Mkuu wa kituo cha Polisi, wenzake sita kortini wakituhumiwa mauaji ya raia

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ก.ย. 2024
  • Askari Polisi wanne akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Kata ya Goziba, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, John Mweji na mgambo watatu wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumuua Baraka Lucas.
    Mwili wa Lucas (20) aliyekuwa mbeba dagaa wabichi Mwalo wa Kisiwa cha Goziba, ulipatikana ukielea Ziwa Victoria Juni 12, 2024 ikiwa ni siku nne kupita tangu adaiwe kukamatwa na polisi wa kituo hicho Juni 9, mwaka huu.
    Ndugu zake baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa ndugu yao na askari wa doria usiku wa manane, walikwenda kituoni bila kufanikiwa kumuona na baadaye Juni 12, 2024 ndipo mwili wake ulionekana kando ya Ziwa Victoria ukielea.
    Hii ni kesi ya pili kuhusisha maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya ile ya inayoendelea Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, ikiwahusisha maofisa saba walioshitakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis.

ความคิดเห็น • 6

  • @happyemanuel2070
    @happyemanuel2070 22 วันที่ผ่านมา

    Uwii Mungu wangu.😢😢

  • @teddymassawe3583
    @teddymassawe3583 หลายเดือนก่อน +1

    Mimi nikiwa nakimbizwa na mbaya nikikutana na askari naona ndiyo kupona kwangu kumbe yeye ndiye ananimaliza kabisa ,haya tutaponea wapi sasa

  • @HanifaOman-oo4pl
    @HanifaOman-oo4pl หลายเดือนก่อน

    Subuhanallah.

  • @uwezawamungumkuu.amaniafrika
    @uwezawamungumkuu.amaniafrika หลายเดือนก่อน +1

    Tumwamini nani sasa?.

  • @teddymassawe3583
    @teddymassawe3583 หลายเดือนก่อน

    Askari ndiyo tunawatemegea kuwa walinzi wetu,hao hao ndiyo wanatumaliza uwiiiiiiiii jamani Dunia hii inatufikisha wapi

  • @SalmaMuhammed-u8s
    @SalmaMuhammed-u8s หลายเดือนก่อน +1

    Awa mmbwa