TCAA Yakifungia Chuo Cha Tanzania Aviation College
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 6 ม.ค. 2025
- Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imekifungia Chuo kinachotoa mafunzo ya usafiri wa anga cha Tanzania Aviation College chenye matawi yake jijini Dar es Salaam, Arusha na Mwanza kwa kukiuka taratibu za kuendesha vyuo vya usafiri wa anga. Hatua hiyo imetangazwa tarehe 30/09/2020.#TCAA
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba