Salama Na DEO GRATIUS SE6 EP64 | PRIVILEGED?! PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 24 เม.ย. 2023
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Deo Gratias, jina tu linatosha kujielezea kama wewe nawe utakua kama mimi wa kutaka kujua maana ya majina ya watu ili uweze kujua tabia zao au ujiulize wazee wake walikua wanafikiria nini wakati wanaamua kumpa jina hilo mtoto wao. Kwa Deo maana imejibeba na imejikamilisha na kwa yeye kuamua kubaki na jina lake hilo hilo mpaka kwenye stage ambako ndo sehemu yake ya kazi inabidi hilo nalo likuambie jambo kuhusu yeye na jinsi ambavyo anajichukulia na kuyachukulia mambo ambayo ameyachagua kuyafanya.
    Shukrani ziende kwa Mungu ndo maana ya jina lake, shukrani ziende kwa Mungu kwa kila alifanyalo leo, shukrani ziende kwa Mungu maana baada ya wazee wake kumsomesha kwenye shule ambayo walikua wameianzisha wao na kuhakikisha kijana wao anapata elimu ambayo anastahili lakini yeye akaamua kuiacha fani ambayo aliisoma na kuamua kuwa mchekeshaji basi nadhani Shukrani ziende kwa Mungu, Shukrani ziende kwa Mungu kwa wazazi wake kuelewa, Shukrani pia ziende kwa Mungu kwasababu mwanga umeanza kuonekana kwenye lile alifanyalo sasa.
    Yeye na rafiki zake ambao ni vijana wenzake wamejikusanya na kuanzisha kundi lao linaloitwa Watu Baki, ila hawakuamka tu wakaanzisha, kuna ka story hapo nyuma yake ambapo ndo panaleta maana kwenye maisha yetu na yao kama watafutaji. Deo anakumbuka audition ya kwanza ya Stand Up Comedy ambayo aliwahi kuifanya na akashinda huko Mbagala, chini ya shindano lililokua likisimamiwa na Evans Bukuku, Deo anakumbuka kushinda MILIONI nadhani kwenye shindano hilo ingawa alipofika home aligundua kuna mwana alichomoka na elfu kumi yake, yaani kuna mwana alimuangalia Deo, kisha akakiangalia kibunda alafu akasema nah, hawezi kumpa yote lol.
    Courage ya kufanya mengine mengi ikiwa na pamoja na ambayo yanaendelea leo ilianzia hapo. Mengine yakabaki story!
    Story ya kujikusanya na wanae enzi za Cheka Tu na baadae kuamua kundoka na kuanzisha WatuBaki ilikua mmoja inabidi awe na uthubutu na uthubutu huo uliwezekana na mpaka leo wamesimama na wana time yao kwenye DSTV ambayo inatoa burudani nzuri tu kwa watu wao na vile vile bado matamasha ya nje wanafanya wao kama wao.
    Kwa wengi ikiwa pamoja na mimi tulipewa story kwamba Deo ni mtoto flani wa kishua alokua kutoka kwenye familia inayokula wali kwa kijiko na ndo maana baadhi ya mambo ilikua rahisi kwake kufanyika kwasababu ana uwezo wa kurudi nyumbani kwa Baba na Mama na akarudi na mzigo wa kutosha ambao unasaidia mambo yaende. Ila kwa mujibu wake, hiyo si habari na wala yeye hajatoka kwenye mazingira hayo ambayo wengi wanadhani ametokea.
    Bado safari ndo kwanza imeanza na kwa wenzake yeye akiwa kama kiongozi anaamini kama wakitulia pamoja na kufuata maono yao basi mengi mazuri tu yatakuja, ila sasa huo uwezo wa kuweza kutulia pamoja na kutengeneza kitu kikubwa na kizuri ndo inawezakana ikawa mtihani. Si wengi wameweza ingawa wapo ambao wameanza pamoja na mpaka leo wanaunguruma pamoja. Inawezekana na yangu matumaini wao pia wataendelea kuwa WatuBaki kwa muda wote ulobaki.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camSalamaNa
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • บันเทิง

ความคิดเห็น • 50

  • @Unique653
    @Unique653 ปีที่แล้ว +2

    I love when he said you have to believe first then you see!
    Nyie huyu ni intellectual sana

  • @salmasaid8964
    @salmasaid8964 ปีที่แล้ว +3

    Uyu ndo alinifanya nianze kufatilia show za cheka 2
    Na walivyoama nkaama nao mazima
    Deo anajua sana
    Vichekesho vyake uksikiliza juu juu unaweza usielewe 😁😁
    Big up Deo unapendwa na Wengi sana mkuu
    #wa2baki

  • @Beingnoela
    @Beingnoela ปีที่แล้ว +4

    I laughed, enjoyed and got educated, this man is talented trust me guys 🙌🏾💯.
    Keep shining Deo Gratius 🤎

  • @Unique653
    @Unique653 ปีที่แล้ว +2

    THIS GUY IS SO UNIQUE. I RELATE DEEPLY TO HIS STORY ❤️🥰

  • @RedmarLeeuwendal
    @RedmarLeeuwendal ปีที่แล้ว +6

    Learning Kiswahili in university right now. this really helps!

  • @matronashirima1489
    @matronashirima1489 ปีที่แล้ว +6

    #Pay attention and speak magical words# Nimeidaka hii

  • @christk24
    @christk24 ปีที่แล้ว +4

    Very nice interview hongera Deo and big up to the team na Salama

  • @ishakafaki3501
    @ishakafaki3501 ปีที่แล้ว +2

    Daahh jama anaongea kama anapiga story but anaongea pwent mingi aisee 💯🙌 SALAMA SHKRN SANA KWAKO NA STON KWA UJUMLA

  • @vannapple1
    @vannapple1 ปีที่แล้ว +10

    This guy hata olevel alikuwa ivo ivo,Anaongea vitu vya kufikirika,Ukimsikiriza kwa juu juu unaeza ona anazingua tuu

    • @kaizilejackson862
      @kaizilejackson862 ปีที่แล้ว

      Kabsaaaa... Unajua bado napata shida kumuelewa hii hip hop ya fid Q mmmh!!!

    • @daphresmfugale9435
      @daphresmfugale9435 ปีที่แล้ว

      Yah sure, kuongea kitu ni mpaka atoe mfano at least 😅😅

  • @mtafutajiog1939
    @mtafutajiog1939 ปีที่แล้ว +3

    Da ongera sana sister ujawahi kukosea kwenye kuandaa program so tuletee kitale mkude simba

  • @henrykabupa2816
    @henrykabupa2816 ปีที่แล้ว +1

    The guy is smart n genius 🖐🖐👐

  • @mariawandiba6736
    @mariawandiba6736 ปีที่แล้ว +2

    Deo, you are unique and genius big up

  • @felisterherman2568
    @felisterherman2568 ปีที่แล้ว +1

    The boy is genius had bac ❤

  • @rhodajackson2213
    @rhodajackson2213 ปีที่แล้ว

    Hongera Salama kazi yako njema sana

  • @bahatijonas2183
    @bahatijonas2183 ปีที่แล้ว +1

    Salama Tunaomba Tuletee WACHAMBUZI WA MCHONGO 😢😢😢 Ganslay and Headmaster These Guys Are Viral Now everywhere Tunataka Tuwajue zaidi

  • @doreenkifaluka4568
    @doreenkifaluka4568 ปีที่แล้ว +1

    This Guy So Genius Tunaomba Wachambuzi Wa Mchongo pia

  • @danforddavid6023
    @danforddavid6023 ปีที่แล้ว

    very smart explanation

  • @thebrand9350
    @thebrand9350 ปีที่แล้ว +2

    You know why they are so smart?..... Because they think a lot and also they see what is coming before you do. so mostly they don`t feel happy about it but they stay fun to comfort themselves, na maranyingi ni watu wanaokuwa lonely sometimes kwasabuba wanakuwa pekeao maranyingi. huwa hawamechi na groups nyingi kwenye jamii inayowazunguka.
    I know the feeling simply because naiishi hali hiyo.😀😀😀😀

    • @Unique653
      @Unique653 ปีที่แล้ว +1

      I feel you. I'm exactly like that.

  • @derickdepota101
    @derickdepota101 ปีที่แล้ว

    Smart and Talented🙌🏿

  • @Bob-kz2ql
    @Bob-kz2ql ปีที่แล้ว +3

    Salama bado mkojani bin darwesh

  • @mercyjsaid1628
    @mercyjsaid1628 ปีที่แล้ว +1

    I'm enjoying the way he speak na salama anavyouliza

  • @rehemarwanda6039
    @rehemarwanda6039 ปีที่แล้ว

    Deo ur so intelligent

  • @shosetz7200
    @shosetz7200 ปีที่แล้ว +4

    He's very smart🙌

  • @ingabireritha3740
    @ingabireritha3740 ปีที่แล้ว

    Very nice

  • @brianlynch485
    @brianlynch485 ปีที่แล้ว

    Really smart guy

  • @SamuelSingogo-tf6tv
    @SamuelSingogo-tf6tv ปีที่แล้ว +1

    Nasubiri salama na young killer msodoki

  • @dianerditto
    @dianerditto ปีที่แล้ว

    Leo mapeema kabisa

  • @moekan_3612
    @moekan_3612 ปีที่แล้ว

    Salama na Wema sepetu

  • @goodlucktemu3149
    @goodlucktemu3149 ปีที่แล้ว

    Mwamba ni mtu mno anajua kujieleza sana

  • @uwerapraxeda7240
    @uwerapraxeda7240 ปีที่แล้ว +1

    Tuletee Eliud wa cheka tuu

  • @nasrikileo7291
    @nasrikileo7291 ปีที่แล้ว

    Salama, siku moja tuletee nikki mbishi

  • @itsbazil5787
    @itsbazil5787 ปีที่แล้ว

    Mdogo mdogo mpk tutafika

  • @giftwieland6322
    @giftwieland6322 ปีที่แล้ว

    Tunaomba evans bukuku📌

    • @shizaarfred4059
      @shizaarfred4059 ปีที่แล้ว

      Kasha pita fuatilia za nyuma utamuona huko we kaangalie amevaa kapelo nyeusi 😀😀

  • @laurentrevoh3216
    @laurentrevoh3216 ปีที่แล้ว +1

    Next stop Wachambuzi Wa Mchongo please 🙏

  • @fauziasultanikilewa7602
    @fauziasultanikilewa7602 ปีที่แล้ว +1

    Jaji mwenye roho mbayaa😂😂

  • @abdulhakimmwango9370
    @abdulhakimmwango9370 ปีที่แล้ว +3

    He's speak in joke but realistically 🎉

    • @albertlokoya7937
      @albertlokoya7937 ปีที่แล้ว

      I also noticed, also school plays a a part in his speaking ideology

  • @Yusufu940
    @Yusufu940 ปีที่แล้ว

    Salma tena pumbavu imetoka wapi ihi?

  • @zawadilutufyo8771
    @zawadilutufyo8771 ปีที่แล้ว

    He is genius

  • @camillah1097
    @camillah1097 ปีที่แล้ว

    Maswal ya uigizaji sijasikia

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +1

    🤣😂🔨

  • @giftwieland6322
    @giftwieland6322 ปีที่แล้ว

    Tuletee evans bukuku

  • @charlesmakuke3809
    @charlesmakuke3809 ปีที่แล้ว

    WANGAPI WANASUBIRI KUONA SALAMA NA WACHAMBUZI WA MCHONGO Ganslay na Headmaster?!!!!!!! 🏃🏃🏃🏃🏃

    • @haniphadaud667
      @haniphadaud667 ปีที่แล้ว

      Wakwanza hapa😅😅😅 nawasaubiria sana