NAIBU ASEMA MAZITO IFIKAPO 2025 /WIZARA YA ELIMU YAONESHA HAYA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 17 ต.ค. 2024
  • Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba dhamira yake ya kuwawezesha Wanafunzi kuingia mkondo mmoja inatekelezeka ifikapo mwaka 2025.
    Mhe. Ghulam ameyasema hayo huko Skuli ya Furaha msingi katika hafla maalum ya kuwatunuku ZAWADI wanafunzi waliofaulu mitihani ya darasa la Saba na kidato Cha Tano ikiwa ni muendelezo wa utoaji wa ZAWADI ambazo hutoletwa na mwakilishi wa Jimbo la wawi .
    Amesema mpango huo wa serikali umelenga kuona wanafunzi na walimu wanapata muda mzuri wa kufundishia na kujifunza, hivyo serikali itahahakikisha inatatua changamoto zinazoikabili sekta katika maeneo mbali mbali.
    Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar amesema wataendelea kutekeleza ahadi walizozitoa katika kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi Ili kuikuza sekta ya elimu nchini.
    Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Moh`d Nassor Salim amesema uongozi wa skuli ya Skuli ya furaha umeweza kuleta mapinduzi ya kimaendelo hivyo kuwataka vitongoji kuendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya elimu .
    Mwalimu mkuu wa skuli ya furaha sekondari amesema kuwa Hadi sasa skuli ya sekondari Haina jengo hivyo kuiomba wizara kuwajengea skuli Ili kuongeza ufaulu katika skuli hio.
    Katika hafla hio ZAWADI mbali mbali zilitolewa ikiwemo mikoba sare sambamba na uongozi wa skuli ya msingi Kupatiwa computer pamoja na chakula Kwa wanafunzi wanaokaa DAHALIA

ความคิดเห็น • 1

  • @haroubmbarouk7858
    @haroubmbarouk7858 2 หลายเดือนก่อน

    Naibu waziri nasisi tuangalieni mutujengee skuli ya secondary katika kijiji cha sizini wilaya ya micheweni kaskazini Pemba vijana wetu wanasumbuka