Huu ndio ukweli mwanamke aliyepigwa visu 25 Rombo na kufariki

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 ต.ค. 2024
  • Beatrice Minja (47) mkazi wa kijiji cha Mbomai juu kata ya Tarakea mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kuchomwa kwa kisu mara 25 mwili mwake na kukaa ICU kwa siku 46 katika hospitali ya KCMC.
    Beatrice Minja alishambuliwa siku ya tarehe 12/11/2023 katika kijiji hicho majira ya jioni alipokua akitokea katika majukumu yake na mtu ambaye mpaka sasa hajakamatwa na jeshi la polisi.
    Akizungumzia tukio hilo mtoto wa marehemu,Glory Mchomba amesema mama yake alikua akifuatiliwa na kupewa vitisho na mtu ambaye hawakumtaja jina na aliripoti kituo cha polisi lakini aliachiwa kwa dhamana na aliendelea na vitisho na baadae mama yake kujeruhiwa.
    Aidha mdogo wa marehemu ,Joyce Minja amesema mhusika ameshakuja mara nyingi nyumbani na kutoa vitisho na kuomba jeshi la polisi liwasaidie.
    Jeshi la polisi Nchini limetoa taarifa na kuthibitisha kuwa marehemu huyo alifariki tarehe 27.12.2023 akiwa anaendelea kupokea matibabu kwenye hospitali hiyo.
    Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa ambaye baada ya kutelekeza tukio hilo alikimbia.

ความคิดเห็น • 8

  • @Patricia-t4k8x
    @Patricia-t4k8x 9 หลายเดือนก่อน

    Jamani poleni sana wanafamilia 😭😭😭😭😭😭😭

  • @lisawilliam2491
    @lisawilliam2491 9 หลายเดือนก่อน

    Polen

  • @annamadavid4152
    @annamadavid4152 9 หลายเดือนก่อน +1

    Mm kafaa!!

  • @chayomgonja3131
    @chayomgonja3131 9 หลายเดือนก่อน

    Hizo issue za pf3 ujinga mtupu.. mgonjwa anahitaji matibabu ya haraka mnaanza kukimbizana na polisi… serikali inabidi itafute utaratibu mwingine mambo ya aibu kbs karne hii

  • @callicevallice7383
    @callicevallice7383 9 หลายเดือนก่อน

    Mama Samia asaidie hii familia ipate haki yake. Inaumiza sana

  • @vibetz9991
    @vibetz9991 9 หลายเดือนก่อน

    Au madaktAri wa kcmc walichomoa betri baada ya kuskia ndugu hawana HeLa???????

  • @Hamy1109
    @Hamy1109 9 หลายเดือนก่อน +3

    Ndugu wa marehemu wamsake kimya kimya huyo mtuhumiwa wamalizane nae mtaani.

  • @inukauleunywe5717
    @inukauleunywe5717 9 หลายเดือนก่อน

    Kumbe watu wanamfahamu. Kama aliyasema hayo kwa watu ni dhahiri watu wanamfahamu