RAIS MWINYI: HAIWEZEKANI HATA SIKU MOJA | SERIKALI INAWEKA DHAMANA ITALIPA.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 20 ธ.ค. 2023
  • SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imewatoa hofu Mfuko wa Hifadhi ya Huduma za Jamii Zanzibar, (ZSSF) na kuwataka kuwekeza fedha zao kwenye miradi mikubwa ya Serikali ya kimakakati.
    Pia, Serikali imejizatiti kuweka dhamana ya miradi mikubwa ya maendeleo itakayotekelezwa na Mfuko huo pamoja na kuwahakikishia usalama wa fedha zao endapo zitaathiriwa kwa namna yoyote na ujenzi wa miradi hiyo.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa maegesho ya magari, Malindi Wilaya ya mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
    Alisema, lengo la Serikali kuweka ujenzi wa maegesho hayo ni kupunguza msongamano wa magari mjini pamoja na kuweka usafiri wa umma wa aina moja na wa kisasa ili kwenda sambamba na mahitaji ya mji kwa wakati uliopo.
    .................................................................................................
    Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote.
    Follow Ktv Tz Online
    Facebook | KTV TZ ONLINE
    INSTAGRAM |@ktv_tz_online
    Wasiliana nasi kupitia number
    +255 717 619 834
    Ktv Tz Online Journalists
    cc: Sadia Rashid
    cc: Sauti Byego
    Camera Department"
    Dadi Ali
    Omar (OJ)
    Nassor Shaibu
    Abdallah Juma
    Editors:
    Juma Maulid
    Dadi Ali
    Video Zingine:
    Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima
    - Ali Kiba akiwa Oman
    • ALICHOKIFANYA DIAMOND ...
    • NI KWELI ALI KIBA AMNU...

ความคิดเห็น • 16

  • @AhmedAli-gh1lm
    @AhmedAli-gh1lm 7 หลายเดือนก่อน +5

    Mheshimiwa tunashukuru sana kwa kazi unazofanya, na tumeona ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wako kumeanza kutokea mabadiliko makubwa hapa nchini khasa katika upanade wa miundo mbinu. Unastahiki pongezi nyingi kwa hilo, na tunataka uendelee kuibadilsha Zanzibar nayo iingie katika Karen ya 21. Ila Mh. usisahau kuufanyia kazi upande wa maisha ya watu huku mitaani, jambo kubwa linalotuumiza ni NJAA, bei za vyakula ziko juu ya uwezo wetu tulio wengi. Kama ungeweza kutafua njia za kupunguza ukali wa maisha kwa sisi watu wa kawaida ungetusaidia sana.

  • @zainamasoud-vz8nw
    @zainamasoud-vz8nw 7 หลายเดือนก่อน +2

    Muheshimiwa hongera sana Allah akupe umri mrefu wenye baraka Tele mwenye macho haambiwi tazama

  • @afropanorama4730
    @afropanorama4730 7 หลายเดือนก่อน +1

    kwenye la public transport apo sawa kama kweli muko serious,mana kisiwa kishazidiwa na magari na mengi mabovu kuliko mazima

  • @mohddelo
    @mohddelo 7 หลายเดือนก่อน

    Safi

  • @awatifalghanim1106
    @awatifalghanim1106 7 หลายเดือนก่อน

    Rais Mungu akuweke..wewe umeona mambo mengi ya kisasa manake umesafiri sana na umeona maendeleo ya Nchi za watu . Usafi ni kitu muhimu kwenye Nchi kabla ya hayo Maendeleo ya kujenga majumba. Wananchi wachukuwe juhudi kubwa ya wasafisha Nchi yao kwanza wasisubiri kuja Wageni ndio waanze kusafisa mji.

  • @pavillioncry5241
    @pavillioncry5241 7 หลายเดือนก่อน +2

    Achana na act hawana sera

    • @nassorseif7907
      @nassorseif7907 7 หลายเดือนก่อน

      Walokua hawana sera na ccm mwaka wa 60 huu hawana moja walolifanya

    • @hamadabdullahkhamis977
      @hamadabdullahkhamis977 7 หลายเดือนก่อน

      CCM juu zaidi...

  • @mullestv2680
    @mullestv2680 7 หลายเดือนก่อน +1

    Mh kwanza hongera nchi unajenga but si wananchi hatuli masako barabara Wal zahanati kuimarisha miundo mbinu huenda sambamba na uimarishaji wa matumbo. Wachache nd wataelewa

  • @khatibal-zinjibari6956
    @khatibal-zinjibari6956 7 หลายเดือนก่อน

    Majengo kwa Kampeni za 2025.

  • @husnamohamed9245
    @husnamohamed9245 7 หลายเดือนก่อน +1

    Sawasawa mheshimiwa tunataka na viwanda wananchi pia wanataka kula wananchi wanataka kazi funguwa viwanda pia watu wasilale na njaa. Vijana hawana kazi viwanda muhishimiwa

  • @user-dw6hj8wu8x
    @user-dw6hj8wu8x 7 หลายเดือนก่อน

    Sisi tunafaidika naa nini naomba majibu

    • @mohdmohd8428
      @mohdmohd8428 7 หลายเดือนก่อน

      Mwendo kasi ni mradi kodi yake ni faida kwa serikali, na wafanyakazi ni faida ajira, pia utaenda kwa muda ktk kaz zako mjini, pia maendeleo sheikh

    • @user-dw6hj8wu8x
      @user-dw6hj8wu8x 7 หลายเดือนก่อน

      @@mohdmohd8428 hujajuwa Dunia wewe misingi ya wananchi nikujenga taifa lako kuwa na ajira nyingi na unafuu wa vitu na maisha afazali wewe Baki tuu

    • @user-dw6hj8wu8x
      @user-dw6hj8wu8x 7 หลายเดือนก่อน

      Tunataka masilahi ya maisha sio Kila kituu bei juuu na uwezoo wa kuweka maisha kuwa afazali inawezekana