PADRI ALIYEBAMBIKIWA KESI ya UBAKAJI AELEZA kwa UCHUNGU, "ALINIAMBIA HAJAONA SIKU ZAKE"..

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 24 ต.ค. 2021
  • PADRI ALIYEBAMBIKIWA KESI ya UBAKAJI AELEZA kwa UCHUNGU, "ALINIAMBIA HAJAONA SIKU ZAKE"..
    Takribani mwaka mmoja na miezi ipatayo miwili tangu padri Erasmos Swai alipofikishwa mahakamani kwa kosa linalosadikika kusingiziwa na watu wenye nia ovu juu yake na kuidanganya mahakama kuwa padri Erasmos Swai alifanya kitendo cha ubakaji na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne...
    Mnamo Tar 21.10.2021 hakimu Thrustone Kombe aliifutilia mbali kesi hiyo kwa kukosa ushahidi wenye uweledi ikiwemo kutokufika kwa vithibitisho vya vina saba baada ya binti huyo kujifungua mtoto ambapo hapo awali alisema ujauzito huo alipewa na padri huyo
    ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/globalradio/
    ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
    ⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
    ⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx
    ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: • GLOBAL COMEDY/MOVIES
    ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
    ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982)
    ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
    ⚫️ OUR PLAYLISTS:
    ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
    ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
    ⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globalradio
    ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusive_interviews
    ⚫️ Subscribe Global TV bit.ly/globaltvonline

ความคิดเห็น • 1.3K

  • @methodiutou7278
    @methodiutou7278 2 ปีที่แล้ว +98

    Glory to God! Mungu ndiye Jaji na Hakimu, hakika Mungu aliyeruhusu hayo na atatenda makubwa zaidi na zaidi kwako. Ila ile wao maana hukumu ya Mungu ni haki na ya milele.Pole sana Padri

  • @pulikisia7963
    @pulikisia7963 2 ปีที่แล้ว +43

    Tulishinda kesi bila ya mtetezi,tulikula mtama kwa maji tukanawili kuliko wao,hatukupambwa kama wao tukapendeza zaidi yao,walitubadilisha majina hawakubadili hatima,walipotutupa shimoni tukaibukia ikulu,kule walipotukusumia ndiko Mungu hupumzikia,walidhani wanatukimbiza kumbe wanatusindikiza.Bwana wangu,Yesu,Yesu,Yesu........By Ambwene Mwasongwe.

  • @happyshayo372
    @happyshayo372 2 ปีที่แล้ว +48

    Sijui kwa nini nalia tu kadri ninavyoendelea kumsikiliza padri anavyojieleza. Dah 😭😭😭😭😭 huyu mwanafunzi Mungu anamuona😭😭😭

  • @severimkatomutegeki6930
    @severimkatomutegeki6930 7 วันที่ผ่านมา +1

    Tumsifu Yesu Kristu Padri Swai pole kwa hayo matukio Mungu akupe uvumilivu na Kumshukuru daima . Mungu akujarie urejee kwenye uduma ya kiroho.

  • @nickson3473
    @nickson3473 2 ปีที่แล้ว +6

    Hii kazi ni ngumu sana, nilipomaliza darasa la saba nilikuwa na hamu ya upadri, ila nilipokaa seminarini nilisoma maisha ya mapadre kwa makini sana, nilikiri ni kazi ngumu inayohitaji moyo sana, niliondoka form four, nilisema Mungu anisaidie niendelee na safari ya maisha, MTUMISHI VIATU ULIVYOVAA NI VIGUMU SANA, MUNGU AKUTIE NGUVU

  • @edakiputa1108
    @edakiputa1108 2 ปีที่แล้ว +33

    Padri nimejifunza kitu kikubwa sana kwako, (msamaha)Mungu azidi kukutetea na kujidhihirisha ktk hili, Amina.

  • @tumaininyambita5002
    @tumaininyambita5002 2 ปีที่แล้ว +65

    Pole sana baba,hiyo ndio sadaka ya kweli maana imekupa maumivu makali sana.Mungu akutie nguvu wewe ni dhahabu iliyopita Kwenye moto .

    • @nelsonpaul4618
      @nelsonpaul4618 2 ปีที่แล้ว +1

      Pole sana padri

    • @hubman6780
      @hubman6780 2 ปีที่แล้ว +1

      Covert plans are lean on to exterminate compitent people. Baba fuatilia pia maisha ya babako mzazi huenda alipobarikiwa baraka za maisha walimuinukia.Ombea roho ya ulinzi na karama ya heshima.
      Naomba Mungu akutunze na kazi wakurejeshee palepale au usharika wa jirani

    • @victoriabayo7704
      @victoriabayo7704 ปีที่แล้ว

      Pole sana father Mungu siku zote yupo upande wa kweli na ataendelea kukusimamia

  • @kaguhewilly1905
    @kaguhewilly1905 2 ปีที่แล้ว +16

    Pole father, ndugu wakristu waombeeni viongozi wetu wa dini, wanapitia changamoto nying nying sana, wanajaribiw sana sana, wanapitia mambo magumu ambayo wao pia kam binadamu wadhaifu kuna kipindi wanaanguka dhambini lkn katika yote tuwaombee sana sana viongozi wetu wa dini, Mungu aliewapa kibali cha kuwa na wito walionao atawashindia daima katika mabaya yote!! Father Mungu ni mwema kupitia wewe kuna ya kujifunza mengi kupitia hili, ndugu wakristu tuwaombee viongozi wetu wa dini tuwaombee sana sana sana!!

  • @markogallus2046
    @markogallus2046 2 ปีที่แล้ว +16

    Mwenyezi Mungu aliyekuongoza katika kipindi chote hicho kigimu, atakuongoza katika kipindi choote cha utume wako Baba Padre... May Almighty God Bless you..🙏🏽🙏🏽🙏🏽

  • @ramadhanmohamedi9793
    @ramadhanmohamedi9793 2 ปีที่แล้ว +11

    Wadwahil wanasema tenda wemaa nendazako kilichokusaidia mpakasasa kuwa huru namanisha uraian ilimtanguliza mwenyezi mungu mbere mhukuru sana meenyezi mungu polesana

  • @boniphacemasau3068
    @boniphacemasau3068 2 ปีที่แล้ว +48

    Maelezo ya padri tu naamini kabisa hajafanya hivyo. Mungu yu nawe.

    • @rosekimaro384
      @rosekimaro384 8 วันที่ผ่านมา

      Kabisa huyu mungu mwacheni tu❤❤

  • @michaelrimisho
    @michaelrimisho 2 ปีที่แล้ว +38

    Pole sana father, jirani yangu..nakumbuka sherehe yako ya misa ya shukrani 2009 ...Mungu azidi kuwa nawe daima!!

    • @juliethkavishe1586
      @juliethkavishe1586 2 ปีที่แล้ว

      Walter wew Uko poa? Felix hajambo?

    • @deus8629
      @deus8629 ปีที่แล้ว +1

      Alafu na ww ulikimbia upadre bisha nitoe ushaidi

    • @michaelrimisho
      @michaelrimisho ปีที่แล้ว

      @@deus8629 🤗🤗hapana bhana sijakimbia

    • @janetmallya3242
      @janetmallya3242 ปีที่แล้ว

      mm huyu ndio amenikominisha na kipaimara padree wangu

  • @angelanaftael7965
    @angelanaftael7965 2 ปีที่แล้ว +23

    Ni kweli kabla ya kutenda wema ni muhimu kummuuliza Mungu ili adui asipate nafasi katika wema huo.Mungu akusaidie sana na akuponye majeraha yako father.hakika Mungu yuko na atakujibia wa haki.

    • @mwanga3358
      @mwanga3358 2 ปีที่แล้ว +1

      Kweli kabisa dunia inatisha Mungu atupe utambuzi, na hilo tu ni mipango ya shetani ili watu wasifanye mapenizi kwasababu watu wataanza kuogopa kusaidia

    • @gracenavilo7946
      @gracenavilo7946 2 ปีที่แล้ว

      Mungu Ni hakimu wa haki ,,Atazidi kutenda Mambo makubwa kwako.Wakapate aibu

    • @zuwenaabdallah7748
      @zuwenaabdallah7748 ปีที่แล้ว

      Yaan kaongea kwa hisia sana Mungu akufariji padre😪

  • @lizzy2423
    @lizzy2423 2 ปีที่แล้ว +13

    Jmn Huyu Binti kwanini ameamua kumchafua Padri na Kuharibu Ajira Ya Padri. Ambaye aliyejiitolea Kumsaidia. Watumishi Sasa wataogopa Kusaidia wahitaji. Padri Swai pole Sana. Mungu akulinde na maadui

    • @trophywilson7211
      @trophywilson7211 2 ปีที่แล้ว +1

      Alimpenda Padre huyo

    • @prosperjohn4298
      @prosperjohn4298 2 ปีที่แล้ว +1

      Kuna mtu yupo nyuma yake na ana vihela hela,, Ila Mungu Yu kazini

  • @annambokaanatoli9700
    @annambokaanatoli9700 2 ปีที่แล้ว +9

    Father umeniumiza sana wengi tulisikia hatukujua UKWELI ni uongo wa magazeti. Mungu akulinde Bikira Maria akufiche kwenye bushuti lake... umenipa nguvu ya IMANI kuwa Mungu anawatuona.. because God is God of mercy

  • @toma634
    @toma634 2 ปีที่แล้ว +8

    Nimelia kwakweli mnavyojitoa hivyo bado mtu anakubambia ujinga huo Ooh Mungu wangu lkn Mungu anasamehe na ww wasamehe pia nawapenda sana mapadre Mungu awatie nguvu🙏🏻🙏🏻

  • @tonymsoma1666
    @tonymsoma1666 2 ปีที่แล้ว +13

    Inauma sana😥😥😥......Wamekuchafua lkn Mwenyezi Mungu atakung'arisha bb padre......Endelea kusimama na Mungu mpaka Shetan ashangae.......

    • @phatumaibrahim8329
      @phatumaibrahim8329 2 ปีที่แล้ว

      Xn Tena ila mungu yupo pamoja nae

    • @dionisiamlowe6759
      @dionisiamlowe6759 2 ปีที่แล้ว +2

      Jamani alichofanyiwa huyu mimi pia nilifanyiwa sema mimi niliponea chupuchupu kupelekwa polisi kwa kuwasaidia watu wanaokuja kanisani kuomba msaada nilijitoa kuwasaidia kumbe nategwa kama huyo mtumishi

    • @janethkomba4485
      @janethkomba4485 ปีที่แล้ว +2

      ​@@dionisiamlowe6759 poleni sanaa 😭kwakwer inaumiza Sanaa😭Wema Unageka kuwa ubaya😭kwakwer Mungu Awasaidiye Sanaa🙏

  • @mariaregulla5215
    @mariaregulla5215 2 ปีที่แล้ว +28

    Pole sana padre kweli inaumiza sana,,,Mungu ndiye hakimu na mwamuzi wa wanyonge

    • @neemakileo3181
      @neemakileo3181 2 ปีที่แล้ว +1

      Pole sana Padri Mungu atakusaidia zaidi ya hapo atakurudishia vyote ulivyopoteza na zaidi ya hivyo

    • @rosetenga6979
      @rosetenga6979 2 ปีที่แล้ว

      Pole Sana padre Mungu ndio hakimu wetu 😭😭😭😭

  • @FlavianMallya
    @FlavianMallya 4 วันที่ผ่านมา

    Father God bless you hakika hukumu yao i tayari mbele zaBwana Mungu wasamehe Bure!

  • @jeunajuatv817
    @jeunajuatv817 2 ปีที่แล้ว +25

    huyu padr namjua alikuwa parokia ya manushi kabla ya kuhama. alikuwa mtu mwema sana

  • @gracekagoma3231
    @gracekagoma3231 2 ปีที่แล้ว +17

    Pole sana padri.Huyo i binti amelaaniwa Tenda wema wende zako..Hata Yesu alisuribiwa bila makosa.Huyo binti mi shetani mkubwa mwenye miguu saba.

  • @mariajoseph3743
    @mariajoseph3743 10 หลายเดือนก่อน +2

    Pole Sana padri Mimi kanisa katorik wamenisomesha hao mapadr Mungu awabariki Sana najivunia kuwa mkatoriki

  • @epimackmkunde2264
    @epimackmkunde2264 2 ปีที่แล้ว +11

    Pole Rev. Fr. Erasmes. Mungu Yuko nawe na kamwe usirudi nyuma. Nakufahamu vyema na njia yako kufikia utume wako. Mungu ataonesha njia.

  • @zawadjose5440
    @zawadjose5440 2 ปีที่แล้ว +11

    POLE FATHER , POLE SANA BABA USIJALI KWA HILO .MUNGU YUPO NAWE

  • @goodluckmshana6765
    @goodluckmshana6765 2 ปีที่แล้ว +27

    Nikupe pole za dhati Padre. Hadithi Hii ni ngumu sana kumeza lakini Mungu amekufungulia njia mpya…

    • @mamandekirwa5751
      @mamandekirwa5751 2 ปีที่แล้ว

      Pole Sana Padre mungu azidi kukupa Amani ndani ya moyo na uwe na Afya njema ya Imani

    • @Zaburi-
      @Zaburi- 2 ปีที่แล้ว

      @@mamandekirwa5751 Mungu/MUNGU na sio mungu

  • @richardsoka2400
    @richardsoka2400 2 ปีที่แล้ว +13

    FIDIA NI KAZI YA MUNGU! wonderful! May the Almighty God Bless you Father and grant you long life. Kweli huwezi dai fidia kutoka kwa Shetani.

  • @mamachris6811
    @mamachris6811 2 ปีที่แล้ว +6

    Padre
    Hapo kwa marafiki,mshukuru Mungu,maana kupitia hili,umejua marafiki wa kweli na wanafki

    • @dafrozakahamba8707
      @dafrozakahamba8707 2 ปีที่แล้ว

      Mungu pigana nao wanaopigana nami zab:35 Hongera Fr.kwa kujua kuwa unajukumu la kusamehe. Mungu atakupigania siku zote. Zab.121.

  • @manuelnuer3329
    @manuelnuer3329 2 ปีที่แล้ว +8

    Mtumishi wa Bwana hupitia vikwazo vingi mwenyezi Mungu yu pamoja nasi

  • @emamkuyu4061
    @emamkuyu4061 2 ปีที่แล้ว +11

    Pole sana mtumishi wa Mungu.Lakini nakuhakikishia ubaya hauna kwao wahusika wote Yesu ni jibu.Watapigwa dhoruba kali mno.

  • @teddymassawe2834
    @teddymassawe2834 12 วันที่ผ่านมา

    Hata yesu alisulubiwa Kwa ajili ya wanadamu .pole sana kaka yangu.

  • @s0phialwassa574
    @s0phialwassa574 2 ปีที่แล้ว +7

    Anaongea Padri ila moyo unaniuma mimi, pole sana Baba

  • @judithkemunto2403
    @judithkemunto2403 2 ปีที่แล้ว +29

    This earth is hard, tunahitaji ukombozi wakiroho,may God give you wisdom padri🙏

  • @adamuibrahimu5868
    @adamuibrahimu5868 2 ปีที่แล้ว +13

    Pole sana baba Padri. Umekuwa dhahabu mpya, stephano shahidi. Mungu YU PAMOJA NAWE.

    • @mikaelmbombo528
      @mikaelmbombo528 2 ปีที่แล้ว +1

      🙏🙏🙏waa mgemeyae mungu ni kama mlima sayuni

  • @dunstangeorge3263
    @dunstangeorge3263 2 ปีที่แล้ว +16

    Pole sana Fr Erasmus, Mungu wetu yupo kazini, wema wako kamwe hausahauliki, iyo familia Mungu atailaani.

  • @ernestgeorge8412
    @ernestgeorge8412 หลายเดือนก่อน +1

    Pole Sana father, samehe kwa maana imeandikwa tusamehe saba mara sabin.. Kila jambo linasababu huenda Mungu hakupanga kwa kipind hicho uendelee na utumishi, upo wakat sahihi wa Mungu utainuka na utasimama upya 🙏

  • @neyjohn923
    @neyjohn923 2 ปีที่แล้ว +21

    Dah! Mungu amrehemu huyo dada na familia nzima. Hii ni laana ya kizazi. Itawatafuna mpaka kizazi cha nne. Pole sana Fr. Mungu akuponye kwenye mahangaiko yako. Safi sana kwa kujituma. Nondo nondo! Chuma chuma.

    • @Fm-MornStar2014
      @Fm-MornStar2014 2 ปีที่แล้ว +7

      Hongeza sauti maana wengi hawalijui hilo. Hata isingekuwa ni Padre, tuhuma za namna hii ni mbaya sana.

  • @sr.teresakarugaba9883
    @sr.teresakarugaba9883 2 ปีที่แล้ว +63

    Courage Fr, you have been Christ's witness, and He is experiencing the pain with you, surrender to Him by forgiving and praying for them. May God strengthen you in your difficulty moments.

    • @maxwellking9399
      @maxwellking9399 2 ปีที่แล้ว

      Hello Sr Teresa, Thanks kindly for your courageous and kindly words to Fr Swai.

    • @anwaritesal4695
      @anwaritesal4695 2 ปีที่แล้ว

      Thanks to God.

    • @newug3347
      @newug3347 2 ปีที่แล้ว

      Sr kwani unaelewa Kiswahili??

    • @angelomedard
      @angelomedard 2 ปีที่แล้ว

      Right says

    • @jumanesaidi7635
      @jumanesaidi7635 ปีที่แล้ว

      INASIKITISHA ! !

  • @andrewmatunu4186
    @andrewmatunu4186 10 หลายเดือนก่อน +1

    Pole Sana padre
    Psalm 23
    Bwana Mungu ni Mchungaji mwema hutapungukiwa na kitu....

  • @jerrymboyya2346
    @jerrymboyya2346 2 ปีที่แล้ว +9

    Mungu akutie nguvu baba . Kwenye haki nikama( dhuluma nahaki) hafichanganyiki. Naamini Mungu yupo pamoja nawe pia🙏🙏

  • @lydiarichard8307
    @lydiarichard8307 2 ปีที่แล้ว +6

    Samehe tu Mungu ndo mwenye kutoa kisasi we samehe acha maisha yaendelee

  • @theresianduku9837
    @theresianduku9837 2 ปีที่แล้ว +26

    With God all things are possible.father, waombee waweze kuchegi tabia zao.wasidhulu wengine

  • @neemamtumbati607
    @neemamtumbati607 2 ปีที่แล้ว +16

    Pole sana baba, Tunakuombea urudi katika utume, simama imara, shetani aliona kazi zake zinaharibiwa na utume wako, akatafuta mtu akumalize, ameshundwaa kwa jina la Yesu🙏

  • @teddymassawe2834
    @teddymassawe2834 12 วันที่ผ่านมา

    Kaka swai pole sana.nimejifunza meñgi sana kwako Lile neno tuu kusamehe.

  • @josephinegravasiano8860
    @josephinegravasiano8860 2 ปีที่แล้ว +27

    Jaman pole Father nilpoisikia niliumia sana,Mungu akutetee baba penye uongo ukweli hujitenga.

    • @gracemgandu716
      @gracemgandu716 2 ปีที่แล้ว

      Pole baba kwa changamoto kiimani fanya kazi uliyoitiwa mungu

  • @ceciliaonyango5488
    @ceciliaonyango5488 2 ปีที่แล้ว +16

    Shetani yuko kazini kuwadhoofisha watumishi was Mungu usijali Mungu atakulipia Ili dhahabu ingae lazima ipitie kwenye moto Yesu ndie jibu

  • @davidndyamukama3148
    @davidndyamukama3148 7 หลายเดือนก่อน +1

    Kuna wakati unamsikia mtu animba wimbo wa masikitiko pasina sababu. Huo ndo ulikuwa wakati wa kuimba Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana wakati wa mateso. Pole sana Fr.

  • @SuperCamle
    @SuperCamle 2 ปีที่แล้ว +6

    Mungu ni Mkuu sana. Asante sana Fr. Swahi kwa kufa na kufufuka na Yesu mwenyewe. Maelezo yako na mang'amuzi uliyoyapitia yamenigusa sana na kuona jinsi ulivyo ndani ya Yesu, jinsi ulivyofanyika padre, na jinsi unavyojitoa kuokoa Roho zetu waumini wako. Nimejofunza toka kwako uthabiti katika imani, umahili katika maisha na moyo wa Huruma. Mungu azidi kukuimarisha baba na kukuponya majeraha yote. Umepitishwa katika tanulu ya Moto ili ung'ae zaidi. Bwana na apewe sifa.

    • @veronicamduba2864
      @veronicamduba2864 2 ปีที่แล้ว

      Pole sana padre mungu pekee ndiye hakimu wa kweli njama zao zimeshindwa kwa jina la yesu

    • @edithashayo7546
      @edithashayo7546 2 ปีที่แล้ว

      Mungu wa huruma wahurumie waliomsingizia padri. Wafungue dhambi yao wape moyo wa kuomba msamaha

  • @fridahisaac1462
    @fridahisaac1462 2 ปีที่แล้ว +4

    Long life father!.Acha hii vita sio yako baba,utapiganiwa na MUNGU.Hii Familia ya huyu binti ijitafakari sana hata waweze kujitambua waombe msamaha.Nimejikuta nalia hii habari niliisikia tuu kwenye radio na kuona kwenye magazeti nikawa staki hata kusikia leo nmekusikiliza Father.Hata dhahabu ikipitishwa kwenye moto itang'ara tuu

  • @alphonceikandilo1101
    @alphonceikandilo1101 2 ปีที่แล้ว +5

    Pole sana baba Swai kwa yote uliyopitia hakika Mungu ni mwema kila kitu kitadhihirika na utarejeshewa huduma kwa imani.

  • @bartholomewluwanja6693
    @bartholomewluwanja6693 หลายเดือนก่อน

    Yes father Mungu pekee ndiye atakaye kulipia fidia!!!! Wewe leo ni mwalimu wetu kiroho wakimatendo. ❤❤❤❤❤❤

  • @yohanamaiga3031
    @yohanamaiga3031 2 ปีที่แล้ว +6

    Pole sana Baba. Ndo maisha ya hapa duniani. Ndo maana Yesu alisema Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu. Mungu azidi kuwa pamoja nawe Fr.

  • @msofe1985
    @msofe1985 2 ปีที่แล้ว +17

    Pole sana Pd. Mungu akupe mwanzo mpya wenye hekima ya Mungu, inahuzunisha sana, Mtetezi wako yu hai.Nimejifunza mengi sana kutoka kwako Pd.

  • @maryrwelengera5665
    @maryrwelengera5665 2 ปีที่แล้ว +24

    Pole sana mtumishi wa Mungu, wewe ni shahidi mwaminifu na wa kweli. Hiyo familia hiombe msamaha araka kabla Mungu ajafa ya ya kwake. Umenifunza mengi Fr. Asante mama mzazi wako na ndugu na majirani. Kwa wema wa kumtunza Padre wetu.

  • @paulmayala9798
    @paulmayala9798 7 หลายเดือนก่อน +1

    Atukuzwe Yesu kwaajili ya Fr. Swai!

  • @apostleprophetkennethngoli657
    @apostleprophetkennethngoli657 2 ปีที่แล้ว +16

    Inaumiza sana
    Hakika hii familia imepata hasara kubwa kwa jambo hili.
    Hongera kwa maneno ya Hekima hii kubwa

  • @mariavianeypeter2991
    @mariavianeypeter2991 2 ปีที่แล้ว +12

    Maadui wa kanisa na kwa watumishi wa Mungu ni wengi. Pole sana padri Mungu atakupigania.

    • @beatricejohn800
      @beatricejohn800 ปีที่แล้ว

      Sometime ukweli unajificha kwenye uongo,kwanini Padre aonane na mwanafunzi hotel? Kwanini asinge onana naye ofisini kwake? Hapo Padre kala buana siamini mwanafunzi asingizie yeye

    • @mariavianeypeter2991
      @mariavianeypeter2991 ปีที่แล้ว +1

      @@beatricejohn800 anayejua ni Mungu ndiye anayehukumu

  • @melaniaantoni5845
    @melaniaantoni5845 2 ปีที่แล้ว +8

    Padri swai jipe moyo mkuu wote tuko Nyuma yako tunakuombea . Hongera kwa ujasiri wako huo nasi tumejifunza mengi kwa hayo yaliyonipata .Tunakupenda na tunakuombea sana .Kwa Mungu sote tuna nanafasi ndani ya moyo wake.

    • @catherinphilipo3503
      @catherinphilipo3503 2 ปีที่แล้ว

      Poleeeeeee padri wangu hapo hata maelezo yana jitosheleza poleeee ww tenda wena nenda zako nakupendaaa jmn piya niombee sana na matatizo yako

  • @winnerjudith2007
    @winnerjudith2007 2 ปีที่แล้ว +15

    Pole sana Padri Mungu alikupitisha hapo ili kukupandisha viwango vya juu, ni sawa na Yusufu kwenye Biblia. Mungu kakushindia

    • @charlesjustin4805
      @charlesjustin4805 2 ปีที่แล้ว

      Nimesikiliza mara 2 nikagundua fr ameonewa mnooo

  • @ceciliesulle2812
    @ceciliesulle2812 2 ปีที่แล้ว +7

    Hofu ya Mungu wanadamu, mwogopeni Mungu. Maumivu aliyonayo Baba huyu da!!!

  • @mariasafari1004
    @mariasafari1004 2 ปีที่แล้ว +17

    Wanadamu hawana shukrani kabs,na maskini ndo ambao hawana shukrani kabs.

    • @francisemmanuel1551
      @francisemmanuel1551 2 ปีที่แล้ว

      Adui wa mwafrica ni mwafrica

    • @sumayasumaya6455
      @sumayasumaya6455 2 ปีที่แล้ว +1

      Maria safari..kama ungekua mwanaume ningekupa bint.yangu bureeeee uoe..na mtaji nawapa wa biashara kuubwaa..., Sie sio watu kabisa tena ukitaka kuthibitisha kuwa na msaada kwao..utaona dunia juu chin chin juu..eeh mungu tuokoe

    • @mariasafari1004
      @mariasafari1004 2 ปีที่แล้ว

      @@sumayasumaya6455 sasa unasomeshwa Bure halafu haohao wazazi wapotolo hawaoni kama Padre wawatu kawahurumia ndo nn dahhhhh

  • @aroldcharles7753
    @aroldcharles7753 2 ปีที่แล้ว +17

    Mungu akukumbuke Fr katika sadaka zote ulizotoa kwa ajili ya utukufu wake..

  • @YustaAlfonsi
    @YustaAlfonsi ปีที่แล้ว +1

    Pole Sana padri nae mungu atajibu kadiri aonavyo yeye na macho yake.

  • @annasanga733
    @annasanga733 2 ปีที่แล้ว +11

    Pole sana baba na hongera kwa ujasiri Mungu ni mwema kila wakati. Endelea kutenda kazi ya Mungu na yeye atatenda sawasawa na mapenzi yake.

  • @angelsblackboard8008
    @angelsblackboard8008 2 ปีที่แล้ว +22

    Mapadri wanapitiaga mitihani mingi sana, kusingiziwa , kudhihakiwa, yani. Mungu awasimamie sana.

    • @temuemanuel4671
      @temuemanuel4671 2 ปีที่แล้ว

      Amina.

    • @bulugubujashi6378
      @bulugubujashi6378 2 ปีที่แล้ว +2

      Kunawakati mwingine hawasingiziwi,mana engine wamezaa mtaani

    • @maryomiro5701
      @maryomiro5701 2 ปีที่แล้ว

      POLE SANA BABA PADRI MUNGU AKUPONYE MAJERAHA ULIOPATA NI VIGUMU KUAMINI,LAKINI JIPE MOYO KWANI HATA YESU ALITESWA KWA WEMA ALIYOTENDA,ENDELEA KUMTUKUZA MUNGU KWA HILO KUNA KITU TUNAJIFUNZA KWAKO HURUMA ILETAYO MATESO BILA KUTARAJIA, POLE MTUMISHI WA MUNGU,

    • @angelsblackboard8008
      @angelsblackboard8008 2 ปีที่แล้ว +1

      @@bulugubujashi6378 mara nyingi wanasingiziwa kuliko kweli. Amini. Yanakuzwa na shetani baba wa uongo.

    • @bulugubujashi6378
      @bulugubujashi6378 2 ปีที่แล้ว +1

      @@angelsblackboard8008 nikweli ila pia wapo waliozaa mtaani nawanao Tembea nawadada mtaani wapo ila najaribu kuwaza tu.

  • @anyesimaholo8553
    @anyesimaholo8553 2 ปีที่แล้ว +7

    Pole sana father, tumewatupia sana mawe, tumewaumiza sana, Mungu akutie nguvu. Ushuhuda wako utawafungua maadui wa kanisa. Ila mababa zetu mapadre mkitoa misaada kwa hawa watu kuweni makini, wengine ni masikini ila ni agents wa shetani.

    • @marykarebeti9410
      @marykarebeti9410 2 ปีที่แล้ว +2

      Kweli kabisa ndugu. Umeongea vyema saana. Umakini uongezeke kwa watumishi wa Mungu wanaotoa misaada. Wakumbuke sheteni yuko kazini.

    • @temuemanuel4671
      @temuemanuel4671 2 ปีที่แล้ว

      Kweli kabisa ndugu.

    • @omaryjudasymwanga7172
      @omaryjudasymwanga7172 2 ปีที่แล้ว

      Unamtoa paka kisimani asante ni kukuparua ila anyway kweli kama hatakiri na kusafisha huyo padri huyo bint atajapata balaa yeye na uzao wake

  • @regybahati5986
    @regybahati5986 2 ปีที่แล้ว +1

    Pole Baba, pole Sana, sadaka ya maisha yako kwa Mungu itakulinda. Hilo teso tolea kwa Mungu Kama Sala ya kuokoa roho za wakosefu na za walioko toharani. Fr. Bahati.

  • @traudkamugisha8051
    @traudkamugisha8051 2 ปีที่แล้ว +13

    pole sana padre mwachie Mungu atakulipia.

  • @aurorabenedicto3197
    @aurorabenedicto3197 2 ปีที่แล้ว +29

    Pole sana padre waliokungizia Mungu atatenda tu juu yao,na wewe kumbuka waliochaguliwa na Mungu hushambuliwa sana na majaribu hii ni moja ya hatua ya utakatifu Mungu akupe nguvu Baba padre.⛪

    • @temuemanuel4671
      @temuemanuel4671 2 ปีที่แล้ว +4

      Ni kweli ndugu yangu. Nimegundua mapadre hushambuliwa sana kwa kusingiziwa, mara nyingi huishia bila mtetezi na kuonekana mashetani lkn Mungu huwa mtetezi wao daima kwa kuwa yeye ndiye aliyewachagua na kuwatuma kuchunga kondoo zake. Mungu ampe nguvu huyu Padre na kuimarisha utume wake

    • @joshuabongole3837
      @joshuabongole3837 2 ปีที่แล้ว +8

      Kweli Dunia hii kabla hujamsaidia mtu mwombe Mungu kwanza akuonyeshe maono

    • @anyesimaholo8553
      @anyesimaholo8553 2 ปีที่แล้ว +2

      @@temuemanuel4671 ee kaka yangu mapadre hawana mtetezi mara nyingi na tunawagandamiza sana, kinachoumiza sana ni wakristu wanaowahudumia ndiyo wanaowafanyia ubaya.

    • @temuemanuel4671
      @temuemanuel4671 2 ปีที่แล้ว +1

      @@anyesimaholo8553 Ni kweli Dada Anyesi Maholo

    • @rosebeauty700
      @rosebeauty700 2 ปีที่แล้ว +1

      Ni Hatua ya utakatifu sana Mungu amupe padri wetu nguvu.

  • @user-fh8yy8uk3n
    @user-fh8yy8uk3n หลายเดือนก่อน

    Pole sana father. Waovu wanapotafuta njia za kuumiza wateule wa Mungu kwaajili ya Utumishi, hufanikiwa kwa uchungu na misiba kama kupigwa tauni. Lakini kwa hakika, Kuna baraka kubwa Kwa mtumishi wa Mungu kupitia changamoto na majaribu maana changamoto na majaribu ni mbolea ya Imani. Mungu asikupungukie baba katika mahitaji ya utume wako. Amem

  • @davidwilliam4820
    @davidwilliam4820 2 ปีที่แล้ว +6

    Fr. Pole sana, namshukulu Mungu kwa simlizi ya mapito yako kwetu na changamoto hii, nimejifunza mengi kubwa zaidi nikumtegemea Mungu ktk yote!

  • @iddimgombero6853
    @iddimgombero6853 2 ปีที่แล้ว +6

    Nimelia sana baba, mungu aendelee kukulinda hilo in jaribu tu

  • @mmetvonline7521
    @mmetvonline7521 2 ปีที่แล้ว +13

    Nimejifunza sana juu ya hii kesi " Sisi kama wanaume kama tunajitolea kuwasaidia watoto wa kike nabidi tuwe makini sana kwani wanaweza wakatuangamiza hakika watoto wa kike ni watu Majasiri sana yaani wapo tayari kumuangamiza mtumishi wa Mungu kwa maslahi yao ya uongo"

    • @annahulilo6719
      @annahulilo6719 8 หลายเดือนก่อน

      Ni kweli kabsa... Mungu awazididshie hekima maana kama ameweka ndani yako moyo wa huruma, wa kuwasaidia wahitaji au watu kama hao huwezi acha kufanya! Roho Mtakatifu awawezeshe!!!🤲🤲🤲🙏 Mabinti dizain hiyo nyuma yao huwa kuna jambo/watu wanaowasukuma kufanya hivyo! Nao Mungu awasaidie wawe wanajitambua tu🙏

  • @SARAHKONKI
    @SARAHKONKI 14 วันที่ผ่านมา

    Mungu ni mwaminifu father kwa kila jambo

  • @kokuhabwarutechura6272
    @kokuhabwarutechura6272 2 ปีที่แล้ว +5

    Mungu na aendelee kukusimamia Fr. Baada ya msalaba utukufu! Mungu ni mwema sana. Amani iwe juu yako Fr.

  • @josephkajinga5114
    @josephkajinga5114 2 ปีที่แล้ว +7

    Mungu akubariki Padre. Mtegemee muumba wako na endelea kumtumikia Bwana!. Padre, kama Yesu alibambikiziwa kesi na Wayahudi sembuse wewe binadamu? Tenda kazi ya utume wako.

  • @francismsonde3307
    @francismsonde3307 2 ปีที่แล้ว +13

    Pole sana Padre ! Mungu atajibu ! Ila hii ndio inapelekea nchi hii watu wanatuhumiwa Ugaidi kwa ushahidi usio na mashiko.

  • @magretmukami1180
    @magretmukami1180 21 วันที่ผ่านมา

    Don't worry umepitia hayo yote dio wengine wajipatie nguvu na wewe you are the fruit of God,God will open many blessing of you.

  • @uvinza_stationery8
    @uvinza_stationery8 2 ปีที่แล้ว +1

    Pole sana padre naomba ujifunze kwa mt maria goreti alivyo mjibu melikiades nimemsamehe na ninamuombea neema ya kutubu,nimapito tu hayo padre ambayo ni lazima upitie Mungu anahitaji kukuinua kwa viwango vya juu, Majaribu ni kipimo cha imani usivunjike moyo baba

  • @florentinefmmkenda3902
    @florentinefmmkenda3902 2 ปีที่แล้ว +28

    Pole sana Padri, Mungu aendelee kukulinda uendelee kwangazia watu wake na kuendelea kukuza upendo , amani na matumaini kwa watu wa Mungu.

    • @eucabethnyagero9636
      @eucabethnyagero9636 2 ปีที่แล้ว

      Haki binadamu ni wabaya hadi mtumishi wa mungu mnampaka matope mungu atamtoa tu pole sana padri

    • @idrisabdulrahman8709
      @idrisabdulrahman8709 ปีที่แล้ว

      Pole sana.MWENYEZI MUNGU YUKO PAMOJA NAWE,AMIIN

    • @eliawezaayoub8868
      @eliawezaayoub8868 ปีที่แล้ว

      ​@@eucabethnyagero9636 so

    • @eliawezaayoub8868
      @eliawezaayoub8868 ปีที่แล้ว

      ​@@eucabethnyagero9636

    • @peragiacosmas4778
      @peragiacosmas4778 ปีที่แล้ว +1

      Mungu akutetee Fr. Uyu Dada kajitaftia rahana maneno yako yanaumiza Sana Mungu awe pamoja na wewe. Atambuhi karama yako atapata taabu Sana amrudie Mungu na kutubu na kuakikisha ametubu mbele ya Mungu na jamii nzima.

  • @johnmligo6966
    @johnmligo6966 2 ปีที่แล้ว +11

    Mungu ni mwema.... umenifunza sana wewe Padre!

    • @casmirimringo6021
      @casmirimringo6021 2 ปีที่แล้ว

      Pole sana padri

    • @annahalale9083
      @annahalale9083 2 ปีที่แล้ว

      May the good Lord give u all the neccesary graces u need in ur life.

  • @danielnicco5421
    @danielnicco5421 14 วันที่ผ่านมา

    Pole sana Padri Swai. Mapito hayo nimewahi kupitia nayaelewa ya kusingiziwa na hatimaye
    Daaaa so sad

  • @angelomedard
    @angelomedard 2 ปีที่แล้ว +1

    Inauma saana Fr.
    Ila kwa ushauri nikwamba ingia ktk mafungo binafsi ya novena Mungu hawezi kubali fedheha ikiwa Kama kwa kubali chake alikusimamisha altareni basi utarudi kwa damu ya Yesu

  • @filbetersalvatory9725
    @filbetersalvatory9725 2 ปีที่แล้ว +23

    🤲Hekima ya kiMungu ikae ndani yako,Mungu wet aikuzee imani yako na kuidumisha zaid usiteterekee in Jesus name 🙏

  • @glorydavidmramba8750
    @glorydavidmramba8750 2 ปีที่แล้ว +8

    Mungu atakutetea,very sorry Fr everything's happens for a reasons Mungu alikuwa na sababu yake na ndiyo maana aliliruhusu lipite na litaisha utarudi maisha yako ya utume MUAMINI MUNGU.....watu wengine wanakosa misaada kwa sababu ya vitu kama hv jamn badilikeni mambo mengine yanaumiza sana hii ni sawa na uuaji!!

  • @shidabeatus253
    @shidabeatus253 หลายเดือนก่อน

    Pole Sana Padri hii Dunia ni ngumu Sana tumejifunza kitu. Hapa mfadhili mbuzi na SI binadamu uliemtendea Wema amekuwa adui Yako Fanya Kazi ya Mungu na atakulipa hiyo familia na yule alimtumia huyo Binti wameitafuta laana tu maisha Yao yatakuwa magumu tu Mungu akulinde

  • @CharlessMasanja
    @CharlessMasanja 22 วันที่ผ่านมา

    Pole Sana father Mungu ni mwenye haki

  • @nyabahailani3169
    @nyabahailani3169 2 ปีที่แล้ว +10

    Waandishi wa habari ndio wamekua matapeli wakubwa ingawaje sio wote wana njaa sana

  • @marykarebeti9410
    @marykarebeti9410 2 ปีที่แล้ว +8

    Kweli dunia haina huruma. Mtu unamsaidia, halafu anakuumiza kwa kukusingizia.
    Waliofanya hivyo mbona watashaa.
    Daaaaahhhhhh!!

  • @JosephaNdomba
    @JosephaNdomba 11 วันที่ผ่านมา

    Pole sana mtumishi wa mungu,kila mwanadamu anajlribu lake

  • @DoroselaSalvatory-ml8sg
    @DoroselaSalvatory-ml8sg หลายเดือนก่อน

    Mungu wetu ni mwaminifu hakika ametenda,padri wetu utainuliwa na Mungu mahali pa juu juu zaidi

  • @janslinjanslin9889
    @janslinjanslin9889 2 ปีที่แล้ว +15

    Tunakuombea Padri Mungu atasimama na wewe ila hiyo laana itawatafuna mpaka kizazi chao cha 4

  • @upendoeliudi5196
    @upendoeliudi5196 2 ปีที่แล้ว +5

    Pole father, Mungu ana tenda kwa haki

  • @christermapunda503
    @christermapunda503 9 วันที่ผ่านมา

    Mungu akuokoe na mtego wa muwindaji. Pole sana.

  • @EwaldKweka
    @EwaldKweka หลายเดือนก่อน

    Siku zote mtimiza kusudi lazima ajaribiwee,so shetani siku zote anapenda kuzuia kusudi la Mungu ila mtimiza kusudi la Mungu azuiliwii na mwanadamu, Jesus is my way,Mungu akulinde bro swai,

  • @cesskemush8635
    @cesskemush8635 2 ปีที่แล้ว +28

    I'm really so much hurt for this but be strong Father....remember what Jesus went through until his death may almighty God be with you and stand with you forever...God will punish them

  • @nmatuja2191
    @nmatuja2191 2 ปีที่แล้ว +14

    Pole sana padre, Mungu akutie nguvu.Imeniuma sana.

  • @jescaedwardkurumela4333
    @jescaedwardkurumela4333 2 ปีที่แล้ว +2

    Daudi akasema siwezi kumgusa mpakwa mafuta wa Bwana,
    Oole ole ole wako uliyemgusa😭 mpakwa mafuta, maana umegusa mboni ya Mungu, pole Sana binti na familia yako rehema ya Mungu iwe juu yenu

  • @AnnaMmary-rn2xc
    @AnnaMmary-rn2xc 28 วันที่ผ่านมา

    Mungu atende sawa na huruma zake siku zote za maisha yetu

  • @happymsaki1720
    @happymsaki1720 2 ปีที่แล้ว +3

    Nimejikuta nalia kwa kweli Father hakuna kama msamaha na wala hawana cha kukulipa muachie Mungu peke yake yy ndiye atakayekufuta machozi yako

  • @michaeljoel2139
    @michaeljoel2139 2 ปีที่แล้ว +5

    Aisee mungu akujalie,msamehe tu huyu binti maana ugumu wa maisha ndoo ulimfanya aseme ivo akijua anajikomboa kumbe ndoo anaharibu