HATIMAE ILE BANDARI YA 'WATER TAXI BOAT' RAMANI IMETOKA RASMI LEO, SMZ YATILIANA SAINI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ม.ค. 2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
    Mwinyi, amesema serikali ina kila sababu ya kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya baharini ili kuweka mazingira mazuri ya usafiri wa bahari kwa wananchi wa Zanzibar na wageni wanaoingia nchini .
    Dk. Mwinyi alieleza hayo mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini
    mkataba wa ujenzi bandari ya abiria Mpigaduri Maruhubi baina ya wizara
    ya Mawasiliano na Uchukuzi chini ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Khadija
    CHINI YA na kampuni ya Zanzibar for a Brighter Future ZF Devco Ikulu
    Mjini Zanzibar.
    Alisema serikali imeamua kujenga bandari ya mpiga duri kutokana na
    bandari ya Malindi ya abiria kuzidiwa,kuleta msongamano mkubwa na hata usalama wake kuwa mdogo.
    Aidha alisema mradi huo itakuwa mfano mkubwa wa ushirikiano wa sera
    ya serikali na sekta binafsi ya PPP katika kufikia malengo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
    Alibainisha kuwa serikali haikuweza kuivunja bandari ya Malindi bali
    imeamua kujenga eneo jengine la mpiga duri ambayo itahusisha maeneo
    tofauti ikiwemo eneo la abiria la kisasa.
    Dk. Mwinyi alibainisha kuwa mradi huo utakapokamilika ni ni fursa kubwa
    ya biashara na wameamua kuingia makubaliano ili nchi iweze kufaidika
    kiuchumi na kuondosha changamoto ya usafiri kwa wananchi wa Zanzibar
    hasa kwa wasafiri wanaotoka kisiwani Pemba na Dar- es salam.
    “Abiria waopita hapo ni kati ya 5000 mpaka 12,000 kwa siku hiyo ni fursa
    kubwa ya biashara, wenzetu tumezungumza nao na tumeshirikiana na leo
    tumeamua kwa pamoja kuingia mashirikiano ili kuweza kufaidika
    kibiashara, kiuchumi na pia kutoa huduma bora kwa wananchi wetu,”
    alibainisha.
    Rais Mwinyi alibainisha kuwa serikali imejipanga kuwa na usafiri wa aina
    mbalimbali ikiwemo usafiri wa barabara kwa kuwa na mabasi ya gesi na
    umeme ,treni na usafiri wa majini kwa kutumia water tax.
    .....................................................................................................
    Angalia Video Hii Mwanzo mwisho , Kisha Subscribe ili uendelee Kupata Habari Zote.
    Follow Ktv Tz Online
    Facebook | KTV TZ ONLINE
    INSTAGRAM |@ktv_tz_online
    Wasiliana nasi kupitia number
    +255 717 619 834
    Ktv Tz Online Journalists
    cc: Sadia Rashid
    cc: Sauti Byego
    Camera Department"
    Dadi Ali
    Omar (OJ)
    Nassor Shaibu
    Abdallah Juma
    Editors:
    Juma Maulid
    Dadi Ali
    Video Zingine:
    Angalia hapa - Diamond Platnumz Alivyolisha watoto yatima
    - Ali Kiba akiwa Oman
    • ALICHOKIFANYA DIAMOND ...
    • NI KWELI ALI KIBA AMNU...

ความคิดเห็น • 23

  • @user-nn6id3dd6v
    @user-nn6id3dd6v 6 หลายเดือนก่อน +6

    Wewe ndo rais wa kweli kura yangu ipo kwako baba usijali inshaallah

  • @aaahadventures4214
    @aaahadventures4214 6 หลายเดือนก่อน +5

    Excellent

  • @Asilimedia
    @Asilimedia 6 หลายเดือนก่อน +7

    Hapa Zanzibar tumepata Rais ❤❤❤❤

  • @ProfessorLee-xs4qo
    @ProfessorLee-xs4qo 6 หลายเดือนก่อน

    mashallah,hekko Dkt.Mwinyi Kwa kupig hatua kubw na kukaza mkanda na Buti to our modern znzbr,,,so good strong foundation to znzbr.

  • @scoutpwanimchangani6711
    @scoutpwanimchangani6711 6 หลายเดือนก่อน +4

    Mheshimiwa hata akimaliza Muda wake wa uongozi itakuwa ameifumuwa zanzibar

  • @husnamohamed9245
    @husnamohamed9245 6 หลายเดือนก่อน

    Nzuri mashallah mmungu akueke doctor mwinyi watu watapata kazi

  • @johnbernad3990
    @johnbernad3990 6 หลายเดือนก่อน

    Mungu akulinde Rais wetu akukinge na maadui bado tunakuhutaji saana kwenye kisiwa chetu yajayo ni neema 💪

  • @mangulimanguli3974
    @mangulimanguli3974 6 หลายเดือนก่อน

    Rudi Tanganyica Mwinyi tumrudishe Mama yao ww ni mfano wa Magufuli unapiga kazi sana Hongera

  • @Qur-x4i
    @Qur-x4i 6 หลายเดือนก่อน +2

    Imekaa sawa tulikukubali kabla hujawa rais

  • @suleimansaid769
    @suleimansaid769 6 หลายเดือนก่อน +4

    Mh kwakwl unazidi kuiheshimisha Zanzibar

    • @mangulimanguli3974
      @mangulimanguli3974 6 หลายเดือนก่อน

      C mlisema mbara arudi kwao Njooni mumchukue Mama enu Turudishieni Mwinyi wetu

  • @ahmednajad5608
    @ahmednajad5608 6 หลายเดือนก่อน +3

    Naona kama dkt mwinyi hajatoka ccm

  • @kimsamir965
    @kimsamir965 6 หลายเดือนก่อน

    VIZURI SANA

  • @user-ex6sh1rl4d
    @user-ex6sh1rl4d 6 หลายเดือนก่อน +2

    Na zile sain za mpiga duri vp zile chelezo viwqnda vyuo

    • @ktvtzonline
      @ktvtzonline  6 หลายเดือนก่อน +1

      kilichofanyika leo ni utiaji saini mkataba wa ujenzi bandari ya abiria Mpigaduri Maruhubi,

    • @Allybinamour
      @Allybinamour 6 หลายเดือนก่อน

      khaswaaa, kuna mpga duri ya meli za makontena ilitiwa sain toka dk mwinyi alipoingia tu madarakani, kuna ya maruhubi ya kusarifu na kuhifadhi samaki ilitiwa saini tayar. au labda zitaanza zote kwa pamoja.

    • @abadalaali7736
      @abadalaali7736 6 หลายเดือนก่อน

      ​@@Allybinamourilikua ni feasibility study sio ujenzi

  • @mohdseif2459
    @mohdseif2459 6 หลายเดือนก่อน +1

    Na ule mradi wa kujenga mji wa malindi umeishia wapi au ndio kila sku kutia saini tu

    • @MohamedAhmada-ie7ke
      @MohamedAhmada-ie7ke 6 หลายเดือนก่อน

      Ukiskiliza vzur ule mradi wa malindi wala hutauliza maana mbaka ihame bandari ya malindi au hukusikia vzr

    • @mohdseif2459
      @mohdseif2459 6 หลายเดือนก่อน

      @@MohamedAhmada-ie7ke tusubiri tuone ayo yalotiwa sauni leo then njoo tena hapa baada ya miaka 7 unipe mrejesho

    • @MohamedAhmada-ie7ke
      @MohamedAhmada-ie7ke 6 หลายเดือนก่อน

      @@mohdseif2459 Tukijalwa uhai na uzima In Shaa Allah

  • @omarsaid7153
    @omarsaid7153 6 หลายเดือนก่อน

    Mazonge tu !

  • @Qur-x4i
    @Qur-x4i 6 หลายเดือนก่อน +1

    Imekaa sawa tulikukubali kabla hujawa rais