REV. DR. ELIONA KIMARO: NIDHAMU NI HATIMA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 ก.ย. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY (FRIDAY PRAYERS) 16. 02. 2024.
    HII NI KWARESMA: SIKU YA 3
    UJUMBE WA LEO: "NIDHAMU NI HATIMA"
    "DISCIPLINE IS DESTINY"
    "ZITAFAKARINI NJIA ZENU"
    "CONSIDER YOUR WAYS"

    NENO KUU: HAGAI 1 : 7
    7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
    Luka 23 : 39 - 43
    39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.
    40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
    41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
    42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
    43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
    HOJA ZA MSINGI ZA KITHEOLOJIA & KIFALSAFA KUTOKANA NA WEZI WAWILI MSALABANI.
    LUKA 23:39-43
    1. Kabla ya toba ilitangulia NIDHAMU/ADABU.
    NIDHAMU ndiyo iliyomsukuma kutubu.
    (MWIZI MWENYE ADABU)
    2. NIDHAMU/ADABU Ni nguvu ya kuzitambua FURSA na kuzitumia ili kutengeneza HATIMA.
    (Reff. Ruthu Mmoabu Mama wa WAFALME wa Israel )
    3 . Lugha ya MAUDHI na kukosa ADABU hua inagharimu maisha ya watu wengi.
    (ADABU NI MAISHA NA MAISHA NI ADABU)
    Reff. Nabali Mumewe Abigail
    1SAMWELI 25
    4. Asiye na ADABU/ NIDHAMU habebeki, kama Yesu Alimshindwa mwizi na akamwacha msalabani wewe hutamweza.
    Reff. Mungu akushindwa kwenda na waisrael waliokosa ADABU Jangwani hata wakaponza na Musa.
    Kumb. 32:48 - 52
    MUNGU HAENDI NA MTU ASIYE NA NIDHAMU NA KUKOSA ADABU.
    5. Kwenye Maisha tutazidiana kwa kila kitu kulingana na kiwango cha
    NIDHAMU/ADABU tuliyonayo.
    NIDHAMU ITAAMUA UWE WAPI.
    Esta 8 : 15 - 17
    15 Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.
    16 Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.
    17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.
    6. NIDHAMU/ ADABU inakupa uhakika wa mahali unapokwenda.
    Yesu akamwambia yule mwizi pale Msalabani...
    Amin, Amin, Nakuambia leo hivi utakuwa pamoja nami PEPONI.
    UHAKIKA WA DESTINATIONS.
    7. Neema ipo kiasi cha Tele,
    Ila Neema inamfikia Maisha ya mtu kwa njia ya ADABU /NIDHAMU.
    Usiipungukie Neema ya Mungu kama Esau.
    Waebrania 12:14-17
    14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
    15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
    16 Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
    17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.
    PRAYER POINTS:
    1. TOBA
    2. JIOMBEE KUBADILISHWA TABIA YAKO.
    3. OMBEA MAISHA YAKO NA VUNJA NA KEMEA MISUKUMO YA UHARIBIFU KATIKA MAISHA YAKO.
    4. OMBEA MAMBO BINAFSI YA MAFUNGO YAKO YA KWARESMA.
    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

ความคิดเห็น • 5

  • @geraldotieno6010
    @geraldotieno6010 5 หลายเดือนก่อน +1

    Much love from Kenya powerful Oration... may the most high bless you

  • @user-bw7gw4zi3e
    @user-bw7gw4zi3e 6 หลายเดือนก่อน

    Bwana apewe sifa nilkua naomba haya mafundisho ya kwaersima yawe na sehem mfano party one na kuendelea ili tuweze kusikiliza vizuri Barikiwa sana!!!

  • @furahamtweve4222
    @furahamtweve4222 6 หลายเดือนก่อน +1

    Adabu
    Mungu nisaidie niwe na adabu

  • @naeema8155
    @naeema8155 6 หลายเดือนก่อน +1

    Mungu naomba niwe na nidhamu kwa kila mtu🙏