtessa8607
    @mbwanamtessa8607 ปีที่แล้ว +2

    Nakupenda sana dada salama kwa kazi nzuri. Me nakuona wewe ni mtaalam wa mahojiano.

  • @swahiliteacher4255
    @swahiliteacher4255 ปีที่แล้ว +1

    Brother hongera sana uzidi kubarikiwa, Salama dada wa taida... big up sana,

  • @dayana5513story
    @dayana5513story ปีที่แล้ว +1

    Best mc in Tanzania wish you the best ❤

  • @MOJAZAIDI.
    @MOJAZAIDI. ปีที่แล้ว +2

    Salama unafanya kazi nzuri sana.

  • @marrymwalimu1811
    @marrymwalimu1811 ปีที่แล้ว +1

    Namfaham mwanao Jensen,ukimkuta sasa anajitambulisha mi mtoto wa Gara b,anajiita Gara boy.

  • @collinssoundsmusic3182
    @collinssoundsmusic3182 ปีที่แล้ว +1

    There are diff. In filming with motion here. But the show its awesome❤🎉

  • @hermanwenceslaus5497
    @hermanwenceslaus5497 ปีที่แล้ว

    what a character Gara b.....

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว

    Hongera sana garb

  • @ZaituniMuhammed-go4nw
    @ZaituniMuhammed-go4nw 7 หลายเดือนก่อน

    Nlikuwa interview nzurrr ❤❤

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 ปีที่แล้ว

    Gara B,nakukubali sana Bro

  • @knowwithasha
    @knowwithasha ปีที่แล้ว

    brain on point

  • @aloyceshaban1348
    @aloyceshaban1348 ปีที่แล้ว +1

    Dah

  • @HERIETHNATHANEL-pb7ep
    @HERIETHNATHANEL-pb7ep ปีที่แล้ว

    Waaaaah

  • @bettysalvatory9136
    @bettysalvatory9136 ปีที่แล้ว

    Wa kwanza😊

  • @dianerditto
    @dianerditto ปีที่แล้ว +2

    😘🤩🤩🤩

  • @richardsaidi2448
    @richardsaidi2448 ปีที่แล้ว

    🔥🔥🔥

  • @geofreybarama4000
    @geofreybarama4000 ปีที่แล้ว +1

    DADA WA TAIFA NA MC WA TAIFA..

  • @carolineanthony1095
    @carolineanthony1095 2 หลายเดือนก่อน

    ❤❤

  • @luciamsani
    @luciamsani ปีที่แล้ว

    Pc yangu iko vizuri mbona kwa interviews nyingine vinaenda sawa warekebishe bhana hamtaki kuambiwa au mnataka comment zipi jaman?

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    Dada wa Taifa 😂😂🤣

  • @mwanaidimuhindi6671
    @mwanaidimuhindi6671 ปีที่แล้ว

    Anko Michael wa Anitha 😁

  • @nicolenabintu2509
    @nicolenabintu2509 ปีที่แล้ว +1

    Gara whaaaat 😅🔥 ila Mange hadi auwe watu na blood pressure 🤔🩸 💔

    • @user-qs7lj7kj1k
      @user-qs7lj7kj1k ปีที่แล้ว

      Kama na muona mange kimambi anakuja tz 😂😂

  • @damiodamio4332
    @damiodamio4332 ปีที่แล้ว

    Next mlete salama na Joseph kusaga @salama

  • @luciamsani
    @luciamsani ปีที่แล้ว +1

    sauti na matamshi ya mdomoni hayaendi pamoja watu wa sound warekebishe hapo

    • @viceboy7368
      @viceboy7368 ปีที่แล้ว

      Labda simu yako mkweche

    • @viceboy7368
      @viceboy7368 ปีที่แล้ว

      Sorry nilkuwa xjaichek

    • @luciamsani
      @luciamsani ปีที่แล้ว +1

      @@viceboy7368 basi usiwe mwepesi wa kujibu kabla ya kuhakiki kisemwacho nia yangu ni njema tu si kuharibu coz personally kuna vitu najifunza kupitia some of interviews ila quality pia ni muhimu hata kama nahitaji kusikia tu bila kuangalia mdomo wa mtu

    • @viceboy7368
      @viceboy7368 ปีที่แล้ว

      Kwel dada

  • @christinenyamu1645
    @christinenyamu1645 ปีที่แล้ว

    Jamaa wa editing kuna mahali sauti na picha haziendani

  • @aloyceshaban1348
    @aloyceshaban1348 ปีที่แล้ว

    Dah

  • @patriciacarlo7236
    @patriciacarlo7236 ปีที่แล้ว

    ♥️♥️♥️

  • @aloyceshaban1348
    @aloyceshaban1348 ปีที่แล้ว

    Dah

  • @aloyceshaban1348
    @aloyceshaban1348 ปีที่แล้ว

    Dah