SONGEA WANAVYOFURAHIA NDEGE ZA ATCL

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 ธ.ค. 2024
  • Wananchi mkoani Ruvuma wameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka ratiba ya safari za ndege za ATCL mara tatu kwa wiki.
    Abiria hao wametoa pongezi hizo wakati wanazungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye uwanja wa Ndege Songea.
    ATCL inatoa huduma za usafiri wa anga Kutoka Dar es salaam hadi Songea siku za Jumatatu,Jumatano na Ijumaa.
    Hata hivyo wananchi wameiomba serikali kuongeza safari kwa sababu hivi sasa abiria wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka na ndege imekuwa inajaa.
    Meneja wa Uwanja wa Ndege Songea Jordan Mchami amekiri abiria ni wengi ambapo ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila inapofika na kuondoka inabeba abiria zaidi ya 70 na kwamba wanatarajia kuanza safari za usiku.

ความคิดเห็น •