Salama Na DORIS MOLLEL SE6 EP68 HALF WOMAN, HALF AMAZING PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 พ.ค. 2023
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Doris Mollel kwa kuanzia tu tuanze na jina lake, ni zuri lenye kukumbukwa ki rahisi, yeye mwenyewe pia ni mrembo na mkarimu, sana. Roho yake ni kama rangi yake, nyeupe na kwa bahati Mimi namfahamu yeye kiasi kwa kupitia rafiki zangu ambao yeye anafanya nao kazi na pia ana mahusiano nao mazuri, sana. Pia namfahamu mume wake ambaye tukianza shindano la kumtafuta nani mkarimu kati yao tunaweza kukamaliza kwa suluhu. Huwa naamini Mwenyezi aliwakutanisha ili kwa pamoja waweze kufanya makubwa kwaajili yao na familia zao na jamii ambayo imewanzunguka ambayo kwa kiasi kikubwa ina uhitaji wa yale ambayo wao wameyaona wanaweza kufanya jambo ili yawe mepesi.
    Sasa tuanze kwa vipi Doris amekua akifanya ambayo anayafanya sasa ambayo baada ya kufanya kipindi hiki mengi ambayo aliyaongelea kama ya Serikali ya Uganda kumpa tuzo na kumkaribisha nchini mwao ili aweze kushirikiana nao bega kwa bega kwenye suala zima la kuwaokoa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani ‘NJITI’ na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia S. Hassan kutoa MILIONI 70 kwaajili ya kuchangia mfuko wake wa Doris Mollel Foundation. Yeye alikua anataka tu kufanya kitu kwaajili ya kuisadia jamii yake, ananiambia wakati analizungumzia hilo huku akitafuta jambo la kufanya ndipo Mama yake alipomfugua macho kwa kumuambia masuala ya watoto njiti, taa iliwaka sasa baada ya Mama yake kumkumbusha kwamba hata yeye alizaliwa kabla ya wakati. Alipoambiwa hivyo hakukua na kurudi nyuma tena baada ya hapo.
    Ananisimulia vikwazo ambayo aliwahi kupata mwanzo kuanzia nyumbani mpaka kwenye kutafuta hizo pesa ambazo zinasaidia mpaka leo hii, Doris ananihadithia jinsi ambavyo alipata bahati ya kuwa na watu ambao wamemsapoti na wanamsapoti mpaka leo kuanzia nyumbani kwa mume wake. Mtu ambae ndoa yao ilikua changa kuanza kuwa na vikao na watu mbali mbali mpaka usiku wa manane inamtaka mtu muelewa sana kuweza kuamini na kuyaacha mambo yaende. Mumewe alikua huyo mtu. Kwa ambao walimpigia simu mara ya kwanza baada ya kuona anchojaribu kufanya, watu kama Asas wa kule Iringa na wengine ambao wamekua wakijitokeza siku baada ya siku. Anakumbuka na anajua kwamba kutokata tamaa kwasababu ya changamoto kadhaa ndo ambapo kunamfanya awe ni mmoja ya watu wanao heshimika zaidi kwa mchango wake kwenye jamii yetu.
    Binafsi naamini huu ni mwanzo tu wa mazuri mengi ambayo binti huyu halisi wa ki Tanzania anajaribu kufanya. Sekta ya kulea watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati inahitaji hela nyingi na kwasababu ambazo Mimi na wewe hatuzijui kumekua na vifaa VICHACHE sana vya kuwahifadhi watoto hao mara tu wanapo zaliwa. Doris na Foundation yake amekua akipigana vita hiyo kuhakikisha vifaa vinapatikana sio mjini tu, hata mikoani ili kuokoa maisha ya watoto hawa ambao wengine huishia kwenye debe la taka kwasababu tu walizaliwa kabla ya wakati wao.
    Yangu matumaini utamuelewa na utapata nafasi ya kumfuatilia na kama utakua na lolote ambalo unaweza kuchangia basi yuko kwenye mitandao ya kijamii maana siku hizi kumpata mtu na kujua ambacho anakifanya imekua rahisi kupitia mitandao hiyo. Mimi najivunia sana yeye na yangu matumaini atafanikiwa sana kwenye sekta hii kama nasi tutaweza kumsaidia pale panapowezekana.
    Tunahitaji kina Doris tele kwenye jamii yetu maana vya kusaidia viko vingi.
    Yangu matumaini episode hii itasaidia kukufungua macho kwenye mengi ambayo jamii yetu ina uhitaji.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camSalamaNa
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • บันเทิง

ความคิดเห็น • 32

  • @ofmae-thebrainstech3501
    @ofmae-thebrainstech3501 ปีที่แล้ว +2

    Salama unafanya kazi kubwa sana kutuletea watu muhimu wanaozidi kutu'Inspire sisi wenye ndoto kubwa kuendelea kuzipambania. Allah akuweke sana I wish uendelee hivyo maana siku moja utakuja kunihoji hapo.

  • @parachichiFM
    @parachichiFM ปีที่แล้ว +6

    Tunaomba Salama na Madenge wa Twitter✊🏽

    • @jerrybasaya5377
      @jerrybasaya5377 ปีที่แล้ว

      Sasa mtu kama Madenge ana lipi la kuinspire?

  • @mtilimsita6675
    @mtilimsita6675 3 หลายเดือนก่อน

    I love this girl

  • @jazminehussein5004
    @jazminehussein5004 ปีที่แล้ว

    Finally nmesubiri sana

  • @JanethKomba-tv7jy
    @JanethKomba-tv7jy ปีที่แล้ว +1

    Always a get what a interview from my rolemodel ecejay

  • @ahmedhamdan8526
    @ahmedhamdan8526 ปีที่แล้ว +1

    ❤ safi

  • @eddiearts3713
    @eddiearts3713 ปีที่แล้ว +3

    Mwanamke ataki usawa anataka kuwa juu ...anataka power...na women cant control power...limitation ya power....hakuna cha nafasi nje ..utaka kufanya kitu ambacho sio chako...nyie ndio mnatengeneza imbalance and confusion mnafanya kazi ya shetani wazungu wamewajaza na mmejaa ....

  • @juliethbenard2358
    @juliethbenard2358 ปีที่แล้ว +1

    Salama na Dr.Isack Maro

  • @nataemsuya
    @nataemsuya 19 วันที่ผ่านมา

    Uvae dira ❎
    Uvae dera✅

  • @Ara_gadgets
    @Ara_gadgets ปีที่แล้ว +1

    Salama na madenge wa twitter 🔥

  • @Alkebulan-Afrika
    @Alkebulan-Afrika ปีที่แล้ว +2

    Salama na George Iron Mosenya

    • @Alkebulan-Afrika
      @Alkebulan-Afrika ปีที่แล้ว +1

      Huyu kaka ni mwandishi mzuri sana wa vitabu, na Dhani pia ndiyo mwanzilishi wa simulizi za sauti Tanzania.
      Nampenda sana nahitaji kufahamu zaidi kuhusu yeye na ninaamini anamchango mkubwa kwa vijana na waandishi wa vitabu chipukizi.

  • @Maggie_32
    @Maggie_32 ปีที่แล้ว +1

    Salama na Mama Alaska🤲🏾

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 ปีที่แล้ว +1

    Salama Na Diamond na Ray kigosi

  • @shaletmlaghui510
    @shaletmlaghui510 ปีที่แล้ว +2

    Leo nimekuwa wa kwanza😂😂🎉🎉

    • @MD-sz5ti
      @MD-sz5ti ปีที่แล้ว

      umepata bei gani

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว

    Good

  • @superserengeti9629
    @superserengeti9629 ปีที่แล้ว +1

    Salama na harmorapa🏃

  • @reinatave780
    @reinatave780 ปีที่แล้ว +1

    Afu mbona salama na doris wanafanana...aisee

  • @reinatave780
    @reinatave780 ปีที่แล้ว +1

    Salama na mpoki...

  • @Curioustraveller254
    @Curioustraveller254 ปีที่แล้ว +1

    Salama naomba umlete Hanscana

  • @itsbazil5787
    @itsbazil5787 ปีที่แล้ว +2

    Salama na mpoki

    • @reinatave780
      @reinatave780 ปีที่แล้ว

      Umejuaje yaan salama nampok iyo siku itakua poa mno

  • @mrfashion1687
    @mrfashion1687 ปีที่แล้ว +1

    Tunaomba salama na Millard ayo

  • @shadrackkamugisha4481
    @shadrackkamugisha4481 ปีที่แล้ว +1

    To be in the top of the hierarchy lazima uwe committed enough kushindana unatakiwa uwe Smart enough huwezi kutaka usawa usio kuwa na matokeo hasi nyie ambao ni radical feminist mnawadanganya wengine

  • @husnasaidi7247
    @husnasaidi7247 ปีที่แล้ว +1

    Salama na mwijaku plzz

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 ปีที่แล้ว +3

    Tunaomba Lukas wa jua kali

  • @danielbihuzu2365
    @danielbihuzu2365 ปีที่แล้ว +3

    First to comment can I please getting myself likes ??

  • @andrewmalekela3577
    @andrewmalekela3577 ปีที่แล้ว

    😝😂ngedere

  • @Yusufu940
    @Yusufu940 ปีที่แล้ว

    Dada Iyo upo katika Biblia mwanaume utakula kwa jasho ulimwengu wa Sawa sika masani kwa SS Kila MTU Ni jukumu lake

  • @madameg874
    @madameg874 ปีที่แล้ว

    Salama mbona umeacha kuweka majina na umaarufu wa mtu wakati wa interview, inavutia kusikiliza