Mafunzo Tunayoyapata Kwa Kukamatwa Kwa P. Diddy

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 13 ม.ค. 2025
  • Na hii ndiyo hali iliyomkuta mheshimiwa Pii Didi. Kwa miaka karibia kumi na sita, inasemekana amekuwa akiwatenda watu ndivyo sivyo, na kisha kutumia nguvu zake za kipesa kuwanyamazisha watu hao, wasimpatie mashitaka yeyote.
    Inasemekana, katika makaratasi ya kimahakama, amenyanyasa watu kijinsia, amewapatia watu madawa ya kuwalevya bila kujijua, amewalazimisha wadada kuwa katika utumwa wa kingono kwa lazima, amawatengenezea watu pati za kingono na kisha kuwarekodi, kama njia ya kuwablakimaili, wasiweze kumfanya chechote.
    Inasemekana kuwa, kuna baadhi hata aliwaua. Hapo tunawaacha wengi ambao wanamlalamikia kuwa, amewatapeli haki zao za kimuziki.
    Hapo tunawaacha wengi ambao wanamlalamikia, amewashulumu mapato yao ya kazi zao za Sanaa. Kuchukua jasho la kazi zao walizofanya kihalali.
    Hapo tunawaacha wale ambao aliwanyanyasa, sababu tu walikuwa na shida, kwa hadaa kuwa atawapa nafasi, kutoka na nafasi yake katika biashara na Muziki.
    Na kwa miaka kumi na sita, ameyafanya haya, bila kuguswa na mkono wowote wa sheria. Kitu kilichomfanya aamini kuwa, yeye hagusiki. Kitu kilichomfanya aamini kuwa, pesa zake zitamlinda na lolote.

ความคิดเห็น •