MTEGO wa POLISI WAWADAKA WEZI wa VIFAA DARAJA la JPM MWANZA, KAMANDA AZUNGUMZA...

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 9 ธ.ค. 2022
  • MTEGO wa POLISI WAWADAKA WEZI wa VIFAA DARAJA la JPM MWANZA, KAMANDA AZUNGUMZA...
    DESEMBA 9, 2022 muda wa saa 13:47 mchana wilayani Sengerema, Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Wilbroad Mutafungwa alitoa taarifa ya kukamatwa kwa vifaa vya ujenzi vilivyoibwa katika mradi wa daraja la Hayati Dk John Pombe Magufuli (JPM) la Kigongo-Busisi.
    Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Mutafungwa alisema, mnamo Desemba 8, 2022 muda wa saa 07:30 asubuhi, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa kampuni ya ujenzi wa daraja hilo ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kuwa kuna wizi wa vifaa vya ujenzi wa daraja la JPM la Kigongo-Busisi.
    Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji wa haraka na upelelezi wa kina kupitia taarifa za kiintelijensia walifika katika Kitongoji cha Busisi Madukani kwenye nyumba inayomilikiwa na Makona Samwel.
    Kupitia upelelezi huo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kupata vitu mbalimbali vikiwa vimefichwa ndani ya nyumba hiyo.
    Baada ya upekuzi, kwenye chumba cha Halfani ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya CCECC kama fundi nondo (steel fixture) vilikutwa vifaa vyote vilivyoibwa katika mradi wa kimkakati wa daraja la JPM.
    Vitu hivyo, ni pamoja na mashine saba za kuchomelea, stick za kuchomelea vyuma aina ya THJ 422 box 30, welding cable na drilling bit mbili ambapo bado kufahamika thamani yake.
    Imeandaliwa na Johnson James- GPL
    ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/globalradio/
    ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
    ⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
    ⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx
    ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: • GLOBAL COMEDY/MOVIES
    ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
    ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 657 693 210), ( +255 713 750910)
    ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
    ⚫️ OUR PLAYLISTS:
    ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
    ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
    ⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globalradio
    ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusive_interviews
    ⚫️ Subscribe Global TV bit.ly/globaltvonline

ความคิดเห็น • 32

  • @globaltv_online
    @globaltv_online  ปีที่แล้ว +1

    SUBSCRIBE NOW NA BONYEZA ALAMA YA KENGELE🔔 UWE WA KWANZA KUONA👉 bit.ly/3MraYdQ

  • @machachehardware5975
    @machachehardware5975 ปีที่แล้ว +1

    Nashukuru jeshi la polisi kwa kazi nzuri

  • @yohanakananika3586
    @yohanakananika3586 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana jeshi la polisi , safi sana mchina

  • @azizamohamed7692
    @azizamohamed7692 ปีที่แล้ว +2

    Mchina umetishaa kwa kuongea kiswahili

  • @stellanyamuhogota1832
    @stellanyamuhogota1832 ปีที่แล้ว +1

    Mchinaaa😀😀👍

  • @omarymohamed168
    @omarymohamed168 ปีที่แล้ว +2

    Ety gari yenyewe imekaa tuu. Hata haijuw kama imekamatwa na polisi

  • @msafirimiracle6613
    @msafirimiracle6613 ปีที่แล้ว +1

    Nawaza kabla ya mtego,dah!wahuni waliishabeba vyao.

  • @ashirafukitololi540
    @ashirafukitololi540 ปีที่แล้ว +1

    Yan Bongo njaa zingine bwana sometime ss ndo nini ukiiba ivyo vifaa vinakupeleka wap?

  • @jamessichimata36
    @jamessichimata36 ปีที่แล้ว +1

    Wabongo bwana

  • @barakarobert1029
    @barakarobert1029 ปีที่แล้ว

    Asante sna kamanda

  • @rahimaaaaa8699
    @rahimaaaaa8699 ปีที่แล้ว +1

    Mchina anawazidi hata wtz wengine

  • @hallin9561
    @hallin9561 ปีที่แล้ว +1

    jaman izo mali tugawane wote, waziri anasaini daraja billion 10, yeye analijenga kwa billion 4 apo ameshaiba billion 6, bado mafundi nao wanaiba cement na nondo, sasa nasis wananchi tule wapi. kama kuiibia nchi tuiibie wote kwa pamoja

  • @charlesmugisha6529
    @charlesmugisha6529 ปีที่แล้ว

    Si wafunge camera kila sehemu?

  • @lilianwambui1035
    @lilianwambui1035 ปีที่แล้ว +1

    🏃🏃

  • @bajagihaji8923
    @bajagihaji8923 ปีที่แล้ว +1

    Tunataka maendeleo lakini baadhi yetu wizi kwenye damu tutafika kweli wapewe adhabu kali

  • @anithawidambe7543
    @anithawidambe7543 ปีที่แล้ว

    KAZI NZURI SANA MAASKARI WETU.HAO WAFUNGWE ILI LIWE FUNDISHO KWA WENGINE.

  • @jeremiahsanare8754
    @jeremiahsanare8754 ปีที่แล้ว

    Daah mchina kachoma

  • @hassanabdillah3325
    @hassanabdillah3325 ปีที่แล้ว

    Ikisibitika wameiba wafungwe miaka mia wanatuibia mali zetu wananchi kodi zetu hizo hao walioiba hawana utu

  • @welcometoeat165
    @welcometoeat165 ปีที่แล้ว

    Yani haibu sana kwakwel

  • @zobakazizi7637
    @zobakazizi7637 ปีที่แล้ว

    Hawa ndio wanaoshelewesha miradi halafu tunaanza kumlalamikia Rais. Hivi watanzania tukoje?

  • @ameedamilja7992
    @ameedamilja7992 ปีที่แล้ว

    Polisi wangeweka kituo cha muda kwenye daraja linalojengwa tena vituo viwekwe pande zote 2 za daraja mpaka kazi itakapomalizika kituo kimoja kibaki hata kama ni kidogo.

  • @babuloliondo74
    @babuloliondo74 ปีที่แล้ว

    Mchina oyeeeeee au kadikiwa aaaa apana ajandikiwa aaaaa siokweri aaaaaaaiiiiiiiiiiiiiii aaaaaa mchina oyeeeeeeeeeeeeede

  • @abdirizakibrahim1975
    @abdirizakibrahim1975 ปีที่แล้ว

    Uzalendo ni muhimu

    • @hallin9561
      @hallin9561 ปีที่แล้ว

      uzarendo ungeanzia kwa hao mawaziri wezi wanaosaini mabilion ya ujenzi alaf wanagawana nusu

  • @kabwelasutiviraka4765
    @kabwelasutiviraka4765 ปีที่แล้ว

    Kwa nini JKT au jeshi wasilinde hapo mbona serikali hamko makini , ni mradi mkubwa mnawapa walinzi wasioeleweka

    • @avitusmichael5
      @avitusmichael5 ปีที่แล้ว

      Wao ndo hawataki hela? Kwanza pale kuna walinzi wa Suma jkt

    • @kabwelasutiviraka4765
      @kabwelasutiviraka4765 ปีที่แล้ว

      @@avitusmichael5 mkuu umesikiliza vizuri au unakurupuka tu kujibu aliyeiba sio mlinzi wa suma jkt , na kama wanaona walinzi wengine hawafai Kwa nini wasiwape hiyo kazi jeshi

  • @bongo39
    @bongo39 ปีที่แล้ว

    Naombeni polisi hawa watu ni wanyama msiwaachilie kabisa na tunaomba muwaweke hadharani wote tuewajue na mahakama iwahukumu kama wahujumu wa uchumi wasionewe huruma hata kidogo halafu mnajiita wazawa wazalendo ndio uzalendo huu ili iwe mfano kwa wengine na sehemu zengine zote mpaka kwa wafanyakazi waserikali huko ndio kula njenje kama mali za mama zao hii ni kodo zetu lazma tuwe na uchungu

  • @allyhassan7522
    @allyhassan7522 ปีที่แล้ว

    Watu kama hawa si tuwanyo*ge tu!

  • @msetikebwasi7270
    @msetikebwasi7270 ปีที่แล้ว

    Hata wachina wanahusika sana ktk wizi,,wasijishaue hapo