REV.DR. ELIONA KIMARO: BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI/ SEXUAL TRANSMISSION CURSE

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 ก.พ. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
    IBADA YA MORNING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING
    'HII NI KWARESMA:SIKU YA 8
    22/ 02/ 2024
    MADA:
    NIDHAMU NI HATIMA
    DISCIPLINE IS DESTINY
    SOMO LA LEO: BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI
    SEXUAL TRANSMISSION CURSE - STC
    Ufunuo 17 : 1 - 7
    Ufunuo 18 : 1- 3
    NENO KUU:
    "Zitafakarini njia zenu"
    (Consider your ways)
    Hagai 1:7
    Ufunuo 17 : 1 - 7
    1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
    2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
    3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
    4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
    5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
    6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
    7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
    Ufunuo 18 : 1- 3
    1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
    2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
    3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

ความคิดเห็น • 36

  • @merikebukasayo3714
    @merikebukasayo3714 5 หลายเดือนก่อน +1

    Hapo mchungaji pole Hilo fungu umetafisili uongo na unapotosha watu wa mungu.hayo maandiko yanazungumzia mfumo wa kishetani ambayo unasimamiwa na mamlaka za serikali pamoja dini usidanganye watu wa mungu.kumbuka Neno limesema Babeli mkuu.babeli ni mfumo wa kinyama na ukandamizaji dhidi watu wa mungu

  • @tumainijoshua5090
    @tumainijoshua5090 5 หลายเดือนก่อน +3

    Kadri Watumishi wa Mungu wengine wanavyozidi kuona ni aibu kuyanena haya na si mambo ya msingi kuhubiri,ndivyo wanavyowaangamiza wengi bila kujua,because My People Perish due lack of knowledge, na Hekima ya wasomi inasema pia INFORMATION IS POWER

  • @jacobfaustine7866
    @jacobfaustine7866 5 หลายเดือนก่อน +1

    Mch wangu, hakika wewe ni mwl wa neno la Mungu. Barikiwa sana.

  • @tumainijoshua5090
    @tumainijoshua5090 5 หลายเดือนก่อน +1

    Ubarikiwe Pastor kwa Kutufungua macho,hii Lecture naomba ifike kwa Mamilion na wasikie wakombolewe especially Vijana

  • @terevaelikaaya8199
    @terevaelikaaya8199 5 หลายเดือนก่อน

    Barikiwa sana mchungaji tunafunguliwa sana,je kijana aliyefanya mapenzi katika Hali hiyo hatatokaje kutumika na uchumi wake ukasimame tusaidie njia ya kutoka

  • @user-hs5qm8yx4r
    @user-hs5qm8yx4r 5 หลายเดือนก่อน

    mtumishi wa MUNGU,,,,,,,, BWANA YESU ASIFIWE,,,,,barikiwa sana mchungaji,,,, MUNGU wa mbingu na nchi akubalike sana maana uzinzi ulinisumbua sana,,, sasa nimepona kwa Jina la BWANA YESU

  • @rehemasuleman6720
    @rehemasuleman6720 5 หลายเดือนก่อน

    Aiseeee this is huge. Ubarikiwe sana Mchungaji hii ni kweli kabisa

  • @user-dz3rl1ki6u
    @user-dz3rl1ki6u 5 หลายเดือนก่อน

    Mchungaji kwa mafundisho haya hakika Kuna kusudi kubwa la Mungu umelibeba na lazima Vita kukuelekea iwe kubwa maombi yangu kwa Mungu wetu aliye juu akufunike kwa Damu tukufu ya Yesu Kristo ulindwe kila kuitwapo leo daaah!! Kwakweli unafundisha vitu very clinical ubarikiwe Sana mtumishi

  • @user-yu7bn9wo7v
    @user-yu7bn9wo7v 5 หลายเดือนก่อน +2

    Hii ni kweli kabisa, nilienda kwenye utafutaji na 3m nkampata mdada mzuri sana nilipofanya naye zinaa tu.... Nilipata hasara pesa yote iliisha nakurudi na nauli tu.

  • @dapinitiative2451
    @dapinitiative2451 4 หลายเดือนก่อน

    Mwenyezi Mungu akubariki sana

  • @amosziro7054
    @amosziro7054 5 หลายเดือนก่อน

    Asante pastor..Mungu tusaidie

  • @rahabnkya8276
    @rahabnkya8276 5 หลายเดือนก่อน

    Baba Eliona Kimaro unayofundisha leo nimeguswa nayo mimi kama mimi, nami naomba Mungu anirehemu kwa somo hili dhahiri, nawe Baba, Mungu asikuache, wewe, watoto wa UZAO wako , nao pia wakue na KUACHA kabisa Zinaa hii unayofundisha , STC, MBAYAA.

  • @clementgaspersoka4139
    @clementgaspersoka4139 5 หลายเดือนก่อน

    Leo nimekuelewa sana Mtumishi wa Mungu

  • @adenhyera4820
    @adenhyera4820 5 หลายเดือนก่อน

    Mtumishi ubarikiwe zaidi endeleaaaa hivyo hivyo kufundisha kweli

  • @user-wg2oi3kp1k
    @user-wg2oi3kp1k 4 หลายเดือนก่อน

    😭😭😭😭 ooh My God stay with me

  • @user-zq6xk8ou9w
    @user-zq6xk8ou9w 5 หลายเดือนก่อน

    Mafundisho manzuri kweli Mungu akuweke

  • @marysdiosa8764
    @marysdiosa8764 5 หลายเดือนก่อน +1

    Kama mim nikifanya mapenzi na baba mtoto wangu, lazima nigombane na mtu ,sana sana wapangaji wenzangu , mara tatu sasa

  • @teddysisty320
    @teddysisty320 4 หลายเดือนก่อน

    Mungu nisaidie 😢😢

  • @ceciliavintany2113
    @ceciliavintany2113 5 หลายเดือนก่อน +1

    Leo mm nimeelewa vyema Asante Sana mtumishi

  • @bhokeshinta5140
    @bhokeshinta5140 5 หลายเดือนก่อน +1

    Leo umenipata mtumishi wa mungu😭😭

  • @cmsa1r
    @cmsa1r 5 หลายเดือนก่อน

    Bwana Yesu. Tusamehe!!!!

  • @peterkashamba
    @peterkashamba 5 หลายเดือนก่อน

    Be blessed pastor 🙏🏿🙏🙏🏿

  • @user-wl9ry9tk7p
    @user-wl9ry9tk7p 5 หลายเดือนก่อน

    Nakuelewa Mchungaji niko Misungwi Mwanza.

  • @user-us8xw9cg4o
    @user-us8xw9cg4o 5 หลายเดือนก่อน

    Mchungaji zidi kubarikiwa

  • @oscarngowi4750
    @oscarngowi4750 2 หลายเดือนก่อน

    Kimaro nenda kajifuze unabii wa Danieli na ufunuo kwaza acha kudanganya watu wa Mungu . Mwanamke ni kanisa mnyama ni utawala(serikali) maji au mchanga wa bahari ni watu wengi dunia nzima BABELI ni mamlaka ya UPAPA

  • @user-mn2wt9fu6v
    @user-mn2wt9fu6v 5 หลายเดือนก่อน

    God be with you uzidi kutufungua

  • @terevaelikaaya8199
    @terevaelikaaya8199 5 หลายเดือนก่อน

    Mchungaji nitapataje naomba zako

  • @williamjumbe1988
    @williamjumbe1988 5 หลายเดือนก่อน +1

    Pastor naweza kupata namba zako mchungaji,

    • @GAUDENSIAKIMARIO
      @GAUDENSIAKIMARIO 5 หลายเดือนก่อน

      Ingia u tube kwenye masomo ya Eliona kimaro kijitonyama utapata namba hapo

  • @marysdiosa8764
    @marysdiosa8764 5 หลายเดือนก่อน

    Hivi Huwa wanarudishaje nyota jaman 😮

  • @simonjackson4722
    @simonjackson4722 5 หลายเดือนก่อน +1

    Leo umenipata pia mtumishi

  • @belfastmoshi9005
    @belfastmoshi9005 5 หลายเดือนก่อน

    Babeli mkuu ninani ?

  • @tobesimatiku1987
    @tobesimatiku1987 5 หลายเดือนก่อน +2

    Rafiki yangu kimaro fundisha mambo yote lkn siyo hayo mafungu hapa unadanganya Dunia yote nenda kajifunze zaidi upate kuelewa......kwanza lazima uelewe mwanamke ni Nini? Mnyama ni Nini? ..maji ni Nini? ..naona unaongea usaniii mtupu aiseee.........Daniel 7:1-25 kasome yote ufunuo 17:15 Iko wazi .....