Jengo jipya la abiria MWANZA AIRPORT liko kitaalam sana- Mongella

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 27 ต.ค. 2019
  • Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo litakalogharimu Bilioni 12 hadi kukamilika Aprili, 2020.
    Ujenzi huo katika hatua ya awali ya msingi umefikia asilimia 60 ambapo kazi inafanyika usiku na mchana ili kufikia malengo ya kukamilika ndani ya miezi sita badala ya miezi 12 kama ilivyopangwa hapo awali.
    Hatua ya ujenzi wa jengo hilo jipya na la kisasa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 wakazi akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela zinachangia shilingi bilioni nne kwenye ujenzi huo.
    Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kupitia mfumo wa "Force Account".

ความคิดเห็น • 10

  • @gm7045
    @gm7045 4 ปีที่แล้ว +1

    Everything looking good 👌Can pls try to remove the stagnant water can damage the wall

  • @amanichomola6696
    @amanichomola6696 4 ปีที่แล้ว +1

    Safi Bmg tunafarahi sana kupata taarifa kamahizi

    • @BMGOnlineTV
      @BMGOnlineTV  4 ปีที่แล้ว +1

      Tunashukuru kwa mrejesho....Share

    • @lameckseko979
      @lameckseko979 4 ปีที่แล้ว

      @@BMGOnlineTV hao wataalamu wanasemaje kuhusu idadi ya wasafiri wanaoweza kuhudumiwa kwa mwaka. Kwasababu moja vigezo vinavyotumika kujaji ukubwa wa uwanja ni idadi ya wasafari wanaoweza kuhudumiwa kwa mwaka.

    • @BMGOnlineTV
      @BMGOnlineTV  4 ปีที่แล้ว +1

      @@lameckseko979 Tutakuletea majawabu hapa hapa

  • @mahembotandula4232
    @mahembotandula4232 4 ปีที่แล้ว

    Mwanza kumenoga Hongera JPM.

    • @BMGOnlineTV
      @BMGOnlineTV  4 ปีที่แล้ว

      Hakika

    • @jamesmshanga1098
      @jamesmshanga1098 4 ปีที่แล้ว

      Nawapongeza kwa ujenzi ila ondoeni maji kwenye foundation nunueni vifaa vya kaz

  • @lamecktheonest225
    @lamecktheonest225 4 ปีที่แล้ว

    Ebana wee kweli Tz inapaa, kama masiala vile kumbe ndo tunasonga

  • @michaelnestory2530
    @michaelnestory2530 4 ปีที่แล้ว

    Chuga hampakumbukag