SABABU zatajwa Kinachosababisha SANAMU la Mwalimu NYERERE kukosewa

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ก.ย. 2024
  • Wataalamu wa uchongaji na uchoraji wametaja sababu zinazoweza kufanya sanamu kushindwa kubeba mfanano wa mtu husika ikiwemo kukosekana kwa uwiano halisi na vipimo.
    Mbali na kutoa sababu hizo, pia wameshangaa kuendelea kuwapo kwa sanamu ambazo hazina uhalisia, huku wakieleza kuwa hivi sasa teknolojia imerahisisha kila kitu ikiwemo utengenezaji sanamu.
    Wametoa kauli hizo ikiwa ni siku moja baada ya kuzinduliwa kwa sanamu la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere nchini Ethiopia, huku likiacha gumzo mitandaoni na watu wengi kudai kuwa sanamu hilo halifanani na hayati Nyerere.
    Sanamu hilo lililozinduliwa makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Adis Ababa, Ethiopia limewekwa mbele ya jengo la siasa, amani na usalama la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika na kuhimiza umoja na Amani.
    Hatahivyo, Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa Nyerere alipohojiwa alisema akiwa miongoni mwa wanakamati kwa ajili ya kusimamia mchakato wa utengenezaji wa sanamu hiyo, waliipitisha kwa zaidi ya asilimia 90.
    Akizungumzia changamoto katika uchongaji na ufinyanzi, Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam idara ya Sanaa, Digna Enock ansema makosa yanayofanyika ni wasanii kushindwa kufuata kanuni za uchongaji na ufinyangaji.

ความคิดเห็น • 19

  • @user-qm2vf2qz3l
    @user-qm2vf2qz3l 6 หลายเดือนก่อน +1

    Huyoo alikuwa sio msanii ila alikuwa mpigajii me kama mtanzania nasemaa hiyoo sanam ibadilishwe

  • @denisipaulo7785
    @denisipaulo7785 6 หลายเดือนก่อน

    Tumepigwaaaaaaaaaaa

  • @KhaleedHamad-vl7lz
    @KhaleedHamad-vl7lz 6 หลายเดือนก่อน

    Umeonekano haupo kbs musijikanyage

  • @mabondolawrence1812
    @mabondolawrence1812 3 หลายเดือนก่อน

    Kwani bado linachongwa! Hivi kwanini misanamu!

  • @rkcomercialenterprises3209
    @rkcomercialenterprises3209 6 หลายเดือนก่อน

    Hii sanamu siyo mmmmhhh

  • @kiatu
    @kiatu 6 หลายเดือนก่อน

    Huyu mama technology imekwacha nyuma 😅

  • @elbaricktv1632
    @elbaricktv1632 6 หลายเดือนก่อน

    Live vip mzeee technology imebadilika saiv kwan wakimtazama kwenye video hawawez ona sura halisi?

  • @calvinshirima2654
    @calvinshirima2654 6 หลายเดือนก่อน

    Huku ni kumkejeli
    Mwal.Nyerere 😢

  • @JustineKashililika-tc8sx
    @JustineKashililika-tc8sx 6 หลายเดือนก่อน

    Wazungu ndio maana wanatuita weusi manyani kweli wewe umekubaliana na Nyerere wa Ethiopia

  • @smarty1064
    @smarty1064 6 หลายเดือนก่อน

    Huo ni UONGOOO bana

  • @user-zc1qh6ti2p
    @user-zc1qh6ti2p 6 หลายเดือนก่อน

    We mama wee acha kutetea waharifu. Kukosea kupo ila ndo wamuweke komwe

  • @dicksonjailos670
    @dicksonjailos670 6 หลายเดือนก่อน

    Tatizo sisi wasanii wa Tanzania wakufinyanga mnatuzarau ndiomana mmetuletea sanamu isiyo sahihi? Mlishindwa nini kutupeleka tukalihakiki hukohuko hata kama hatujasoma make tuna tarent

  • @smarty1064
    @smarty1064 6 หลายเดือนก่อน

    Propotion si ni vitu wanajifunza kwenye madarasa ya sanaa ya uchongaji, nayo inabidi wamuone live? uongo uongo tu mwingi kubeba watu wasio na viwango kwenye profession zao

  • @faustinluambano2958
    @faustinluambano2958 6 หลายเดือนก่อน

    Eangeliwapa WAZUNGU hii aibu wasongeliipata

  • @alexmalyango1405
    @alexmalyango1405 6 หลายเดือนก่อน

    Sasa akikosea kwanini mpitishe wakati tumewatumeni ninyi?

  • @Msemakweli2024
    @Msemakweli2024 6 หลายเดือนก่อน +1

    Mnaopinga tengenezeni za kwenu. Ninyi siku zote mnamuona kwenye picha halafu mnapinga. Hii kwanza ni sanamu sio picha (photo). Kuna vigezo maalum vinafuatwa

    • @adkajisi4536
      @adkajisi4536 6 หลายเดือนก่อน +2

      Ndo uliye tengeneza nini?

  • @chinamilenas3375
    @chinamilenas3375 6 หลายเดือนก่อน

    Videos za mwalimu zipo nyingi tuuu wangeoneshwa...why watumie picha?