WAZIRI SILAA AINGILIA KATI SAKATA MGOGORO WA GREENHOOD BAGAMOYO | AWATAKA WANANCHI WASIZUE TAHARUKI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 5 ก.ค. 2024
  • Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi na mwekezaji toka mwaka 2004 wa shamba Na.2126 & 2127 linalomilikiwa na kampuni ya GREENWOOD FARM LTD lililopo katika kijiji cha Makurunge wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ambapo kampuni hiyo ilimilikishwa mashamba hayo toka mwaka 2004.
    Waziri Silaa baada ya kupitia nyaraka pamoja na kuwasikiliza wananchi hao amewataka wasizue taharuki katika eneo hilo wasubirie maelekezo ya serikali kwani wao ni wavamizi na eneo hilo ni milki halali ya kampuni ya GreenWood.
    Aidha Waziri Silaa amesema mashamba hayo yalimilikishwa kwa Kampuni hiyo kulitokea baadhi ya wananchi waliopinga umilikishaji huo kwa madai kuwa hawakilipwa fidia lakini sehemu nyingine za mashamba hayo haya kuwa na madai yoyote.
    Pamoja nahilo wananchi wengine waliendelea kuvamia nakujimegea ardhi ndani ya mashamba hayo. Inakadiriwa kuwa ndani ya mashamba kuna wavamizi zaidi ya 800.
    Halmashauri ilianzisha utaratibu wa kufuta umiliki wa Mashamba hayo ambapo mwaka 2022 mapendekezo ya ufutaji wa milki ya mashamba hayo uliwasilishwa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Pwani kwaajili ya hatua zake muhimu.
  • บันเทิง

ความคิดเห็น • 2

  • @lovenessvisent9408
    @lovenessvisent9408 14 วันที่ผ่านมา +2

    Mimi ndio kwanza najitafuta Sasa naona ni muhimu kuwa na mwanasheria wangu sasa

  • @salmanmagwe2612
    @salmanmagwe2612 14 วันที่ผ่านมา +1

    Hii tabia ya kuvamia maeneo ya watu imeshamiri mno Tz,na sio eti kuna matatizo ya ardhi kwani wengi wao wametoka mikoani wameacha maeneo yao makubwa tu na kuja kubanana mijini na kusingizia hakuna maeneo.
    Na pia wa Tz tunapenda mno vya bure,na kutokujali sheria.