Utunzaji wa Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji BILA VIFO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 ธ.ค. 2024
  • Muongozo wa Uleaji wa Vifaranga wa Kienyeji
    Mfugaji ni vizuri ujiandae kupokea vifaranga kama ambavyo hua unajiandaa kupokea mtoto kabla ya kujifungua.
    Maandalizi hayo ni kama yafuatayo:-
    1. Baada ya ujenzi wa banda kukamilika, banda lifanyiwe usafi wiki mbili kabla ya kuingiza vifaranga.
    2. Wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga, matandiko yaliyosafishwa kuondoa vumbi yawekwe bandani, na banda zima lipuliziwe dawa (disfectant). Hakikisha kimo cha matandiko ni angalau inch 3
    3. Tengeneza bruda kwaajili ya kuzuia joto lisipotee na andaa vifaa vya maji, chakula na magazeti yatakayo tandikwa juu ya Matandazo ndani ya bruda kuwasaidia vifaranga kutofautisha chakula na matandazo.
    N.B: Badilisha magazeti hayo kila unapoona yamechafuka ndani ya siku 3-4 za mwanzo ambao atakua mwisho wa matumizi.
    4. Kabla vifaranga kuingi bandani, bruda lipashwe joto kwa masaa sita huku vifaa vya maji yenye glucose na vitamin vikiwa ndani ya bruda.
    Baada ya masaa hayo vifaranga waingizwe bandani na kuruhusiwa kunywa maji yenye glucose kwa masaa 2 mfululizo.
    5. Hakikisha Kuna joto la kutosha muda wote ndani ya bruda ili kuzuia ugonjwa wa vichomi (Pneumonia). Unaweza kutumia vyungu, bulb ya 100w, chemli au vifaa vingine vya umeme au gesi.

ความคิดเห็น • 21

  • @Kevinkangethe-254
    @Kevinkangethe-254 4 หลายเดือนก่อน

    Hae,asante kwa masomo mazuri ningependa kuuliza nawezaje kuimarisha kuku wangu waague mayai yote nliyowaekea,kevin kutoka Nairobi

  • @evancegidion9155
    @evancegidion9155 6 หลายเดือนก่อน

    nimeelewa ahsante sana kwa darasa zuri kwa somo

  • @OliviaAdolf
    @OliviaAdolf 5 หลายเดือนก่อน

    Nimeipenda sana

  • @nancylubango6394
    @nancylubango6394 2 ปีที่แล้ว

    Asante sana for sharing

  • @Felisterkihako
    @Felisterkihako 7 วันที่ผ่านมา

    Asante

  • @rukinishathadeo7215
    @rukinishathadeo7215 ปีที่แล้ว +1

    Naomba unisaidie namba yakoo samahan lakin

  • @efaboy2993
    @efaboy2993 2 ปีที่แล้ว

    Nataka kujua hivi nikiwa nakuku 5 wawiili wakataga halaka watatu wakachelewa lakin nahitaji waanze kuatamia pamja je mayai yakuku walio tangulia kutaga hayawez kuhalibika

  • @anicethngeleja7411
    @anicethngeleja7411 3 หลายเดือนก่อน

    Mmmh mwezi wakubwa hivi???

  • @marrymushi1515
    @marrymushi1515 2 ปีที่แล้ว

    Je? Vfaranga wote wameanguliwa na kuku au machine??

  • @rukinishathadeo7215
    @rukinishathadeo7215 ปีที่แล้ว

    Ili niweze kipata chakula cha vifatangaa

  • @dometngwenga3588
    @dometngwenga3588 ปีที่แล้ว

    Kiukweli najifunza kitu hapo

  • @zanzibargraphicdesign6978
    @zanzibargraphicdesign6978 2 ปีที่แล้ว

    Kibanda chako kilikua na ukubwa gani kwa vifaranga hao wote

  • @yusuphjulius1638
    @yusuphjulius1638 ปีที่แล้ว

    Chakula cha pilate ndo kikoje hicho

  • @kelementbushishi3687
    @kelementbushishi3687 ปีที่แล้ว

    Nimepesa sana ufugaji wako vp naweza kupata namba yako ili tuwasiliane zaind

  • @nancylubango6394
    @nancylubango6394 2 ปีที่แล้ว

    How many kilo grams of starter u have used so far

  • @libanslessons23
    @libanslessons23 2 ปีที่แล้ว

    How old are these chicks

  • @BakariMkulu-lq4gk
    @BakariMkulu-lq4gk ปีที่แล้ว

    Bakari mkulu 0:38

  • @amosmsuya2333
    @amosmsuya2333 2 ปีที่แล้ว

    Na dawa ipi Ni nzuri kuzuia mafua ya kukuu?

  • @yustafaustin964
    @yustafaustin964 2 ปีที่แล้ว

    Chanjo vipi inakuaje

  • @eliaslyuki6516
    @eliaslyuki6516 2 ปีที่แล้ว

    Hi no to

  • @giftnjegere4267
    @giftnjegere4267 2 ปีที่แล้ว

    Hao kuku wakubwa wanaumhim gani kuwachanganya na vifaranga