MITUNGI 400 YA GESI YAGAIWA KWA WANAWAKE MKURANGA, BALOZI WA HESHIMA AZUNGUMZA.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.ย. 2024
  • #wanawake #samiasuluhuhassan
    Katika kuunga juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanawake wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kutunza mazingira.
    Akizungumza mapema leo Aprili, 4 ,2024 Mwanzilishi wabTaasisi ya Reflection Foundation na Balozi wa heshima Toka Visiwa vya Shelisheli, Mary Vonne Pool amesema kuwa wameona kuja kugawa mitungi hiyo ya gesi kwa kina mama wanaoishi maeneo ya Kisele, Kinene na Mwalisembe,Mkuranga kata ya Mwasembe lengo ni kuwafanya wakina mama wapikie nishati safi.
    "Sisi kushirikiana na Oryx Energies tumetoka mitungi hii ya gesi ili kuwarahisishia wakina mama katika shughuli zao za kila siku na kuacha kukata Kuni pamoja na kupunguza gharama za ununuzi wa Mkaa ili mazingira yetu yaendelee kuwa salama kwa sababu miti inapikatwa inasababisha jangwa na kukosa mvua na kusabisha kukosekana kwa chakula.
    "Hivyo niwaomba wakina mama wote ambao leo mmepata fursa hii, kuweza kutumia hiyo gesi na si kuuza kwa kuwa itawarahisishia katika matumizi ya jikoni na pia inawarahishishia kutumia muda mfupi katika mapishi,amesema Mary.

ความคิดเห็น •