Dizasta Vina - Utaliimba Jina Langu Ft G Nako
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 6 ก.พ. 2025
- Official Video for Tanzanian Hip Hop Artist, Songwriter, and Record Producer Dizasta Vina, Performing a record 'Utaliimba Jina Langu' Off the Album 'A father Figure'
Written by Dizasta Vina
Music by Ringle Beatz, J'cob
Drums by Double
Vocals by Dizasta Vina, G Nako, Double
Mixed and mastered by J'cob & Double
Download/Stream Utaliimba jina langu now
TH-cam - • Dizasta Vina - Utaliim...
Mdundo - mdundo.com/son...
Apple music - / utaliimba-jina-langu-f...
Audiomack - audiomack.com/...
DISCLAIMER: Images used in this work were for educational purposes, no harm ever intended
Lyrics
VERSE I
Sitauona uzuri wa mataa
Maua na uturi au usafi wa suti nitayoivaa
Mtajadili kama nilifunzwa chuki na hii njaa
Au msamaha niliomba baada ya kuivunja mioyo kadhaa
Mikono yangu haitaishika sayari
historia nitakuwa nimeimaliza tayari
Naenda upande wa pili, asili itanipiga kabali
Nitakuwa nimeimaliza safari
Maombi hayatakidhi nisimame soja
Nanyi mtaijua hadithi hii ya upande mmoja
Pesa na ustaa hautanibeba
Itaandikwa "mwisho wa kila shujaa ni jeneza"
Siwezi kimbia udhuru hata nikibadili njia
Nakuwa huru dhidi ya kufuru za hii dunia
Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa ama mtaliimba jina langu?
Siku hii iwakumbushe kuwa kesho mbali
Iwakumbushe havina maana pesa mjengo mkali
Vyeo urembo na pesa nyingi
Ni kiburi cha hii pumzi, pumzi ambayo ni temporary
Sijui Nitamwachia nani mama yangu
Ikiwa, nitaacha dini, itikadi ya chama changu
Cheo changu hakitakuwa na maana tena
Nitalala gizani japo mtajua nimelala pema
CHORUS
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
na kweli
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
VERSE II
Nitalala sitahisia karaha zako
Sitasikia matusi sitasikia msamaha wako
Sitasikia kicheko au kilio cha unafiki
Ubongo hautatafsiri mawimbi ya sauti yako
Nini maana ya chuki yako kwangu ikiwa
Siwezi amka hayafungukia macho yangu
Nitakuwa mbali peke yangu futi sita
Hata kivuli hakiwezi kuwepo kando yangu
Ufedhuli ni kibari cha hii nguvu
Ya nyama na mifupa ambayo ni mali ya wadudu
Ipo siku utaimbiwa pambio na wadau
Kisha Ndugu watagawana salio na kusahau
So, nataka nikifa msinidai
Msilie msherehekee niliyoyafanya nikiwa hai
I wonder kama mwangaza usipotimba himaya yangu
Je utafurahi nikifa ama utaliimba jina langu?
Minara yangu imara itadondoka nayo
Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo
Masikini roho yangu mimi
Itaenda wapi pindi mwili utakapogusa
Udongo mkavu chini
Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa, ama mtaliimba jina langu?
BRIDGE
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi...
CHORUS
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
na kweli
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(Dunia inashindwa kunilinda)
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(ni dhaifu na kweli)
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
Dah!! Kuna muda inabidi sisi tuliofanikiwa kuzaliwa kizazi kimoja na THE GREAT THINKER DIZASTA VINA tujivunie na tujipige kifuani hiki kichwa sijui kama kitakuja kupatikana tena Tanzania miaka ya hivi karibuni 🔥🔥🔥
TRUE
Ngumu sana kupatikana kama huyu kama ngwea tu akuna aliye patikana kama huyo jamaa huyu ndo akuna atakaye jaribu ata kuwa hivi
Nimenunua album ilipotoka tu, ila leo nilivyoiona hii lyrics video naiona ni kama mpya na idea yangu imeenda mbali zaidi.
True
True
Dah Nina bahati sana kuipenda HIP HOP huu mziki ni ibada jamani
Ambao tuliinunua hiii nyimbo toka mwaka jana na tumeishika tujuane kwa like ❤
Nanunuaje nyimbo zake Master dizasta
toka mwaka jana mpaka mwaka huu kuna wapo walionunua hii nyimbo na saivi wapo pekeyao ndani futi sita 💔💔JE TUNATAKMBA MAJINA YAO
Nasubiria Mwanasesere
Nmesoma comment zote,,kama sisi ni suppoters wa mziki mzuri toka kwa dizasta vinaa, why ngoma ipo nafasi ya 25 on trending 🕊️🕊️🕊️🕊️🕊️ok twende p1 tupeleke maua yke ngoma ifke No 1 trending
NAKUBALI BOY WANGU
Tulionunua ulbum tuliyapat madini haya tangu mwaka mmoja uliopita. Support kwa HIP HOP .. nunueni ulbum bado kuna vitu mnachelewa kuvipata
Kweli kabisa albamu ndo habari ya mjini
@@yusuphisack285 Sure..ile ni zaidi ya Album Kaka
Naamu kule kuna madini ya kutosha
Maisha ya ukweli salute # ukweli salu T
Ilikuwa ina nikataa sana we umenunua alafu kuna jamaa anakuambia nitumie unatuma namba za dizast
Kama umetambua zaidi ya 90% ya sura zilizoonyeshwa basi you are most likely from the 90s and earlier.
Na hii inamaanisha ushakuwa mtu mzima sasa na huu ndio muda sahihi wa kuhakikisha unaacha kumbukumbu nzuri kabla ya muda kukutupa mkono.
Watambue watu muhimu maishani mwako na hakikisha wanajua kuwa unawapenda na kuwajali.
Sijawahi kumsikiliza vya kutosha @DizastaVina lakini damn! This song just tore my heart to pieces.
Binafsi nimepoteza watu wengi muhimu maishani mwangu over the last few years but i guess kuendelea kupambana kuwa the best version of myself na kuwakumbuka waliotangulia ndio njia sahihi.
R.I.P Philipo Tobias, mdogo wangu, alifariki 22.12.2024,
pole kaka
@@jamesedward1044 . amen🙏
IFIKE STAGE VINA APEWE HESHIMA ANAYOSTAHILI. GOAT!
Ulishawahi kununua album yake hata moja?
@Nickbrown127 FATHER FIGURE
...yes huwaa wanaongea tu wakat hata hajawah kuwa na album ya mchizi
Tutamtengenezea tunzo mashabiki
NO. 1 - VINA
Muda wa kuona Ukubwa wake katika hii tasnia.
Album Imeshiba sana hii📌
Kweli kaka, time ifike media za bongo zimpe airtime ya kutosha
Maana halisi ya HIP HOP ni hii kupeleka ujumbe kwa njia ya fasihi. Fanani (Dizasta) 💯
1:30 Huyu Mwamba ameandika sana Kwenye Hii Ngoma!
Vyote tulivyonavyo hapa Duniani ni vyakupita tu. Tuwe Wanyenyekevu sana na haya Maisha.
Jamaa anaandika sana sio hapa tu
I'm here to speak with you 2050s generation today it's 8 Jan 2025 THIS DUDE WAS BADDEST & MUCH CREATOR in our 90s generation PLEASE MUST RESPECT HIM
Wadau tunaoziona jitihada za story teller tujitahidi kupush kazi za vina tujaribu kuzindua jamii
Hii ngoma najikuta najililia mwenye
R i p brother wangu kipenzi tizo ipo siku tutaonana😭😭😭😭
Pole sana
Sijutii kununua album ya huyu mwamba. The best hip hop kwa Tz kwa sasa.
Daah Dizasta ni mmoja tu sasa hapo watoto wa iringa mmekutana G NAKO kauwasha moto
Watoto w iringa kivipi kaka sijaelewa
@@AmmielNzala-fu4xuhata mm cjamuerewa
Kwhy G nako n wa iringa 😂😂😂, sorry lkn km nmekuelewa vibaya
Hii ya moto sana kaka 🔥🔥🔥🔥🔥
@@emanuelsamkinda2893 kiasili sema kazaliwa na kukulia chuga
Sina cha kusema aisee… kuna wasanii….. hakuna msanii kama huyu Tz nzima, swala sio kuimba, swala ni Tungo. “🫡🫡🫡🫡🫡
G NAKO CHORUS YAKO IPO SO EMOTIONAL ALAFU JINSI VINA ANAVYOFLOW UNAJIFEEL UPO DUNIA NYENGINE SPIRITUAL YOU GUYS ARE MY MENTORS TOO
Aisee unakuta UMETULIA ADI UNAOGOPA lakin ndio song 😂
YE, NAS, TRAVIS SCOT, KENDRICK LAMAR, J COLE hawa watu wanauandishi mzuri na wanafikilia sana TZ tujivunie kuwa na DIZASTA VINNA jamani 🎉🎉🎉🎉
Ila sio same flow kama vina wetu vina mkali ila awezi change Kama awo uliowataja
Nyimbo zako zimekuwazikinijenga sana kwamafunzo, hii nayo funzo tosha wakati tupo hai tuishi kwakuandaa mwisho wetu mwema tusiishi kwakujisahau dunia ni mapito na kila nafsi itaonja umauti, Asante sana D.vina kwakutukumbusha ilo ubarikiwe sana ❤
😢 Dunia inashidwa kunilinda.
"Masikini roho yangu mimi, itaenda wapi pindi mwili utakapogusa udongo mkavu chini"💔
Dizastaa
Ni kweli Kila mtu ana rapa wake Bora kulingana na vigezo vyake kwanguuu Mimi dizasta vina ni kinara wao
Dhida ni mojaa tu mwamba anakaziwa sana ilaa poaa tuu one day yes you will be up than them master thinker but now no 1 to 9 best rapper is dizasta only anaweza akaapiga kibao kikali mpaka FID Q Nkamuona SAJNA tu
Ni time taasisi za elimu ya juu kumualika vinna kutoa elimu ya fasihi kwa wanafunzi wa elimu ya juu…. His lyrical will live forever …. Ni muziki wa guidance kwa kutuweka katika kutunza misingi….. whenever I wanna meditate alone I just put dizasta vina songs on backgrounds …. Pure culture ✍🏿
Ifike muda sasa dizasta vina atoe hata riwaya ili kizazi kichacho kikuje kufaidi vyote viwili yani kitabu na hizi ngoma zake
MUCH RESPECT
Au maktaba za serikal zihifadh kumbukumbu za kazi za huyu jamaa ili kuja kuwapa madini kizazi kinachokuja
Uwezo mkubwa wa kufikiri peni haiwezi kugoma kwenye karatasi, hii nimeikubali sana always salute to "VINA"
Inapoweza Kuibua husia FULANI ndani yako ,Hiyo ndiyo sanaa .."THIS IS ART"
tujuane basi wanangu wa ngumu kumeza kama hizi zenye ujumbe mzuri ndani❤❤❤❤❤
Rapper Bora halindwi mungu ametupa mchizi kama darasa la kujifunza mengi mda mwingine ni kama dini tuu
hakika
Itaandikwa mwisho wa kila shujaa ni jeneza, nipo hapa tena, nilifaidi sana hii ngoma baada ya kununua album January 9th 2024 pamoja na conf of mad father, mwanasesere na ile last confession, ilikuw hunielez kitu kuhus hiz ngoma.
(sad😢) nimewakumbuka ndugu zangu......!
Ukiona comment hii we like ili inirudishe kuisikiliza tena hii ngoma ya mtaalam Dizasta vina
kaka rudi
Video 100%
Lyrics 100%
Audio 100%
Beat 100%
Idea
100%
DIZASTA vina 100%. Moja ya zawadi kubwa kwa kizazi hiki ni kumshuhudia DIZASTA VINA
Really interested music
Real
Ila g nako popote kambi🙌
Genius Dizasta vina umetukumbusha Jambo la muhimu sana kifo,,, Mwenyezimungu atujaalie mwisho mwema🙏
Ameen
Tuko nonde apa kilimani tuna choma uchafu kusafisha akili respect tkoea mbeya .... One love fam
Underground Hip Hop ndiyo ujumbe halisi wa Jamii ulipo Dizasta Vina+G nako mmewakilisha vyema ile maana halisi ya Msanii kioo cha Jamii
13hrs with more than 18k views, big up dizasta...i know the hustle, seeing you making these heights am humbled....shawn midundo apa nina mizigo yako apa kaka
Dizasta has reminded us to know that we are all about to depart this world
UWEZO MKUBWA WA KUFIKIRI 👏
G nako iyo chorus kauwa aise du!
Storyteller mmoja tu DIZASTA VINA
MTALIIMBA JINA LANGU 💪
Take 👊 vina
Hio chorus nlimpaa mwenyewe Wara Wara
Great Work
Thank you! Cheers!
0.39 R.I.P Sajuki
0.51 R.I.P Yusuph Manji
0.53 R.I.P J.K. Nyerere
1.02 R.I.P Godzillah
1.11 R.I.P Albert Mangwea
1.11 R.I.P Geez Mabovu
1.18 R.I.P Kanumba
1.23 R.I.P Amina Chifupa
1.36 R.I.P Agnes Masogange
1.44 R.I.P Augustino Mrema
1.45 R.I.P Benjamin Mkapa
1.52 R.I.P Salutaba (Salu Tee)
1.57 R.I.P Abeid Karume
2.03 R.I.P Vivian Tilia (Vivi)
2.03 R.I.P Saimon Sayi (Complex)
2.06 R.I.P Langa Kileo
2.17 R.I.P Loshilaa Motika (Mr Ebbo)
2.23 R.I.P Samuel Sitta
2.30 R.I.P Cpwaa
2.35 R.I.P Amina Ngaluma
2.43 R.I.P Mandojo
2.47 R.I.P King Majuto
3.01 R.I.P Asimwe
3.09 R.I.P Magufuli
3.14 R.I.P Lowassa
3.21 R.I.P Idi Amini Dada Oumee
3.26 R.I.P Regnald Mengi
3.42 R.I.P James Dandu
3.48 R.I.P Fatuma Binti Baraka (Bi Kidude)
3.56 R.I.P Nasma Khamis Kidogo
4.00 R.I.P Akwelina
4.05 R.I.P Banza Stone
4 16 R.I.P Nisher
4.39 R.I.P Bi Hindu
4.43 R.I.P Kingunge Ngombale Mwiru
4.52 R.I.P Hussein Jumbe
4.57 R.I.P Ephraim Kibonde
4.57 R.I.P Gadner G. Habash
5.02 R.I.P Mohamed Fungafunga (Jengua)
5.07 R.I.P Yusuph Kaimu (Pembe)
5.12 R.I.P Dida Shaibu
5.30 R.I.P Mwalimu Kashasha
5.36 R.I.P Hamza
5.41 R.I.P Ruge Mutahaba
5.46 R.I.P Sharo Milionea
5.55 R.I.P Malcom Masoud Kipanya
Kuna Aquelina, na nisher
Add
Amina Ngaruma
Bi Hindu
Pembe
C pwaa
@@dizastavinafanaccount Cpwaa yupo dakika ya ngapi??
@@allymbondo111 Nisher kaonekana dakika ya ngapi
@@dizastavinafanaccount cpwaa
Vina stay blessed always, nimeamka na kuomba tunaishi tunaishia 🙏🏾🙏🏾
Sasa huu ndio mziki!
Unasikiliza na akili, moyo, na roho.
Sidhani Kam kuna mtu ana mind Kama ya BOE VINA
Utatembea lini Kenya black Maradona tunakukubali sana huku. Consiuos music nearly Godly.
Utalala gizani, japo watasema umelala pema😢
😂❤❤❤
😢😢
Dizasta Vina ni Dizasta kweli,hili ni toleo la mwisho la viumbe wa aina yake.
Twendeni hii ngoma binafsi natamani itfike ata kwenye 10-9-8 trending lakini dah em tukaze wanangu tupite kila platform kuisapoti
Muda ndio huu wakuonyesha upendo kwa dizasta vina inakadiria vichwa miamoja kuja na hii idea @Dizasta ni highthinker
dizasta vina kaondoka nahisia zawengisana kupitia hii❣️🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Na comment ili dunia ikinimeza wajue hii ngoma kuna marehemu ali comment…..fire this song is
😂
😢
Dizasta Huwa Ana fikra Chanya Sana.....
This Guy is truly a Genius. Huu uwasilishaji uliojaa Vina lukuki na Moangilio wa Dhima ya kuliimba jina langu ni wa kipekee sana...Dizasta Vina ni kama mtaala tu kwa Sasa kwenye hichi kizazi cha Young rappers...Beat kali sanaa, Mixing🔥🔥🔥🔥...Animations zimetulia sana...Chorus kali sanaaa...Hip hop at its finest level and Dizasta is the Man of the Moment🔥🔥🔥
Man this is golden!
Ukinunuaa albam ya dizasta vina!! Hutojutia pesa yako... Vina katika kilele cha ubora!!
Album unanunuaje
@dismacking8421 ingia kwenye page za dizasta kuna namba ake unatuma hela anakuwekea kwenye email au kama unataka wasap
Ngoma ina fact nyingi, tz kuna wasanii wengi ila dizasta ni mmoja tu...✍️
Kama umemshuhudia Messi , Umemshuhudia Dizasta Vina , Umemshuhudia na lisu basi Umemshuhudia kila kitu
Tujitahidini kushare kila pande ngoma kali hii iwafikie wana hip hop na wasioelewa wajitambue
Dizasta Vina ulishasema we so malaika we ni Mungu wa rapu
Nidhaifu na kweli dunia inashindwa kunilinda,,
Ambacho hamjui hapa ni kwamba kila mtu anatokea kwenye mstari mahususi, hajawekwa tu
Wimbo wa Dunia vizazi na vizazi respect brother dizavina vs g Nako ❤❤❤❤❤🎉🎉🎉🎉🎉
Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo..!
Huu msitari umenifanya nijisikie vibaya sana😢..!
Mungu aendelee kukuweka kaka.!🙏
Dizasta Mavina
Oya huu ni mgodi ambao hauishiw na madin shabik namb 1 hapa wa dizasta vina
Hii ni mara ya 50 narudia ila bado xjaridhika kbisaaa maana inagusa uhalisia 😢😢😢 UPO KWA AJILI YA JAMII YETU 😢😢MUNGU NDIE ANAJUA UKUBWA WAKO🙏🙏
Hubembelezi warembo we sio marioo,
In loving memory of Malcom Masoud Kipanya 👏🏽
Kama Siku ya kwanza ya dunia ipo hata siku ya mwisho ipo pia....Dini ni njia 😢So fatilia dini yako mambo mangapi inakuficha DUNIA HAIWEZI KUWA MILELE DON'T 4GET FAMILIAR
If u get to be a dizasta fun ur blessed ...DIZASTA ON TOP
Dizasta wewe ni rappa namba 1+
Na ninavyo ona hakuna anae kukaribia maana namba 2, 3 4 na 5 zote zipo wazi, hazija mpata angalau anae kufanania.
Wao wameanza namba 6,7,8...
Na wana struggle kuwa kama wewe ila kalamu inawakataa maana mashairi yao sio stong kwenye masikio
🙌
Great of all time dizasta🇹🇿🇹🇿
Dah brother 😢😢 akika mungu kakujalia uwezo m najivunia saaan kuskiliza ukiimba napata elimu dunia napata hekima napata vingi saaan brother 😢😢 mungu tu akujalie miaka mingi 🎻
Kila nikifikiria fikra zangu najiuliza naweza fikiri kama D,kaka anajua sanaa sayansi yake yake ubungo ipo juu sana ❤
Aise atakae tazama hii video usilie tumu like dizasta vina kwanza ananitoa chozi la uchungu
huusio wimbo tu Bali ni mawaidha pia 🙏
From yesterday 1️⃣ step forward 13-10-09-
Seven days means one week tupo pale 13 na fresh
Dizasta
Disaster NI zaid ya module za chuo 🙌
Kama unaubongo mdogo WA kufikiria huwez muelewa nilazima atakuacha at the beginning 🙌
Watoto wadogo hawawezi kuelewa vinywa vinavyotema madini acha wendelee na wasanii wao 🙏🏾🙏🏾
"Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo" RIP Bi Kidude💔
R.S.P Dadaangu kipenz,, Najua Mbele yko nyuma yetu tutaja onana tena.
Dizasta ni mmoja tu, Rigo beat ni mmoja tu na G nako ni mmoja tu....
Ngoma imesimama hii. Kuanzia Beat, Vocal, Lyrics, Sound, chorus na verse zote.
Vyote vipo emotionally kama dhima ya ngoma.
Sema sauti ya Vina ni ya Gharama kweli kweli
Oyaaaaa mwamba anazingatia sana pen tuache unafiki tukae kwenye ukweli
Dizasta aeshimike sana, yy ndiye tafsiri ya kio cha jami, ❤ from Burundi 🇧🇮
Ishi sana mwamba sauti yako hakika yagharama sana.
Hii ngoma noma sana.
kimaana, Tungo ziko sambamba na picha za marehemu
Kila siku lazima niangalie kama jamaa ameachia jiwe hatimaye la kuanzia mwaka hili hapaa❤❤
Ma meeeeen DIZASTA
Dizasta vina ,bro unajua adibasi maana unatupa darasa kua hiii memory yandgu zetu walio tangulia mbele ya haki wote walikuepo nasi lakni atukuwaikupa sifa napongez zao kwayote waliyo fanya wakiwa hai tuasubiri wapotee kwenye usowaduni ndotuanze kusema ooh alkua bora ooh ailkuIv hapana ,for me thanks u bro unajua kutupa mashabiki zako what we need mmh coz umeimba maisha yakweli kwass tuliopo tujitafakari snaaa 🎶🇹🇿🙏 God bless you and long life to you Eendelea kutupa vitu vzrii
Safi
Toka Congo pokeya zangu respect 🤗
Mara ya kumi hii narudia kuusikiliza huu wimbo daah✊️🙌
Kwenye kazi zake dizasta amekua akitukumbusha tusisahau kuwa hapa Duniani we just passing through ✊
Npo kwenye taifa ambalo dizasta yupo❤❤❤❤❤❤
Daaah mwamba alex kashashaaa
Mungu akuweke mshikaji kuna vitu tunajifunza sana kwako
Huyu ni kama darasa ama din tunajifunza na kueleimika kupitia Talent aliyobarikiwa na mungu..... Eeh M/Mungu Ampe umri mrefu Dizasta kwa AJILI YA kuokoa kizazi chetu kupitia kipaji CHAKO kinatukumbusha kuhus hii TEMPORARY AIR TUNASHUKURU BRO WEWE NDIO UKUMBUSHO WA HIKI KIZAZI CHETU WE LOVE YOU❤❤
Hip hop for my life