HII AIBU!CHAKE-WETE WAMEKOSA NINI?HAKUNA SIASA KWENYE HILI JAMBO| SIASA YETU KUTENGENEZA BARABARA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 20 ต.ค. 2024
  • Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema hajarizishwa na maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Chake-Wete inayojengwa na Mkandarasi Kampuni ya MECCO iliyotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu lakini hadi sasa ujenzi huo bado Unasuasua .
    Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara hiyo ambayo kutokukamilika kwake imekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wanaoitumia barabara hiyo kwa shuhuli mbali mbali za kujitafutia kipato.
    Mhe. Makamu wa Pili wa Rais ameitaka Kampuni ya MECCO kujitathmini na kufanya uharaka wa kukamilisha ujenzi wa barabara hio ili kurejesha Imani kwa wananchi ambao wanapata usumbufu kutokana na uchakavu wa barabara hiyo na endapo watashindwa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa watakuwa wamejinyima fursa ya kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
    Amesema kuwa kumekuwa na ubabaifu wa hali ya juu kwa baadhi ya wakandarasi wanaojenga miradi ya Serikali kwa kutotimiza makubaliano ya mikataba jambao ambalo linaisababishia hasara kubwa Serikali kwa kutofikia malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo.
    Akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa soko la samaki na mboga mboga lililopo Mzambarau Takao na soko la wajasiri amali Kifumbikai Wete Makamu wa Pili wa Rais ametoa mwezi mmoja kwa wananchi waliokwisha kulipwa fidia kuondoka katika eneo hilo ili kupisha ujenzi wa soko pamoja na kupisha utanuzi wa Barabara.
    Amesema kuendelea kuwepo kwa wananchi hao katika eneo hilo kunakwamisha maendeleo ya ujenzi huo ambao kukamilika kwake kutawaondolea wananchi wa Mzambarau Takao na vijiji jirani changamoto ya kufata huduma ya soko maeneo ya mbali pia litatoa fursa kwa wananchi kuweza kufanya biashara zao katika mazingira mazuri na salama.
    Aidha Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Kampuni mbali mbali zinazojenga miradi ya maendeleo Zanzibar ili kuhakikisha miradi hio inamalizika kwa wakati uliopangwa na kuwaondolea kero wananchi wa Unguja na Pemba.
    Kwa upande wao Mawaziri wa Wizara zenye dhamana ya kusimamia miradi hio wamesema kuwa watahakikisha kwa hali yoyote ile miradi ambayo ipo chini wa wizara zao inamalizika kwa wakati uliopangwa ili kuendana na dhamira ya Rais Dkt Hussen Mwinyi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
    Mawaziri hao wamewataka wakandarasi wa ujenzi wa miradi hio kuhakikisha wanaongeza nguvu kazi za kutosha sambamba na kuongeza kasi ya ujenzi ili kumaliza mradi hio kwa wakati kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
    Nao wakandarasi wanaojenga miradi hio wamesema ujio wa Mhe. Makamu wa Pili wa Rais utatatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa malipo jambo ambalo husababisha kuzorota kwa ujenzi wa miradi hiyo.
    Hata hivyo wamemuahidi Mhe.Makamu wa Pili wa Rais kuwa watafanya kazi kwa jitihada zote ili kuhakikisha wanakamilisha miradi hio kwa wakati uliopangwa.
    Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Mhe. Makamu wa Pili wa Rais NI MRADI WA BARABARA YA CHAKE-WETE, MRADI WA SOKO LA SAMAKI NA MBOGA MBOGA MZAMBARAU TAKAO, SOKO LA WAJASIRIAMALI KIFUMBIKAI, UJENZI WA KITUO CHA AFYA JADIDA, UJENZI WA NYUMBA ZA MADAKTARI KINYASINI, KUKAGUUA MAENDELEO YA HOSPITAL YA WILAYA KINYASINI, UJENZI WA KITUO CHA AFYA KINYIKANI NA UJENZI WA KITU CHA AFYA KIUYU MINUNGWINI WETE PEMBA.
    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wananchi wa Mzambarau Takao mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa soko la samaki na mboga mboga linalijengwa katika eneo hilo akiwa katika ziara zake za kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa Kisiwani Pemba.

ความคิดเห็น • 22

  • @jumamohamed3168
    @jumamohamed3168 2 หลายเดือนก่อน +4

    Kwani hizo kampuni za ujenzi amezichagua nani ili zijenge hizo barabara si nyiny wenyewe .acheni mambo yenu ,ina maana yele anayosema Jusa yanaukweli sana tena .

  • @rashidomar2771
    @rashidomar2771 2 หลายเดือนก่อน +1

    Muheshimiwa ndio umeona leo ,,kila mtu anajua kama kampong hiyo haina uwezo wa kujenga hapo,,sijui kwa nini mnailea sana

  • @AbdulRahmanAliy-sr7gw
    @AbdulRahmanAliy-sr7gw 2 หลายเดือนก่อน +1

    Watu walikua hawana sehemu tu madamu mushatengeza kilicho baki ni kutoa tu elimu na kupunguza kodi basi

  • @natafutamatatizo4382
    @natafutamatatizo4382 2 หลายเดือนก่อน +2

    DR MWINYI ANATAFUTA WATA WA KULA NAO, NDIO ANAWAPA MIKATABA. HAYA NDIO MATATATIZO YA MAJAMBAZI YA CCM

  • @MattarMohammed-f5v
    @MattarMohammed-f5v 2 หลายเดือนก่อน

    Ccm Zanzibar ni wezi na wauwaji hawana mradi wala maendeleo kwa Zanzibar

  • @hajiabdalla5772
    @hajiabdalla5772 2 หลายเดือนก่อน

    Jamaa mishipa hao kazi mdomo tu na kulaumu

  • @alzawahirabdallah2299
    @alzawahirabdallah2299 2 หลายเดือนก่อน +1

    Mwendo wa kobe hatuna haraka

  • @lusakaone7782
    @lusakaone7782 2 หลายเดือนก่อน

    Watu wamekosa nn jibu wanalo 😅😅

  • @Allybinamour
    @Allybinamour 2 หลายเดือนก่อน

    kuna mwakilishi mmoja wa pemba alisema kuhusu uzorotaji wa ujenz wa barabara za pemba huyo huyo wazir khalid ndo alomkrash.naomba wazir na leo ampinge na huyo makamo wa pili

  • @princesaha3262
    @princesaha3262 2 หลายเดือนก่อน

    Uchaguzi unakaribia Lazima mutengeneze lkn barabara hyo imekaa miezi kadhaa ukipita kama unatokea wete au chake utakuta Scaveta limefanya kutu na vumbi Kali.

  • @AliMahfudh-ze2ig
    @AliMahfudh-ze2ig 2 หลายเดือนก่อน

    Walaji wakubwa nyinyi😂😂😂

  • @Muhairy
    @Muhairy 2 หลายเดือนก่อน

    Acha ushamba ww hemedi kutoka kwneye ukui wa mkoa mpaka makamo wa raisi acha kutucharukia huna lolote na mara hii munaondoka ccm mushauwa sana 2020 sasa ujinga ujinga huu sasa bas

  • @ibrahimame9805
    @ibrahimame9805 2 หลายเดือนก่อน

    Hahaaaaa ccm hiyo ya ruto

  • @Pemba680
    @Pemba680 2 หลายเดือนก่อน

    Serekali fukuza mkandarasi na faini juu
    Hii ndio faida ya kutuletea wakandarasi wabovuuuu pemba matokeo yake ndio haya

  • @hajiabdalla5772
    @hajiabdalla5772 2 หลายเดือนก่อน

    Wataweka mameza yao barabarani mishipa hiyo

  • @mukhtaromar-g5p
    @mukhtaromar-g5p 2 หลายเดือนก่อน

    Ama kweli anayo yasema. Jusa ni ukweli mtupu Ccm haitufai 2025 tunaenda na othman kua rais wetu kuelekea mamlaka kamili

  • @princesaha3262
    @princesaha3262 2 หลายเดือนก่อน

    Tatzo hamuwezi kuleta maendeleo Pemba

  • @AliMahfudh-ze2ig
    @AliMahfudh-ze2ig 2 หลายเดือนก่อน

    Na badooooo😂😂😂

  • @alinassor391
    @alinassor391 2 หลายเดือนก่อน

    Kwnn soko jipya livuje

  • @omarmohammed5157
    @omarmohammed5157 2 หลายเดือนก่อน

    😈😈😈😈😈