RC CHALAMILA APOKEA MELIVITA YA JESHI LA CHINA, INAFANYA MATIBABU, INA ROBOT "NI BURE JITOKEZENI"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 ส.ค. 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Julai 16,2024 amepokea Melivita ya matibabu iitwayo Peace Ark ya Jeshi la ukombozi la watu wa China katika Bandari ya Dar es Salaam.
    RC Chalamila akiongea wakati wa mapokezi hayo amesema Melivita hiyo itakuwepo katika Mkoa wetu kutoa huduma za kitabibu kwa wakazi wa mkoa huu na watanzania kwa ujumla kuanzia tarehe l16 Julai, 2024 hadi tarehe 23 Julai,2024 ambapo leo Julai 16, 2024 ni siku maalum ya uzinduzi, na kuanzia tarehe 18-23 Julai 2024 ndyio siku rasmi ya kuanza kutoa matibabu kwa wananchi. Huduma hizo za kitabibu zinatolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka sitini(60) ya ushirikiano kati ya Tanzania na China na maadhimisho ya miaka sitini (60) tangu kuanzishwa kwa JWTZ tarehe 01 Septemba,1964.
    Aidha RC Chalamila amesema huduma za kitabibu zinazotarajiwa kutolewa ni pamoja na vipimo, tiba za kawaida pamoja na upasuaji wa kawaida, magonjwa ya kina mama, mifupa, njia ya mkojo, macho, pua, koo, meno, moyo, utumbo pamoja na ngozi zilizoungua na moto ambapo matibabu hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa wataalamu wa Afya wa JWTZ, Hospitali ya Taifa Muhimbili,Tumbi,Amana,Mwananyala,Temeke,na Jeshi la China.
    Vilevile kutakuwa na kikundi cha Madaktari Bingwa watakaokuwa wanakwenda kutoa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mbagala , Hospitali ya Lugalo na Kunduchi ,Hospitali ya Amana, Bunju, Mwananyamala na Temeke pamoja na maeneo mengine ambayo ratiba rasmi itatolewa na JWTZ.
    Sanjari na hilo amesema wananchi watakaokwenda Bandarini kwenye Meli hiyo kwa ajili ya kupata matibabu wanataarifiwa wapitie geti namba mbili(2) la Bandari ya Dar es salaam.
    RC Chalamila amesema Matibabu hayo yatatolewa bure, hivyo ametoa rai kwa wananchi wanaohitaji huduma hizo kujitokeza kwa wingi kuitumia fursa hiyo ya kitabibu.

ความคิดเห็น • 57

  • @HajiKlein-so1rk
    @HajiKlein-so1rk หลายเดือนก่อน +2

    Safi 🇹🇿🇻🇳🇷🇺👏

  • @arjunimayagila9500
    @arjunimayagila9500 หลายเดือนก่อน +2

    Safi Sanaa inaonywsha kwao hakuna kabisa wagonjwa ndio maana wamehamia na kwetu china oyeee

  • @user-il5pk2dr5n
    @user-il5pk2dr5n หลายเดือนก่อน +1

    Kazi iendelee..

  • @msauzib
    @msauzib หลายเดือนก่อน +1

    😂😢😂 wahengw walinambia vya bure vinaua utajikuta washakuchomoa hata Figo

  • @godfreypaul251
    @godfreypaul251 หลายเดือนก่อน +4

    Si watupe kabisa tukae nayo

    • @adamhashim3352
      @adamhashim3352 หลายเดือนก่อน

      Hii ya chanjo ya covido😂

  • @tinnahagustinolyelu4247
    @tinnahagustinolyelu4247 หลายเดือนก่อน +1

    Mmmmmm mtapandikizwa mpaka magonjwa misaada hiyo vipi ingawa wachina ni marafiki zeetu lakini selikari kuweni makini wachina ni wajanja

  • @davinaheven4794
    @davinaheven4794 หลายเดือนก่อน +4

    😮😮😮😮😮We need to be careful

  • @meshajohn8713
    @meshajohn8713 หลายเดือนก่อน +1

    Hawa viongozi wanauza marizetu usiku nahawajaanza leo tangu mzee john,atuache kunadege lilikuja dom,,likaondoka,mda,usojulikanaa

    • @HusseinKarumna
      @HusseinKarumna หลายเดือนก่อน

      We hata kuandika hujui Mali unaandika Marizetu kazi kuandika vita hauna ushahidi navyo

    • @meshajohn8713
      @meshajohn8713 หลายเดือนก่อน

      @@HusseinKarumna kwani hujaelewa,,wee kumakweli ,,🤰

  • @SinemaZaChina
    @SinemaZaChina หลายเดือนก่อน

    sisi kama wachina tunawakaribisha sana

  • @kesterkanyala7718
    @kesterkanyala7718 หลายเดือนก่อน +1

    SHIDA...HAPA KWETU,KILA KITU ,AU MAMBO YOTE NI,"DAR ES SALAAM "....PEKE YAKE....
    -IWE HUDUMA,MICHEZO AU JAMBO MUHIMU,NI DAR..AU ZANZIBAR TU...

    • @salumalriyamy
      @salumalriyamy หลายเดือนก่อน

      Kwa hiyo hiyo meli ulitaka ifike vipi Dodoma kwa mfano?

    • @MANKOLOMATZ
      @MANKOLOMATZ หลายเดือนก่อน

      😂😂​@@salumalriyamy

    • @michaelgilbert1531
      @michaelgilbert1531 หลายเดือนก่อน

      Wnakuwaga pale central.posta

  • @JuhudiJotham
    @JuhudiJotham หลายเดือนก่อน +2

    Ina mambo yao,cdf wetu simuoni mbona,ndo alipaswa ahojiwe imeleta nini hasa,mchina hana rafiki ana maslahi kwake hasa,

    • @JamesJastin-bg1rx
      @JamesJastin-bg1rx หลายเดือนก่อน

      Acha kutafuta kiki ktk mitandao

  • @kingibandajembe2247
    @kingibandajembe2247 หลายเดือนก่อน +1

    Waizi wakubw mbwa hawa

  • @juliusmwakyando3207
    @juliusmwakyando3207 หลายเดือนก่อน

    🎉

  • @ramadhanimwajuma4701
    @ramadhanimwajuma4701 หลายเดือนก่อน

    Kila la kheri kwny maadhimisho ya miaka 60 tangu kuundwa kwa jeshi la ulinzi wananchi wa tanzania

  • @valentinernestkavishe7297
    @valentinernestkavishe7297 หลายเดือนก่อน

    Kenya waje tupigane

  • @christinainnocent3184
    @christinainnocent3184 หลายเดือนก่อน

    Huku America kuna shirika linatoa huduma kama hiyo nchi mbali mbali duniani huwa najiuliza mbona hawaji huko tz

  • @adamhashim3352
    @adamhashim3352 หลายเดือนก่อน +2

    Jipeleke mchanjwe muwekewe chip😂

    • @noonelike6382
      @noonelike6382 หลายเดือนก่อน

      😂😂😂😂

  • @victorvenantkaigarula6255
    @victorvenantkaigarula6255 หลายเดือนก่อน

    Tunashukuru, lakini tuwe makini yawezekana Tanzania ni sehemu ya Majaribio.

  • @bishweko
    @bishweko หลายเดือนก่อน

    Milladi hapo ushapeleka udaku US kuwa China wameleta meri ?

  • @frankndendu2570
    @frankndendu2570 หลายเดือนก่อน

    Tuwe makini jamani.

  • @sijalikifunyo912
    @sijalikifunyo912 หลายเดือนก่อน

    Kwanini waje wanajeshi?
    Nina shaka hapo!

  • @fetychina3969
    @fetychina3969 หลายเดือนก่อน

    Naombeni mnijuze alitaja hospital gani

  • @TeloAwor
    @TeloAwor หลายเดือนก่อน

    Corona???!!!!!

  • @elvisoscar9912
    @elvisoscar9912 หลายเดือนก่อน

    Waende marekani uku wasije

  • @IzackMakungu-ey9jx
    @IzackMakungu-ey9jx หลายเดือนก่อน

    Sasa serikali ijiongeze iliwapate utaalamu wa vifaa vitaa

  • @eddechriss2664
    @eddechriss2664 หลายเดือนก่อน

    Depending football club

  • @user-xc6ls9xn8h
    @user-xc6ls9xn8h หลายเดือนก่อน +1

    China safi sana kuja kwetu tanzania

  • @mubezimwesigwa5395
    @mubezimwesigwa5395 หลายเดือนก่อน

    Matibabu yanaanza lini??

  • @ladislausswai9554
    @ladislausswai9554 หลายเดือนก่อน

    NAOMBA LOCATION SEHEMU WANAPOTOA HAYO MATIBABU

  • @noonelike6382
    @noonelike6382 หลายเดือนก่อน +2

    Haya Sasa!.. fulsa hiyo Kwa Malaya wa daslamu. Wachina wana upwiru kama wote hao.

  • @fetychina3969
    @fetychina3969 หลายเดือนก่อน

    Kigamboni nilini mtujuze

  • @joshuambilinyi6655
    @joshuambilinyi6655 หลายเดือนก่อน

    Sasa mbona mnakwamisha biashara zingine sasa meli inakaaa mda gani pale gat

    • @ladislausswai9554
      @ladislausswai9554 หลายเดือนก่อน

      Kwani hayo matibabu yapo sehem gani?

  • @user-eb1im4dy7h
    @user-eb1im4dy7h หลายเดือนก่อน

    Hii mel inauzwaje?

  • @user-lj6ey7mr4w
    @user-lj6ey7mr4w หลายเดือนก่อน

    Watanzania jamani tuwe makini tusijekua majaribio ya virusi fulani

    • @ChristopherKayera
      @ChristopherKayera หลายเดือนก่อน +1

      Virüsü gani sasa mbona huvitaji,kabla hujazaliwa meli za kivita za China na Nchi nyinginezo Ndio utartibu wao kutembea Dunia nzima kutoa matibabu

  • @fggcggdsgdcdsd8854
    @fggcggdsgdcdsd8854 หลายเดือนก่อน +2

    yani mchina achome mafuta kutoka china aje Tanzania afu akutibu bure?? sawa ni matokeo ya mahusiano kati yetu na wao, sisi tuna toa nini katika mahusiano hayo?? enewi tuendelee kunywa mtori

    • @IzackMakungu-ey9jx
      @IzackMakungu-ey9jx หลายเดือนก่อน

      Inaonekana wew unapenda kutoa sanaa

    • @jonasmbwambo3546
      @jonasmbwambo3546 หลายเดือนก่อน

      Uko Sawa kaka aisyekuwa na D Tatu hawezi kuelewa

  • @DaimaNyakunga-jb6do
    @DaimaNyakunga-jb6do หลายเดือนก่อน

    Acha ujinga ww mhehe

  • @nathanlusulo-po2lj
    @nathanlusulo-po2lj หลายเดือนก่อน

    Majaribio kwa nyani sio mtu

  • @hoseastephen4508
    @hoseastephen4508 หลายเดือนก่อน

    Ebwana ama kweli hiyo lugha Wabongo ilishatukataa piece of land kumbe inamaanisha eneo la amani 😂😂😂

    • @furahamwangosi3896
      @furahamwangosi3896 หลายเดือนก่อน

      😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂