PROFESA MKENDA AJIVUNIA UWEKEZAJI HUU, ASIFU UWEKEZAJI WA VIJANA WA ROMBO NCHINI," INAONGOZA"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 ต.ค. 2024
  • Mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda amewapa tano vijana wachapakazi wanaotoka katika wilaya ya Rombo ambao wamefanya uwekezaji mkubwa hapa nchini na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa.
    Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia mesema serikali inajivunia uchapakazi wa vijana wanaotoka katika wilaya hiyo ambao wamewekeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo kwa Taifa.
    MKenda ameyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wanaoishi katika mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi jengo la uchumi la The Lavender ambalo limejengwa katika mtaa wa Kisasa sheli, Dodoma.
    Profesa Mkenda amesema vijana wengi ambao wamefanikiwa ni wale ambao wamekuwa wakijituma usiku na mchana kuhakikisha wanapiga hatua za kimaisha pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.
    Amesema wengi ambao wamefanikiwa ni wale ambao walitoka makwao bila chocho na kwamba walipofika mjini walionyesha juhudi za utafutaji na kufanikiwa ambapo amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono.
    Instagram #Bananafmtz #98.7 #BananafmKilimanjaro

ความคิดเห็น •