Muuguzi aliyetoweka KCMC alikuwa atoe mahari mwezi huu

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.ค. 2024
  • Wakati uchunguzi wa tukio la kutoweka kwa Muuguzi wa Hospitali ya KCMC, Lenga Masunga (38) ukiendelea, familia yake imesema ndugu yao alikuwa katika harakati za kufunga ndoa na mwezi huu wa saba alikuwa atoe mahari.
    Muuguzi huyo wa Idara ya Masikio, Pua na Koo (ENT) anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Julai 2, mwaka huu nyumbani kwake katika Mtaa wa Rau Pangaleni, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokuwa akiishi.
    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya KCMC, Masunga alikuwa mapumziko ya siku mbili tangu Julai 2 na Julai 3 na kwamba alitakiwa kuwepo siku iliyofuata. Hata hivyo hakuonekana, hali ambayo iliyoibua mashaka na kusababisha uongozi wa hospitali hiyo kumtafuta kupitia simu zake za mkononi ambazo hazikupatikana.
    Jana, mwenye nyumba alikokuwa akiishi muuguzi huyo, Robert Mwakalinga alidai kuwa muuguzi huyo aliondoka usiku wa Julai 2, na kuacha mlango wa chumba chake ukiwa wazi mpaka kulipokucha asubuhi Julai 3, mwaka huu.
    Akizungumza na Mwananchi Digital, kaka wa muuguzi huyo, Paschal Jeremiah, amesema ndugu yake alikuwa akitegemewa na familia yake na mwezi huu wa saba alikuwa na mpango wa kutoa mahari na watangaze siku ya ndoa yao.
    Soma kwa undani kupitia www.meananchi.co.tz

ความคิดเห็น • 3

  • @AtuganileAsubisye
    @AtuganileAsubisye 20 วันที่ผ่านมา +1

    Inauma sana jamanii mahusiano msote mambo yake sawa shetanii aingilie katii eee Mungu fanya njia aonekane wewe pekee wajua alipoo

  • @user-xk7vy4gb6g
    @user-xk7vy4gb6g 20 วันที่ผ่านมา

    Hili swala la kupotea watu nimerudi tena jamani

  • @evamlay8997
    @evamlay8997 19 วันที่ผ่านมา

    mchumba achunguzwe haraka