Kutoka SKUA, Tukio zima Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Lt Gen YH Mohamed Akipokea ITHIBATI kutoka NACTE

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 ก.พ. 2025
  • Katika kuongeza Taaluma kwa Maafisa na Askari, Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga(SKUA) iliyoko Kange Jijini Tanga imepiga hatua kubwa sana katika nyanja ya Elimu, Mnamo Tarehe 07/09/2020 Historia imeandikwa baada ya kufaniikiwa kupata ITHIBATI kutoka Mamlaka ya Kusimamia Elimu ya Ufundi Nchini NACTE, hii inamaana kuthibitishwa kutoa Elimu ya Ufundi wa Ndege kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada ambapo Kundi la kwanza linatarajiwa Kuanza Mwezi October 2020
    Sherehe za Uzinduzi na Upokeaji Ithibati hio zilifanyika SKUA Jijini Tanga ambapo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Afande Luteni Jenerali YH Mohamed alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi. Aidha Kaimu Mkuu wa Shule Brigedia Jenerali MN Mkeremy alifafanua namna ambavyo Shule (SKUA) imejipanga na kujizatiti kuendesha Kozi hio, “Tumejipanga vizuri na Tutaanza mwezi Octoba 2020 kwa Wanafunzi wachache na baadae tunategemea Kudahili Wanafunzi hata ambao sio Wanajeshi” Alisema Mkuu wa Shule
    Akihutubia Maafisa na Askari kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi,i Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Afande Luteni Jenerali YH Mohamed alitoa Shukrani kwa NACTE kwa kuwa na imani na Jeshi, aidha alitoa mwito kwa Shule Kujikita Kuzalisha Mafundi (Techicians) kulingana na hitajio kubwa lililopo kwa sasa
    Hata hivyo Mafanikio haya yote ya Upatikanaji wa Ithibati yamechagizwa na SKUA yenyewe kukamilisha baadhi ya Miundombinu muhimu kama Madarasa, Maabara na Ofisi, ingawa bado juhudi zinaendelea kwa kushirikiana na Makao Makuu ya Jeshi ili kufikia viwango vya juu.
    #wizarayaulinzi #jwtz #jkt

ความคิดเห็น • 12

  • @yusuphmakangemakange4474
    @yusuphmakangemakange4474 ปีที่แล้ว

    Ewe mungu muumba mbingu nakila kichopo dunian ibariki Tanzania ibariki Africa I love you Tanzania I love Africa mungu muumba mbingu nakila kichopo dunian bariki jeshi letu lipe nguvu pia ninaiyomba serekaly ijiweke sawa kuleta zana za kivita zakisasa ili jeshi liwe imara zaidy na zaidy wazi afande

  • @husseinmaula5914
    @husseinmaula5914 3 ปีที่แล้ว +4

    Juzi nilikua safari usiku na gari maeneo ya bagamoyo nikakuta jeshi letu likiwa mazoezi walinisaidia kunipa signal maana hatua chache mbele Kuna roli liliharibika mda mchache hata tryangel walikua hawajaweka huu ndio uzuri wa jeshi mungu alilinde daima milele.

  • @husseinkatumpula6129
    @husseinkatumpula6129 3 ปีที่แล้ว +3

    Kumbe afande mkeremi alikuwa ana mwili bonge 👏👏👏🤣🏃

  • @shukurkatembo2807
    @shukurkatembo2807 4 ปีที่แล้ว +3

    Congratulations to TPDF.. Tunahitaji wapewe elimu zaidi kwa kina na sisi tuanze kuunda walau kwa underlisence.

  • @abdihq4228
    @abdihq4228 3 ปีที่แล้ว +1

    Very respectful army

  • @ebencobbs7036
    @ebencobbs7036 3 ปีที่แล้ว +1

    Please do well to write it in English for us🙏

  • @karimmkejina980
    @karimmkejina980 4 ปีที่แล้ว +5

    Umeona kama nilivyoona mimi bodigard wa mzee magu wa zamani

    • @shukurkatembo2807
      @shukurkatembo2807 4 ปีที่แล้ว +1

      Hakika brother Brg. Gen M. Mkeremi

    • @hendrycomonsiwenga1084
      @hendrycomonsiwenga1084 3 ปีที่แล้ว

      @@shukurkatembo2807 Hakika ujakosea kabisa, ilo ndiyo jina lake sahihi. Tuko pamoja PT. Ahsante

  • @hermanfundi605
    @hermanfundi605 3 ปีที่แล้ว

    Huyu mwanajeshi niyule bodigadi wa kikweye

  • @nyamtigaibrahim530
    @nyamtigaibrahim530 3 ปีที่แล้ว +1

    Hapo Cfa Ni Kukaa Nyuma Maana Kama Nyimbo Huifahamu Full Kuangushia Tu Sasa Omba Mp Asikuone Akikuona Baba Umeisha Ahahahahahahahahahahahahahahahah Uerekeo ni Santiago Bernabeu

  • @gregorymtega6556
    @gregorymtega6556 3 ปีที่แล้ว

    Tpdf mfano wa kuigwa