WAZIRI MKUU MAJALIWA ATAMBA TANZANIA KUSHINDA AFCON NA KUISHANGAZA AFRIKA, ATAJA MBINU NA MKAKATI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 18 ก.ย. 2024
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maandalizi ya mashindano AFCON 2027 yanaendelea vizuri na kwamba Tanzania itafanya vizuri kutokana na maandalizi kabambe yanayoendelea lakini uwepo wa ligi bora kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
    Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Mei 30,2024 wakati akijibu swali la papo kwa hapo kutoka kwa Mbunge wa Makete Festo Sanga ambaye ametaka kujua Serikali inafanyaje kuhusu maandalizi ya mashindano hayo makubwa ambayo Tanzania kwa kushirikiana na majirani zake wamepewa uenyeji.
    Katika hatua nyingine amesema kwa sasa ligi imefika mwisho na tayari washindi wameshapatikana katika ligi ya Tanzania Bara na kule Zanzibar huku akisisitiza kuwa hata mshindi wa kombe la Muungano ameshapatikana.

ความคิดเห็น •