Salama Na GARA B SE6 EP63 | BABA SHUGHULI PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 3 ต.ค. 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Jina MC Gara B ni miungoni mwa majina makubwa sana kwenye ulimwengu wa kazi ambayo mwenzetu huyu amechagua kuifanya. Familia yake, mke na watoto, wazazi wake na wa mkewe pengine, Ndugu jamaa na marafiki na waajiriwa wake wanakula vizuri kwasababu ya kipaji chake Ndugu yetu huyu. Ni mwanaume ambaye akiwa kazini kwake furaha na burudani ambayo huwapa wateja wake ndo inayomfanya azidi kuenda mbali kwenye tasnia hiyo ya ushereheshaji. Again, yeye ni mmoja ya BORA kadhaa ambao wanafanya kazi kama yake.
    Mtandao wa kijamii ni kitu kimoja chenye nguvu sana kwenye miaka ya hivi karibuni, kwa ushahidi tulonao tushawaona wengi ‘wakitoboa’ kwasababu ya Instagram au sehemu nyengine. Mitandao iko mingi na kila mmoja na tobo lake la kufikia mjini. Kazi ambayo MC huyu huifanya yeye huenda na team yake kuiweka vizuri kisha ana post kwenye page yake yenye watu karibia MILIONI MOJA NA NUSU. Akizifikisha mjini kazi hizo wengi huvutiwa nazo na ambao wanakua wana shughuli nao bila ya shaka watamtafuta na kutaka kufanya nae kazi. Ubunifu wake ni wa kipekee kutokana na vingi na wengi ambao tumekua tukiwaona kwa miaka mingi sasa. Mtandao wa kijamii umemsaidia na unaendelea kumfanya awe bora zaidi ya jana.
    Sasa, shughuli hii anayo ifanya ndo ambayo ilikua ndoto zake? Pengine alikua huku anamuona mtu fulani akiwa anaifanya hii kazi kwa ufanisi na ikamvutia? Ilikuaje mpaka akaingia huko? Kwa kumtizama haraka haraka tu utagundua Ndugu yetu ni MCHESHI, yeye anapenda kucheka na kuongea, ingawa hapo kwenye kuongea nako sio kiviiiile ila ni mtafutaji ambaye AMETIMIA. Story yake alotupa kwenye episode hii inajumuisha yeye kufanya kazi zaidi ya mbili kwenye kipindi flani hivi cha maisha yake ili aweze kuishi vizuri. Ki professional mwenzetu ni MWALIMU, ambaye hiyo kazi aliifanya hasa, na akaijumlisha na kazi ya huduma kwa wateja pale Tigo na wakati huo huo akawa anafanya kazi kwenye kiwanda kimoja hivi huko Pugu Road, hakua na wa kumdekea wala kumsubiria na hustle yake hiyo ndo ambayo anaenda nayo mpaka leo kwenye maisha yake.
    Sasa kama Baba na mume kwa mkewe kipenzi ambaye naye alikutana nae sehemu ya kazi yake, Gara B ananijibu kuhusu uaminifu ambao anao kwa mkewe ambaye kwa mujibu wangu kama amekutana nae kwenye mazingira hayo, vipi hujiskia kila mara anapokua kazini mumewe ukichukulia huko ndipo walipo kutana na ndo ambapo wanawake wengi wazuri huwepo? Jibu lake lilikua na kuukonga moyo.
    Alituhadhia pia kuhusu wazazi wake na jinsi ambayo ameweza kujitengenezea jina, siku ya kwanza alipopata kimeo cha ku host harusi ya watu ambayo kwa mujibu wake aliibembeleza sana na hakua amepewa nafasi, ila nafasi ilipojileta akanyoosha kwa umbali mrefu mpaka mengine yamebaki story tu. Na hii ndo ilikua simulizi yangu bora kabisa kuhusu kupata nafasi na kuzitumia vyema.
    Yangu matumaini utaskiliza na kuangalia kwa makini maana humu anatupa simulizi zote za kutokata tamaa na jinsi ya kuchukua nafasi, ila pia anatuhadithia baadhi ya mitihani ambayo huja na umaarufu pia na jinsi ya kupambana nayo. Mimi nili enjoy na natumai itakua hivyo kwako pia.
    Happy Holidays.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

ความคิดเห็น • 46

  • @happynessdavid7921
    @happynessdavid7921 ปีที่แล้ว +3

    Wow naomba nilichojifunza hapa MUNGU kisitoke ktk jina la YESU

  • @Tyrant141
    @Tyrant141 ปีที่แล้ว +4

    Wow such an inspirational interview! Big up salama na Gara B

  • @samsonsimon2610
    @samsonsimon2610 ปีที่แล้ว +1

    Namkubali sana GARA B nimejifunza kupambania kile ninachokiamini

  • @amanmasalu7349
    @amanmasalu7349 ปีที่แล้ว +4

    Salama nakukubali mno very creative sista naomba utuletee mwanamama Jonisia Jacksoni Rukya mwamzi michezo wakike maridadi Tanzania hope tutajifunza kitu mwamba🎉

    • @evancenicholaus7739
      @evancenicholaus7739 ปีที่แล้ว

      Maadili ya kazi yake hatamruhusu kufanya mahojiano na media, mpaka astaafu

  • @egbartrwegasira1250
    @egbartrwegasira1250 ปีที่แล้ว +3

    Kutoka Rio de Janeiro ya bongo... Kule kuna vipaji vingi sana..

  • @mashopluck
    @mashopluck ปีที่แล้ว +1

    Most Blessed Gara B

  • @EmanuelisMichael-kw9nf
    @EmanuelisMichael-kw9nf ปีที่แล้ว

    Big Brother Gara B. Kubali sana
    Natamani Kufanya Kazi yako #Una Busara sana

  • @salomewandya7257
    @salomewandya7257 ปีที่แล้ว +1

    Kweli maisha ni kupambana 👏👏🙏🙏

  • @NuhuMiraji
    @NuhuMiraji ปีที่แล้ว +7

    Salamaaaa real love u but tulete mondi❤

  • @marianajohn5415
    @marianajohn5415 ปีที่แล้ว +3

    What a lovely interview nimependa alivyooneshwa mke wake ❤😂

  • @marianajohn5415
    @marianajohn5415 ปีที่แล้ว +1

    Ndio maana anaufanya vizuri sana uMC! Kumbe ameshakuwa mwwlimu! Big up sana Gara B

  • @aasantemungusays
    @aasantemungusays ปีที่แล้ว +3

    Wa kwanza kuview, whatsup watu wa Tz✌🏾

  • @benjaminsaimon200
    @benjaminsaimon200 ปีที่แล้ว +7

    Sister salama #Millard ayo plz#

  • @johnyoram7876
    @johnyoram7876 ปีที่แล้ว +2

    We need Prof Kabudi pls

  • @godfreymiho4927
    @godfreymiho4927 ปีที่แล้ว +2

    🤗 respect sana salama

  • @alinebakome
    @alinebakome ปีที่แล้ว +1

    Nawapnda sanaaa nyinyiiii wawiliii

  • @souksoukeventsandmarketing653
    @souksoukeventsandmarketing653 ปีที่แล้ว +1

    Robert was my wedding photographer 2010

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    Baba boy 👌🏽tume subiri sana 🤦🏿‍♀️🙌🏿

  • @lizahadongo1801
    @lizahadongo1801 ปีที่แล้ว +2

    Best mc in Tanzania 🇰🇪

  • @marianajohn5415
    @marianajohn5415 ปีที่แล้ว +3

    Tuletee lulu salama

  • @peterkimati7003
    @peterkimati7003 ปีที่แล้ว +3

    Tuletee frida amani

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    Uwiiii nime jifunza mimi kufanya kazi nyingi 🙌🏿🙌🏿🙌🏿📝📝

  • @niriacatering172
    @niriacatering172 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana Asante

  • @FrankAbelly
    @FrankAbelly ปีที่แล้ว

    🎉🎉

  • @juliuskuluo8876
    @juliuskuluo8876 ปีที่แล้ว +1

    Naomba utuletee joti au masanja

  • @Yusufu940
    @Yusufu940 ปีที่แล้ว +1

    Salma ndefu kwa wanaune Ni ushujaa na ukuwaji

  • @dostovan5142
    @dostovan5142 ปีที่แล้ว +3

    Mlete mc eliud

  • @mariamusaulo4429
    @mariamusaulo4429 ปีที่แล้ว +2

    Tuleteee Juma Lokole Salama

  • @ramashemngindo5719
    @ramashemngindo5719 ปีที่แล้ว +1

    Namkubar sana huyu jamaa

  • @goodlucktemu3149
    @goodlucktemu3149 ปีที่แล้ว

    Mafanikio ni safari ndefu.

  • @liannsambu7264
    @liannsambu7264 9 หลายเดือนก่อน

    Sasa autoe mustach mara ya pili unakuwa umejaa mara nyingi nywele ukikata YANAJAA ZAIDI

  • @TreciousMahende
    @TreciousMahende ปีที่แล้ว

    Chris mziwanda aje salama

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    Tuna omba juma lokole please

  • @esterdoriye8377
    @esterdoriye8377 ปีที่แล้ว +2

    Nina extra duty yangu nje na ualimu naenda kusimamia kikamilifu kuptia GARA B

  • @azizamohd4203
    @azizamohd4203 ปีที่แล้ว

    Salama unamtaka nn mbona unacheka sauti iyo ww

  • @EmanuelisMichael-kw9nf
    @EmanuelisMichael-kw9nf ปีที่แล้ว

    Sorry Ni Mwalimu wa Masomo gani.

  • @aishaomarry6996
    @aishaomarry6996 ปีที่แล้ว +1

    Mi mwenyewe mwanamme asie na ndevu simpendi

  • @West-side-lt9nb
    @West-side-lt9nb ปีที่แล้ว

    Rest in peace Gara B