SENYAMULE ATOA TAMKO MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOA WA DODOMA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ต.ค. 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Ametoa tamko kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 12 Februari 2024 mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Juu Jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
    Mhe. Senyamule amesema lengo Kuu la kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa Maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbali mbali za Kimataifa, Kikanda na zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na uwekezaji kwa Wanawake.
    “Kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo pamoja na kuelezea jitihada mbalimbali za Serikali na wadau mbalimbali katika kuwajengea uwezo wanawake.
    “Mwaka 2024 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma itaadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na makundi maalum pamoja na Taasisi ya FAGDI. Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kwa namna tofauti na miaka mingine na Kimkoa yataadhimishwa katika Wilaya ya Chamwino”. Ameongeza Mhe. Senyamule
    Maadhimisho ayo yatafanyika katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimuwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ความคิดเห็น •