Kwanini kukosa kwako Ujuzi kunakufanya Ubaki Masikini wewe na familia yako?

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 26 ธ.ค. 2024
  • Mfumo wa maisha yetu, umetengenezwa kwa njia fulani ya kipekee kidogo. Ili mkono wako uweze kwenda kinywani, lazima kwanza uwe wa msaada kwa binadamu mwenzako anayekuzunguka.
    Hivi ndivyo ulimwengu ulivyoundwa. Ama unapenda, ama haupendi. Ili uweze kupata kitu, lazima uwe na kitu cha kutoa. Aidha ni ujuzi, nguvu kazi, burudani ama starehe.
    Kama hauna kitu cha kutoa. Kwa bahati mbaya, duniani namna ilivyo, itakudharau, hata kama uwe mwema kiasi gani. Na ukiwa una kitu cha kutoa, ambacho sio ujuzi, Dunia itakutumia na baadae kukutupa kama takataka.
    Hivyo basi, kama una malengo unayohitaji kuyatimiza. Lazimi pia uangalie una kipi cha kuipatia jamii. Na vipi kupitia kitu hicho, nawe unaweza timiza malengo yako.
    Kama wewe unataka kujikwamua kutoka kwenye umasikini, hatua ya kwanza, hakikisha unajifunza ujuzi wowote ambao unaweza kukufanya mtu akulipe pesa, kupitia ujuzi huo.
    Na hapa simaanishi elimu ya darasa la kwanza hadi la saba, au elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne, au elimu ya kidato cha tano na cha sita.
    Hapana, pamoja na uzuri na umuhimu wa elimu hii, bahati mbaya elimu hii haikupi ujuzi wote muhimu wa kuuza sokoni. Ni elimu nzuri tu ya kuchangamsha akili na kuondoa ujinga.
    Uzuri wa mazingira yetu ya Kitanzania, ni kuna njia rasmi za kujifunza ujuzi kupitia mfumo rasmi wa shule, kama vyuo vya ngazi zote. Unaweza enda kusoma ujuzi wowote kuanzia ngazi ya cheti, diploma mpaka degree. Njia hii wengi wanaoitumua ni wale wenye uwezo wa kulipa ada.
    Watu wanaweza jifunza mapishi, ushonaji, ufundi, udaktari, Muziki, uanasheria, uinjia na mengineyo. Ukiwa katika mazingira ambayo uwezo upo, ili ujikwamue na umasikini zingatia njia hii, baadae ntakuelezea kwanini.
    Njia ya pili, kama hauna uwezo wa kupitia njia ya hapo juu, ni kujifunza ujuzi kupitia njia zisizo rasmi. Mathalani huna uwezo wala vigezo vya kwenda chuo kujifunza ujuzi. Je ukate tamaa? Hapana. Lakini unataka ujifunze kuwa fundi umeme.
    Kitanzania kuna namna unaweza kujifunza kupitia kujiatachi kwa fundi umeme na kuwa msaidizi wa fundi kwa miaka kadhaa, ambapo mbali na kumsaidia kazi, atakufunza mbinu na ujuzi wa ufundi wa umeme.
    Hili lipo kwenye ufundi wa magari, ufundi uashi, useremala, Udijei, usimamizi wa biashara, kilimo na mengineyo mengi. Katika kupambana na umasikini na harakati za kujikwamua kutoka umasikini, ukikosa mbinu ya kwanza, itumie hii kupata ujuzi ili baadae uanze kupata hela kupitia kazi hizi.
    Kuna namna ya tatu, ambayo uzuri nayo imeanza kuchipuka Tanzania, ambayo inaweza wasaidia watu kupata ujuzi. Hata kama hauna vigezo au elimu, siku hizi kuna vyuo rasmi na visivyo rasmi, vya taasi za serikali na visivyo vya kiserikali, ambavyo vimefokasi katika kupatia watu ujuzi bila kuangalia vigezo vya kielimu.
    Mfano vipo vyuo vya watu vinafunza mapishi ya keki. Unataka kujua kupika keki, unaenda kujifunza kupika keki. Unataka kujifunza kazi za saluni, utajifunza kazi za saluni. Hakuna maswali kuhusu historia ya elimu yako utaulizwa. Unachotakiwa ufahamu, jasti bikozi haujasoma, haimanishi hauna akili au hauwezi kujifunza kitu. Kuna vitu vingi sana unaweza kujifunza na ukawa ujuzi wako, na sokoni vinahitajika.
    Pia kwa upande wa vipaji vya Sanaa, kuna chuo Cha Serikali kama TASUBA, ambao wao, kulingana na kipaji chako, watakufunza na kukiboresha, kufikia pointi ya kwenda kukiuza sokoni. Hawataangalia sijui una sii ngapi au dii ngapi. Hapa unaweza jifunza uchoraji, Udijei, kucheza Ngoma, kuigiza, Muziki, na vingine vingi.
    Hizi zote nilizokuelezea hapa, ni njia ambazo unaweza kuzitumia kukuza kipaji au kujenga ujuzi utakaoweza kuingia nao kwenye soko la ajira au kujiajiri.
    #umasikini #ujuzi

ความคิดเห็น •