JIFUNZE KULEA VIFARANGA,maandalizi ya bruda,kupokea vifaranga na kulea vifaranga wa siku 1.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ม.ค. 2025
  • NJIA BORA YA KULEA VIFARANGA Ni jambo la kuzingatia kwamba vifaranga (Umri wa siku moja) wanapata joto la kutosha katika majuma matatu ya mwanzo wa maisha yao, vinginevyo watakufa. Ni lazima waangaliwe vizuri, watunzwe katika hali ya usafi na kulishwa kikamilifu ili waweze kutoa matunda mazuri hapo baadaye. KUANDAA CHUMBA AU BANDA LA KULELEA VIFARANGA Usafi ni jambo la lazima, chumba au banda ambapo vifaranga watawekwa sharti lisafi shwe kwa kusuguliwa mara mbili au tatu kwa kutumia sabuni au maji. Kabla ya vifaranga hawajawekwa ndani liwe limekauka vizuri. Vyombo vya kulishia chakula na kunyweshea maji pia vioshwe viwe safi . • Mlango wa sehemu ya kulelea vifaranga ifungwe vizuri kuzuia upepo kuingia, pawepo na vidilisha angalau viwili kwa kuingiza hewa na mwanga. • Sakafu ifunikwe vizuri kutumia majani makavu au malanda na magazeti kwa wiki ya kwanza kuzuia baridi. Kazi hii ifanywe siku moja kabla ya kuwasili vifaranga. • Vifaranga wanahitaji joto la kutosha siku za mwanzoni. • Kama kuna umeme basi vifaranga wapewe joto kutumia balbu yenye moto mkubwa (Infra-red lamp) kama hakuna umeme taa ya mafuta inaweza kutumika moja kwa kila vifaranga 100 ikitundikwa nchi 18 kutoka sakafuni kwa siku chache za mwanzoni. • Chakula na maji viwepo ikiwezekana kwa kutumia makasha yaliyosambazwa ili vifaranga waweze kula na kunywa kwa urahisi kuanzia siku ya kwanza. • Tumia vyombo vya kulishia chakula na kunyweshea maji vyenye vipimo sahihi. Kwa mfano chombo cha kulishia chenye urefu wa futi 3 kinatosha kulisha vifaranga 50 na chombo cha maji kimoja kwa vifaranga 25. MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIZA VIFARANGA BANDANI Ingiza kasha lenye vifaranga ndani ya chumba au banda la kulelea, washa taa, vyombo vya kulishia vikiwa vimejazwa chakula na maji ya kunywa yapo. Sakafu itakuwa tayari imefunikwa na majani makavu au malanda ya mbao na kisha magazeti. Toa vifaranga ndani ya kasha na kuviweka karibu na mwanga wa taa, mara tu wataanza kula na kunywa maji. Kama kuna baadhi ya vifaranga wanaonekana kuwa wadhaifu ingiza midomo yao polepole kwenye maji mara mbili au tatu, nao wataanza kula na kunywa maji kama wengine. Funga mlango polepole kwani kelele zitawafadhaisha vifaranga, rudi bandani kuangalia wanavyoendelea mara kadhaa ili kuhakikisha kwamba hakuna walio dhaifu. Jaza vyombo vya chakula kila mara. Chakula kinapopungua na maji safi yawekwe kila siku kwa kumwaga yaliyopo na kuosha vizuri vyombo vya maji. Maji yanayojazwa yasiwe baridi sana. Chunga vifaranga kuona kama hawali, kunywa au kukimbiakimbia, kuna kasoro. Aidha kuna upepo na pengine hali ni ya joto mno au baridi sana. Baada ya siku chache pandisha taa juu kidogo, na endelea kufanya hivyo kwa muda wa siku chache. Baada ya wiki moja acha mlango wazi wakati wa joto lakini ziba mlango kwa waya ili kuzuia wanyama na watoto. Madirisha yafunguliwe wakati wote isipokuwa usiku na panapokuwa na baridi. Siku ya 7 vifaranga wapewe chanjo ya Newcastle (mdondo) na irudiwe kila baada ya miezi mitatu Baada ya siku 10 taa inaweza kuzimwa wakati wa mchana na kuwashwa wakati wa usiku tu. Hakikisha kuwa hakuna panya ambao licha ya kula chakula pia wanaweza kula vifaranga. Baada ya wiki 3 vifaranga wana nguvu za kutosha na hawahitaji tena joto la taa. Vifaranga sasa wanaweza kuhamishwa chumba kikubwa. Baada ya kuhamishia vifaranga katika sehemu mpya, sehemu ya kulelea isafi shwe kwa kuondoa takataka na kuzichoma moto. Pia vyombo vya chakula na maji kwa kusuuzwa kwa dawa (disinfenctant) tayari kwa matumizi ya mkupuo mwingine wa vifaranga wachanga. Sehemu (chumba) ya kulelea vifaranga inapaswa kuachwa kwa muda usiopungua wiki 3 kabla ya kupokea vifaranga wengine. Katika muda huo chumba kisafi shwe, kisuguliwe na kuwekwa dawa mara mbili au tatu. JINSI YA KUTAYARISHA SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI Vifaranga wachanga (umri wa siku moja) tofauti na wanyama wengine wafugwao hawawezi kuishi bila kuwepo uhakika wa joto la kutosha. Kuna njia nyingi za kulea vifaranga wachanga, lakini njia sahihi kwa wakulima wa vijijini pasipokuwa na umeme au mafuta ya taa ni kutumia kasha lililotengenezwa kutumia majani makavu, kama ifuatavyo: Katika banda au chumba kilichosafi shwa vizuri na sakafu kufunikwa majani makavu tengeneza duara yenye upana wa futi 3 kwa kutumia fito zenye urefu wa nchi 9 halafu zungushia wavu wa mbu na kuacha upana wa nchi 9. Ziba waya wa mbu kwa majani makavu na kuacha wazi mlango. Tengeneza paa la msonge kwa kutumia majani makavu ambalo litafunika vizuri duara lililojengwa tayari. Wakati wa mchana paa la msonge laweza kuondolewa kwenye duara ili vifaranga wapate mwanga na uhuru wa kukimbiakimbia. Wakati wa usiku paa la msonge sharti lirudishwe juu ya duara na mlango ufungwe kwa tofali au jiwe ili kuhifadhi joto kwa ajili ya vifaranga. Vifaranga wakishapata nguvu ihakikishwe kwamba vifaranga wanapata chakula na maji safi ya kutosha.
    #mkulimasmart
    #shambadarasa

ความคิดเห็น • 35

  • @ShaameIshaka-pf8lx
    @ShaameIshaka-pf8lx ปีที่แล้ว +1

    Asanteni watalamu wakilimo Na mifugo

  • @duahmbone-9557
    @duahmbone-9557 ปีที่แล้ว +1

    Nalikubali dalasa lako sana

  • @MKULIMASMART
    @MKULIMASMART 3 ปีที่แล้ว

    Iko poa sana

  • @ShakilaBakari-t9h
    @ShakilaBakari-t9h 3 หลายเดือนก่อน

    Ukiwaanzishia pillet ya silver land inafaa vifaranga wa siku 1

  • @apostlepauljoshua8687
    @apostlepauljoshua8687 3 ปีที่แล้ว +1

    Mpo dodoma sehemu gani

    • @shambadarasaTV
      @shambadarasaTV  3 ปีที่แล้ว

      tuko nzuguni karibu na stendi ya mkoa

  • @catherinesawewe9674
    @catherinesawewe9674 3 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana kaka ira mkaa mbona bado mweusi yani moshi.

    • @shambadarasaTV
      @shambadarasaTV  3 ปีที่แล้ว

      KARIBU

    • @bethmgombela3918
      @bethmgombela3918 2 ปีที่แล้ว +1

      @@shambadarasaTV vifaranga wa saso nikiwapa starter mfuko mmoja nikaendelea kuwapa grower itakuwa vibaya?

    • @bethmgombela3918
      @bethmgombela3918 2 ปีที่แล้ว

      Vifaranga 200

    • @shambadarasaTV
      @shambadarasaTV  2 ปีที่แล้ว

      @@bethmgombela3918 WAKO WANGAPI?

    • @bethmgombela3918
      @bethmgombela3918 2 ปีที่แล้ว

      @@shambadarasaTV wako 200

  • @ShakilaBakari-t9h
    @ShakilaBakari-t9h 3 หลายเดือนก่อน

    Wanamaliza kl 50 ya chakula

  • @devisgodson5270
    @devisgodson5270 ปีที่แล้ว

    Duuh hiyo faida sio
    Kwani cost hapo ni chakula tuu hao kuku unapewa bure

  • @ShakilaBakari-t9h
    @ShakilaBakari-t9h 3 หลายเดือนก่อน

    Samahan wangu walikua 100 mbn wanamaliza wiki au siku 5 ama nawazidishia!

  • @dekanyaktown.255
    @dekanyaktown.255 2 ปีที่แล้ว +1

    Nataka nianze kufuga kuku naomba kuuliza kunaaina ngapi za chanjo na unawapatia kila baada ya mda gani.

  • @hellenmbedule6963
    @hellenmbedule6963 3 ปีที่แล้ว +1

    Na icho chakula in shi ngapi

  • @MagrethKalindo
    @MagrethKalindo 7 หลายเดือนก่อน

    Nilikuwa natak kujua yaaaan mfano xaxa ndo unatak kuandaa pesa kwaajil ya kununua ivo vifaranga je Ina gharimu kias gan, naomba nixaidie kwa hilo

  • @jacklinejjmtkmtaki-rn6xc
    @jacklinejjmtkmtaki-rn6xc ปีที่แล้ว +1

    Sasa nitajuajevkama hayo malanda Yako salama hanana wadudu

  • @youngboss7535
    @youngboss7535 2 ปีที่แล้ว +1

    Hiyo elfu 69 ni kwa mfuko mmoja au yote miwili itakayotumik kwa wiki mbili?

  • @honoratussalvatort8700
    @honoratussalvatort8700 3 ปีที่แล้ว

    iko poa sana

  • @shambadarasaTV
    @shambadarasaTV  3 ปีที่แล้ว +1

    KARIBU SANA

  • @hellenmbedule6963
    @hellenmbedule6963 3 ปีที่แล้ว +1

    Chumba kinatakiwa kiwe na ukubwa gani kuweka hao kuku

  • @beatricenelson395
    @beatricenelson395 3 ปีที่แล้ว

    Mbona mkaa wako haujawaka vizuri na mkaa una kabon ambayo ni sumu kwa kuku?

    • @shambadarasaTV
      @shambadarasaTV  3 ปีที่แล้ว

      kweli dada.Hilo jambo muhimu.Madilisha yalikuwa wazi ili hewa chafu itoke

  • @LucyRamson-h5n
    @LucyRamson-h5n ปีที่แล้ว

    Unapatkana wap

  • @catherinesawewe9674
    @catherinesawewe9674 3 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana kaka ira mkaa mbona bado mweusi yani moshi.