RC MAKONGORO NYERERE ''WEKENI MIKAKATI YA KUMALIZA MADENI KUEPUKA MALALAMIKO ''

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ก.ย. 2024
  • WEKENI MIKAKATI YA KUMALIZA MADENI KUEPUKA MALALAMIKO NA KUZICHAFUA HALAMSHAURI ZETU-RC MAKONGORO
    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Charles Makongoro Nyerere ameshiriki katika Kikao cha Utekelzaji wa hoja za Ukaguzi na Mapendekezo ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali 2022/2023 kilichofanyika leo 18 juni 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga.
    Katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023 iliyotolewa Aprili, 2024 ilionyesha kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ilikuwa na Hoja za miaka ya nyuma ambazo hazijafungwa 28 na Hoja za Mwaka huu wa Ukaguzi (2022/2023) 25 hivyo kufanya Jumla ya Hoja 53 na Maagizo 6 ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) hayajatekelezwa mpaka sasa.
    Kupitia Kikao hicho Mheshimiwa Charles Mkongoro Nyerere ameagiza Mkurugenzi na Wataalam wake kushirikiana na Mkaguzi Mkuu wa Nje kufanya uhakiki ili Hoja hizi ziweze kufungwa na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Katibu Tawala Mkoa kuhusiana na usimamizi wa fedha na masuala ya kiutendaji katika Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuweka mipango na mikakati mathubuti ya Ulipaji wa madeni yote ya Halamsahuri yaliyobainishwa kwenye taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali
    Ili kuepusha malalamiko na kuzichafua Halmashauri.
    Aidha Kwa upande wa Usimamizi wa Miradi, amesema kuwa Mkurugenzi pamoja na timu yake ya Wataalam kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kama ilivyokusudiwa ili kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma Stahiki kwa wakati.
    Mheshimiwa Makongoro amesisitiza kwa waheshimiwa madiwani kuwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwaajili ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Waheshimiwa kutoa hamasa kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili mwakani watumie haki yao ya Kidemokrasia. Na kuongeza kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wao muda utakapo fika.
    Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe.Jastine Malisawa amesema kuwa kwa niaba ya Balaza la madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Watumishi mbalimbali waliopo ofisi ya Mkurugenzi wataendelea kushirikiana na kuona namna nzuri ya kuweza kupunguza hoja ambazo zimekuwa zikijitokeza katika hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na kusimamia tataribu za uendeshaji wa shughuli za Halmashauri.
    MWISHO.

ความคิดเห็น •