Maandamano kuelekea Kanisa la Karatu Mjini kwa Ibada ya ufunguzi wa Juma la Pentekoste.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 พ.ค. 2024
  • Leo Jumamosi tarehe 11/5/2024 katika Usharika wa Karatu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Jimbo la Karatu, imefanyika Ibada ya uzinduzi wa Juma la Pentekoste ambalo Kidayosisi linafanyikia Jimbo la Karatu kuanzia tarehe 11 - 19/5/2024. Ibada ya uzinduzi imeongozwa na Msaidizi wa Askofu Mhe. Mch. Deogratius Msanya akishirikiana na Wakuu wa Majimbo ya Karatu {Mch. Barikiel Panga}, Siha {Mch. Elisa Kileo} na Hai {Mch. Biniel Mallyo}. Wengine ni Katibu wa Idara ya Elimu ya Kikristo {Mch. Fadhili J. Kiwera}, Wasaidizi wa Wakuu wa Majimbo ya Karatu {Mch. Phanuel Sippu} na Hai {Mch. Dominic Mushi}.
    Juma la Pentekoste hufanyika kila mwaka katika Juma la kuanzia Rogathe {Ombeni} na kuishia Juma la Pentekoste {Kushuka kwa Roho Mtakatifu} katika kalenda ya Kanisa.
    Kupitia Juma hili, Wahubiri Zaidi ya 164 {Wachungaji 42, Wainjilisti 42, Wahubiri huru 80} watahubiri na kufundisha katika semina na mikutano ya Injili kwenye sharika 15 za Jimbo zenye mitaa 82. Wahubiri hawa wanaambatana pia na Wapuliza tarumbeta 80 ambao Watahubiri kwa njia ya Tarumbeta sharika zote 15.
    Baada ya kutangaza ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Dayosisi, Mhe. Msaidizi Askofu Mch. Deogratius Msanya alitoa neon la utume na kuwatuma Wahubiri kutawanyika katika vituo 82 vilivyopnagwa kwa ajili ya Juma la Pentekoste.
    Juma la Pentekoste linatarajiwa kufungwa Jumapili ya Pentekoste tarehe 19/05/2024 na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mhe. Baba Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo.

ความคิดเห็น •