Dizasta Vina - Mbuzi
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 7 ก.พ. 2025
- Official Lyric video of the record MBUZI as prepared and performed by Dizasta VIna. Off the studio album, A father figure
Stream/Download
TH-cam - • Dizasta Vina - Mbuzi
Mdundo - mdundo.com/son...
Boomplay - www.boomplay.c...
Audiomack - audiomack.com/...
Apple music - / mbuzi-single
Other Musical contents
Audiomack - audiomack.com/...
Boom play - www.boomplay.c...
TH-cam - / dizastavina
Mdundo - mdundo.com/a/2263
Spotify - open.spotify.c...
Apple music - / dizasta-vina
Deezer - www.deezer.com...
Spotify Playlist - open.spotify.c...
Connect with Dizasta Vina on social medias
Instagram - / dizastavina
Twitter - / dizastavina
Facebook - / dizastavina07
sw.wikipedia.o...
Business: Pan.authentik@yahoo.com
Website - bio.link/dizas...
Lyrics
Mbuzi alipata wadudu kwenye kwato
Iliathiri furaha na nguvu alizonazo
Mchungaji alihakikisha mbuzi ananawa
Aliondoa wadudu wote kisha akamweka dawa
Alikampangusa chawa akampa chakula kwa wakati
Akamjengea chumba kwa nafasi
Ajisikie huru, Akashika ratiba na itifaki
Muda ukapita afya mbuzi ikatamalaki
Mtaa ikahamaki ukasukwa uvumi
Kuwa bwana Kheri Anatoa muda kisha sumni
Japo hali yake ya uchumi ilikuwa ni duni
Aliuza matunda mboga chache na kuni
Hakuna siku mbuzi alipiga kelele kwa njaa
Watu walimwonea gere balaa
Alinawiri kwa kilele cha umaridadi
Majambazi walipiga misele kadhaa
Na usiku hauwi mwanana akisikia mbiu
Mbuzi akilalama kwamba anahisi kiu
Mchungaji alikuwa macho, Akatambua kuna
Magonjwa nyemelezi akavumbua chanjo
Mbuzi aling’ara alinona
Manyoya yalitawala kuashilia afya kila kona
Hakuwepo hata mwanga mmoja wa kuroga
Hata Waliojaribu kuchanja walikoma
Najiuliza maana ya upendo nini
Mpaka uwe na kingi ndio ushee?
Au pesa kipindi michango ya sherehe?
Au mzazi anayetamani uendelee?
Ndio maana anakulea ile umlee
Inasadikika kuwa upendo wa kweli ni kujali
Mama mzazi homa ikikushika tu halali
Tabasamu analokupa unaposhika Masarali
Ungekuwa hai ingekuwa kutoa mimba ni halali?
Wazalendo wanahitaji hela na nyadhifa
Wanalipwa kutetea sera za taifa
Wadini wanakumbatia itikadi na imani yao
Mpaka wanamwaga damu wenzao
Au mapenzi kwenye timu inapoingia mtimani
Unaumia inashika mkia na hauhami
Kufichiana dhambi tabia wanayoisifia masela
Au mjeshi anavyofia bendera
Nani anajua siri ya kupenda penda?
(Ni) kujitoa sadaka kwa ajili ya mwenza?
Wapo wanaosema kuwa kupenda ni ushupavu
Wanaumizwa wanachukia wanaandika vitabu
Ukijua mwenza wako ana mtu anampenda
Utampa nafasi aende upige moyo konde?
Mama akifariki na una dawa ya kusahau maumivu
Swali ni utakula vidonge?
Je upendo wa kweli ni mpaka aagize mungu?
Aliyesema ufuge paka alafu umchinje kuku
Amemmtoa mwanaye kama mdhamini msalabani
Awafie watu ambao dini hazifanani
Bado Mawazo yananisumbua nasinzia
Nawaza ingekuwaje tungechagua familia
Je mtoto angempenda baba angekuwa lofa?
Au Baba angemchagua mtoto angejua ni shoga?
Wanandoa tungekuweka kwenye Time Chamber
Muda urudi ungemchagua patner wako tena?
Wangapi wanawish wangepita sehemu hii?
Wangapi wangemchagua Justin Bieber na Jay Z?
Kabla ndoa haijakufunga pini
Jiulize kama mkeo angekuwa na wewe ka' ungekuwa chini?
Licha ya hizi nyimbo zinazofanya watu walie sana
Washikaji walingoja niwe msanii ndio niwe mwana
Pengine inabadili maana ya upendo
Na kuacha swali upendo je ni haja au matendo?
Mchungaji alifuga mbuzi alifuga na ajenda
Alimjali lakini si kwa sababu alimpenda
Kwani ilipofika sikukuu alitoa vitu
Sufuria jungu kuu akanoa visu
Yule mbuzi mzuri aliyenona sana
Ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama
read more about Mbuzi genius.com/Diz...
Nunua nakala yako ya A FATHER FUGURE Kwa whatsApp, Email au telegram. Tuma 10,000tzs au 650ksh kwa Mpesa +255 762 158 871 au Tigopesa +255 655 696 811 (Jina Edger Vicent Mwaipeta). Kisha tuma jina au sms ya malipo kwa hizo namba.
Ina nyimbo ngap?
Poa big brain rapper,ndyo maana DUBO alisema mc mbovu utakata tamaa ukimsikiliza dizasta we ni darasa tosha
Jamn mkuje sasa mnunue albamu yenye magoma makali.. Verse kali, beats kali.. Yani kilakitu kikali.
Despite being an MC, I bought this Albam na sijajutia ...nafikiri vijana wengi wangefata failsafA za dizasta maana nawaona Akina Karl max Napoleon hill na wengine wengi Sana ktk history...walioongelea kuhusu ukombozi wa kifikra...dizasta katuletea mawazo Yao in a simple form Kwa Lugha adhimu Sana ya Kiswahili akiilenga jamii yetu....AFF ni album yangu pendwa na nasikiliza Kila siku ubongo unapata Chakula...Dizasta is the master Art, and the only orchestrated symphony...
Pamoja san kaka👏👏🔥🔥🔥
Mchungaji alifuga mbuzi
Alifuga na agenda
Alimjali, lkn si kwa sababu alimpenda
Kwani.....
Ilipofika sikukuu ..alitoa vitu
Sufuria jungu kuu.. akanoa kisu
YULE MBUZI MZURI ALIENONA SANA , NDIE... ALIECHINJWA NA ADHUHURI ALICHOMWA NYAMA
Sehemu ya kwanza ya wimbo inaonekana kuashiria uhusiano kati ya mchungaji na mbuzi kama mfano wa uhusiano kati ya watawala na wananchi, au hata kati ya watu katika jamii. Mchungaji anawakilisha nguvu au serikali, wakati mbuzi anaweza kuwakilisha raia au watu wa kawaida. Mchungaji anajitolea kumtunza mbuzi, ikionyesha wajibu wa serikali kwa wananchi wake, lakini kuna maudhui ya utata kuhusu nia ya mchungaji - je, anamtunza mbuzi kwa upendo wa kweli au kwa sababu ya faida zake binafsi?
Sehemu inayozungumzia bwana Kheri inaonesha changamoto za kiuchumi na jitihada za kujikimu katika jamii. Ingawa bwana Kheri anajitahidi na hali yake ya uchumi ni duni, anaonyesha uvumilivu na ujasiri katika kukabiliana na changamoto za maisha.
Katika sehemu inayohusu upendo, wimbo unachunguza maana ya upendo na kujitolea kwa wengine. Inaleta mifano mbalimbali kuhusu jinsi upendo unavyoweza kueleweka na kutekelezwa katika maisha ya kila siku, iwe ni katika uhusiano wa kimapenzi, uhusiano wa kifamilia, au hata katika uhusiano kati ya watu na imani zao au utamaduni wao.
Mwisho wa wimbo unatoa picha ya kusikitisha ambapo mbuzi, licha ya kutunzwa na kustawi chini ya uangalizi wa mchungaji, anakatwa na kuliwa. Hii inaweza kuashiria udanganyifu wa watawala au nguvu kuu katika kutumia na kudhulumu watu wa kawaida kwa manufaa yao binafsi, huku wakionekana kama wachoyo au wasiojali.
Na hii verse ya mwisho ndio inasahihisha nia ya utata inayotajwa katika verse ya kwanza.
Verse ya kati, ni kama anaonesha tu upendo wa kweli ni nini, ili aje afanye hitimisho vema kwenye verse au eneo la mwisho
Upo sahihi mwamba
swadakta
Asantee kwa uchambuzi👏👏👏
Oya, huu mbona kama unamuhusu sana Lunya
@@MaulidiHimidi😂😂😂😂 ila watu n wasen
Rafiki zangu wengi wamekuwa wafuasi wa dizastavina baada ya kuwasikilizisha ngoma kazaa...Jana Tu Kuna mwana mmoja kaisifia sana hii ngoma alafu Leo umekuwa released aisee...tunaomba uandae show moja Yako mwenyew tutaingia kwa gharama yoyote.
Hem ngojeni kwanza. Mna hakika huyu jamaa ni mwanadamu wa kawaida.. aseeee big up brother Ediga
Coment Yangu Ni Ya 99 Dizasta Vineration 17 April 2024 when you read My Comment In 2099 Generation this Dude Was The Best & Genius
Aseee nmeelewa kuwa ukiskiza nyimbo za vina ni sawa na siskilizi nyimbo za wanadamu wenzetu..bado natafuta jina la kiumbe wa kumuita tofaut na binadam wa kawaida ila sijafankiwa kupata asee👊🏼🙌
Marafiki zangu wamebadilika na wamekuwa wakielimisha wengine kupitia mistari ya huyu mwamba wengine walipata wapenzi kweli huyu ni Mungu wa Rap 100%
SIO POA WE JAMAA UNAJUA
Jamaa kipindi unajiita dizasta vina ulikuwa unajua kuwa jina lako litakuwa linaendana na vina vyako mwanangu unajua sana sioni wakukufananisha nae
vina anajuwa sana
Waliorudiaa hio nyimbo Zaid ya.mara 10 piga like hapa Jamaa anauwasha Hakuna kama hii kichwaa
Nadiliki kusema tangu niwe mshabiki wa HIPHOP uyu mwamba ndio msanii wangu bora tangu niijue hiphop nikiipokea mikononi mwa prof J oyaaaaa 👊
Vina juu ya vina humu ndani Kuna bonge la disaster kiufupi hamna usalama🔥🔥❤
Nadhani ni muda wa kukubali sasa kuwa Dizasta vina ndie msanii mwenye maarifa mengi zaidi na ana namna nzuri zaidi ya kufikisha kuliko msanii yeyote wa hip hop kwa sasa
Asilimia 90 ya nyimbo za hip hop bongo humalizi hata verse moja unaona unazichosha tu ngoma za masikio yako, lakini ukimsikiliza muwa wa Dizasta vina unatamani hata uwe na verse kumi
Dizasta vina ndie msanii pekee ambaye huwa nakuwa na shauku sana ya kusikia his next project, bro is pure genius, too good for this industry
Sijui hii nyumba ya hip hop imebaki na mihimili mingapi mpaka ianguke ila Dizasta vina ni miongoni mwa mihimili inayofanya ili jumba la hip hop lisianguke
All the best Dizasta vina natumai utakuwa na Madusko yanayoendana na kipawa chako na juhudi ulizowekeza kwenye sanaa yako
Kweriii huyuu jamaa NI NYOKOMBILI 🙌🙌🙌🙌🙌🎧🎧🎧🎤🎤
Daaah peni imezingatiwa sana humu 🔥
Siku zinakuja hili Taifa litabadilika, vijana hawata kuwa inspired na machawa bali ngoma kama hizi....thamani yako itakuwa ya juu sana....Big Up Rasta
Nasema Hivi Hakuna cha fid q wala killer wala Stamina huyu Vina ndo Mwandishi Bora currently
straight up
Nimeelewa kipande cha mbuzi kinanikumbusha tukio la ngwajima kula muhumini wake.
Level 5 sorcerer kutoka far future!!
Ina pigwa violin inapigwa guitar Tunasikia neno baada ya neno..mpangilio mzuri wa Mashahiri hakuna yo-yo..
vina tungo imesimama mzee , n wateule wachache sanaaa tunaelewa izi chuma unatuachia keep moving broo tunakufuata
Vina juu ya vina humu ndani Kuna bonge la disaster kiufupi hamna usalama🔥🔥
mifumo ya taifa letu d..vina umeuwa...🙄🙄 yule mbuzi mzuri aliyenona sana ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama......
Dizasta nataka nimguse huenda sio binadam
Kweli dizasta akiwaka anaweza kumgeuza fid akawa sajna
Yanii huyui mwambaa anapigaa mamboo ambayoo hata fid q anakubalii mwambaa anajua kufichaa maana huyu ni kama langaa wa pilii ila mwambaa sijuii wakumgananisha naee dizastaa ni zaidiii yaoooo aiseeee
Hii ni aina ya mziki ninaoupenda haswa wakati nimetulia
Mimi naomba bifu ya vina na Rapcha tena 🤤...
BLACK MARADONA. SALUTE KWA MADINI BRO.
SOON HUU MZIKI UNAANZA KUA NO 1 ON TRENDING INSHAALAH
Utaratibu au mpangilio wa kutuma pesa kutoka Kenya hadi Tanzania ni upi kakangu @Dizasta Vina
Wewe mwamba unajua sana unafanya ubongo wangu utafakari sana
Vina! Vina! Vina,nimekuita ngapi? Noma sanaa
Mwanangu...! Sema tu kiki ndo hunaga but katika watu ambao ni blessed na branded upo kaka yan ni wewe na darassa yani ni brand za kitofauti mno na ladha kali❤❤. Mbeyahood.
Tulionunua Album day one tu ilivyotoka tunakosa cha ku-comment maana tulishachambua wimbo mpaka tukauchambua tena. Big Up Vina 🙌
Dizasta aseee sema media za bongo chai sana hawasikiagi hivi vyuma kutoka kwa mwana kuvichaka...
Sisi hatutaki media za Bongo....tununue Albam Kwa Dizasta ...Vina
👊 vina kisha somo, umesomeka vina uwezo wako hauwezi kupimwa kwa tuzo za pombe
UNatumia muda gani dizasta ku create golds kaMA hizi 🫡🤗🫢🫢🫢
Nakupenda Sana HIP HOP
Vina best songs 🎉🎉
Kudadekiiii unajua we Fara
Bro this guy deserves more support nunueni album much love dizasta.
ukijuwa mwenza wako ana anampenda
utampa nafasi aende upige moyo konde🔞🧠🎤🎤
Aliyeelewa hii ngoma anieleweshe tafadhari
Asante sana homie hujawai tufelisha wana.
@Mbuzi 💥💥💥
Ujawai kosea mzee. Nice
Yani huyu mwamba kashashindikana kabisaaa🙌🙌
hapa ndipo tunapopimwa IQ zetu huyu jamaa kama umezoea kuskiliza singeli huwezi muelewa bonge moja la ngoma
Kazi kali na ni kazi kubwa sana my brother 🔥🔥🔥🔥🔥
Nmedakia juu kwa juu,,,❤❤
DVN is G.O.T
Upendo nipamoja na kumtendea mwenzako mema,dhana ya upendo ni pana sana ila kwenye upendo jambo kubwa linalotafsir upendo ni uvumilivu, sabab binadamu ni lazima akosee tu so upendo ndio utafanya chuki isiwagawe anapokosea unaempenda au anaekupenda
Kazi nzuri sana mwana fanya kazi moja na bele 9 am sure it will be a banger
VINAAAAAA
Love from 🇺🇸, albam kali kama tindikali, Maji ya betri 🔥💯
Daaaah ifikie hatua watanzania hususa ni wanasanaa wamziki wa hip hop waungamane kwapamoja ili kuweza kuumudu uzito wahuyu jamaa
Unyama ni mwingi sana bro unajua sana 🔥💯✈️
Acha wajisifie nimarapa bora ila wewe ndo mwalim wao✊✊✊
🎉🎉🎉🎉
This ma'faka is an alien💥💥
Hii Hot Kabsa🔥
Kama vile nazama namuona mwamba kadondosha sijui niseme nizare la professa😂❤
Umetisha mkali wa vina 🔥🔥🔥
Nipo kwenye top 2 and iam not second ile ngoma uliua sana
Dizasta mungu azidi kukuweka uachie vigongo we ndo msanii wa hip-hop Wang wa milele
Serikali hainitambui na ushairi Wangu shule 😂👏👏👏🙌
Dizasta vinaaaaa umetisha sana nasubiri uchambuzi but you deserve great Honor in Hip-hop Industry
Mbn kama bado haija isha mkuuu🎉
Uyu mwamba ni makl wa hip hop
Dizasta vina ni Extraordinary 😂💥💥
Mwisho wa siku mbuzi akaliwa nyama😂
Oya wanangu wa mziki mzuri kama huu tusiishie ku like na kusifia tununuue ngoma na tisapoti mziki mzuri ili mwana aendelee kutudondoshe ngoma Kali kama hizi Kuna vitu vingi vya kuimba ila wasanii wa bongo banaa mapezi mapenzi wana boa sana dizasta tuna kuaminia wapige msasa wasani wa mapenzi kila siku❤
Hivi dizasta unavyo andika wimbo kichwa kinakua kinauma au kuna machine unatumiga kutungia nyimbo zako, mm nahis sio kichwa cham2 kinacho andikaga
Uyu mwamba kma akili yako ya kawaida huwezi kumuelewa kbsa###@dizasta🔥🔥🔥
This man is not a human asee dizasta ni monster
Broo uko vizuri up stair Mimi shabiki yako iam above 50 big up keep it up
Japo hali yake ya uchumi ilikuwa duni liuza matunda mboga chache na kuni
Nasubiria uchambuzi wake,
Mnasifia sana tungo za vina ila mnajifanya kama hamuoni namba za kutuma iyo miamala mazee afu kesho na kesho kutwa vina aka pause music mtasema vina kapotea
Fact buddah
Uyu Dizaster vina anapaswa kuwa msanii wa juu sana
Huyu jamaa ni noma 🔥
Sema kuna sehemu Dizasta vina umeandika mchugaji badala ya mchungaji (Sehemu ya mwisho mchugaji,msiba wa mbuzi badala ya sehemu ya mwisho mchungaji,msiba wa mbuzi)👍
Washikaji walingoja niwevshujaa ndo niwe mwana😮😮😮
Stamina Dizasta Nacha toxic Roma Nay killer nawakubar kchz
Mchungaji asitufanyue ivo bs dah salute
Jamaa kabalikiwa kipaji chakweli ❤
Goat 🐐
Oooh no Dizasta... Mbeya we feel high..reee to have you wish u well 🔥 fire man straight from the cold hooray green town.
What the hell bro🤯🤯. Mad Genius Vina. Big up and salute from🇰🇪
Kk umetisha
Black maradonaa.....
Vinaaaa🙌🏾🙌🏾🙌🏾
Huyu mwamba nilichelewa kumjua ila nilivomjua nikamfanya Best RAPPER wa muda wote haiwezi kupita siku bila kusikiliza ngoma zake kama 5, nikianza na TRIBULATION, ACHIA JALA, WACHEZAJI WA TIMU, NO ONE IS SAFE, (zote) na HATIA (Zote)
Likewise
We proud of you rasta, endelea kutupa ivi vitu🇹🇿
This kind of vina hatuna tena kwa dunia hii.
Walipita wengi lakn huyu ndo msanii wang Bora wa hip-hop
nikiwa mkubwa niwe kama wewe, sijui unamaanisha Nini huu wimbooo😢😢😢😢😢😢😢
Hivi vina ni dizasta 👀🎉
Kubababakee umu tu unajua sana mwanangu sema ndo ivo hauishi angani