MBUNGE ATUKANWA NA WANANCHI KISA HAPOKEI SIMU ZAO - "SIWEZI KUPOKEA SIMU ZOTE"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 ต.ค. 2024
  • MBUNGE ATUKANWA NA WANANCHI KISA HAPOKEI SIMU ZAO - "SIWEZI KUPOKEA SIMU ZOTE"
    Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham amewataka baadhi ya Wananchi wanaomtolea lugha za matusi asipopokea simu zao kuacha kufanya hivyo kwakuwa hupokea simu zaidi ya 200 kwa siku moja.
    Akizungumza na wakazi wa kata ya Lupiro wilayani Ulanga alipoenda kutoa msaada wa bati na unga kwa wahanga waliobomolewa nyumba zao na upepo Salim amesema ameweka makatibu wa Mbunge kila kata ili wamsaidie kupokea changamoto za wananchi ili wazipeleke kwake kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
    Aidha Mbunge amewaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa hata asipopokea simu zao changamoto zao humfikia kupitia makatibu wake na zile zilizo ndani ya uwezo wake huzitatua.
    WATCH WASAFI TV📺
    AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113
    LISTEN WASAFI FM 📻
    88.9 DAR/ZNZ/PWANI 📻 | 104.1 DODOMA 📻 | 94.5 ARUSHA 📻 | 97.3 MBEYA 📻 | 94.9 MWANZA 📻 | SHINYANGA 106.3 📻 | KIGOMA 101.7 📻
    Follow Us On:
    INSTAGRAM: / wasafitv || / wasafifm
    TWITTER: / wasafitv || / wasafifm
    FACEBOOK: / wasafitv
    𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2021 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅.
    #wasafi #wasafitv #wasafifm

ความคิดเห็น • 114

  • @hannanommy302
    @hannanommy302 2 ปีที่แล้ว +14

    Kama huwezi kupokea simu subiri kipindi cha uchaguzi ndo utajua hujui;wasikilize Usiogope matusi hayauwi,

  • @mwamkolutego6197
    @mwamkolutego6197 2 ปีที่แล้ว +7

    Busara ni kdg hapo huwezi kuongea hivo na wapiga kula wako ,basi umeshindwa kunyoosha tumia hata uongo bc lkn kwa kauli hiyo kwa huwezi kupokea simu zote tyr anahabu kura zake mwenyewe kazi ipo .

  • @fortunatusphilimon8992
    @fortunatusphilimon8992 2 ปีที่แล้ว +1

    Hatariiii

  • @bernardjohn8788
    @bernardjohn8788 2 ปีที่แล้ว +3

    Hilo ni kosa kubwa sana kwa mwanasiasa angetumia njia nyingine, hiyo clip watakuja kuitumia wakati wa kura, kila mbunge anakutana na hali hiyo ila hawalisemei hadharani inatakiwa uishi kisanii hivyo hivyo

  • @fredrickswai2566
    @fredrickswai2566 2 ปีที่แล้ว +9

    Ajiri mtu wa kupokea simu za wananchi wako.

  • @aronatv47
    @aronatv47 2 ปีที่แล้ว +6

    Wabunge wengi walipita kwa Nguvu ya Serikali ys Awamu ya Tano kwa Mabavu musipoangalia wengi mtakatwa sans 2025.

    • @salumjumaruhaga2513
      @salumjumaruhaga2513 2 ปีที่แล้ว

      Hata mmoja harudi ,yaani ilikuwa kwenye Kura za maoni anachukuliwa mshindi wa mwisho yaani watatu ndio anagombea

  • @KananaKadogholo
    @KananaKadogholo ปีที่แล้ว

    Umechemka,Bora ungefinyia!

  • @simulizi2678
    @simulizi2678 2 ปีที่แล้ว +1

    Yeaaah subiri adi 2025.

  • @maxcharles5436
    @maxcharles5436 2 ปีที่แล้ว +1

    Huyu jamaa yuko vzr sana

  • @adammbuba7230
    @adammbuba7230 2 ปีที่แล้ว

    Kweli kabsa mh

  • @Fks856
    @Fks856 2 ปีที่แล้ว

    Ndivo mnajitetea

  • @floramlowe7078
    @floramlowe7078 2 ปีที่แล้ว

    Jamani watu wa ulanga wanarahisisha uongozi sio kazi rahisi.

  • @jeffkonki8279
    @jeffkonki8279 2 ปีที่แล้ว

    Mbona kwenye uchaguzi mnapokeaga sana

  • @habibumussa7712
    @habibumussa7712 2 ปีที่แล้ว +1

    Tatizo lenu mkisha pata mna sahau sana

  • @benardmwinuka6948
    @benardmwinuka6948 2 ปีที่แล้ว

    Umechemka ww mpuuzi sana

  • @Mbingu77
    @Mbingu77 2 ปีที่แล้ว

    Weka sekretari wa kupokea su tuu😄😄😄😄😄

  • @seifndimbaye1919
    @seifndimbaye1919 2 ปีที่แล้ว +1

    sasa huwez pokea sim zawalio kuchagua ayo maendeleo unayo waletea huwa unayaota au kukiwa namatukio yakustukisa piya unayaota? hufai

  • @latifabashiru5598
    @latifabashiru5598 2 ปีที่แล้ว

    Mda wa kupokea cm huna ila sms unasoma ?

  • @veronicascottmollel7897
    @veronicascottmollel7897 2 ปีที่แล้ว

    Ulanga kwetu ❤️

  • @sonnyr1899
    @sonnyr1899 2 ปีที่แล้ว +6

    2025 kweli ni kugumu mno sema tu upinzani ndio hauendi na fursa ila wengi wenu mmeingiya pale kwa msaada wa marehemu Mze Magu.

  • @AlvinMakenzi
    @AlvinMakenzi 5 หลายเดือนก่อน

    Pokea Sim

  • @benedictmrisho5947
    @benedictmrisho5947 2 ปีที่แล้ว +2

    Hawaelewi Kuwa umma ndio uliomchagua. Wengi wenye maringo huja kujutia uchaguzi ukifika. Subiri uchaguzi ujao Kama unawahangaikia usihofu 2025 watakuenzi lakini Mh kama unawadharau 2025 usijaribu.

  • @yahyahamad1802
    @yahyahamad1802 2 ปีที่แล้ว

    Tenga mda kila wiki au kila mwezi uwafate uwasikilize shida zao

  • @nyellasuwedisanga6929
    @nyellasuwedisanga6929 2 ปีที่แล้ว

    We unashida kwani unafanya bure c unalipwa wanna uliga 😁😁😁

  • @Sangaadam
    @Sangaadam 2 ปีที่แล้ว

    Huyu mbunge hajui kabisa kujieleza daah!!!

    • @Hamy1109
      @Hamy1109 2 ปีที่แล้ว +1

      Hajui siasa huyo....yeye analeta habari za "Logic" mbele ya Wananchi....Ngoja 2025 watasema hayo hayo ya kugoma kupokea simu zao na ndio hapo inakuwa bye bye

  • @frankkimaro1354
    @frankkimaro1354 2 ปีที่แล้ว +2

    Acha dharau Kijana

  • @amooclassic1133
    @amooclassic1133 2 ปีที่แล้ว

    Kijana utangushwa kama kampuni ya kamisi comes 2025 ,,

  • @rajabuamiri5016
    @rajabuamiri5016 2 ปีที่แล้ว

    Piga kazi muheshimiwa

  • @heritier5119
    @heritier5119 2 ปีที่แล้ว

    Wananchi watakula simu,

  • @rukiaiddyyahaya9506
    @rukiaiddyyahaya9506 2 ปีที่แล้ว +1

    Hahaha nimecheka mpaka mate

  • @emmanuelndahan9815
    @emmanuelndahan9815 3 หลายเดือนก่อน

    Kauli zako hazina afya

  • @fabianmayunga1166
    @fabianmayunga1166 2 ปีที่แล้ว

    😲2025 UTAJUA HUJUI🤕

  • @johnmakubi190
    @johnmakubi190 2 ปีที่แล้ว

    kwani alichaguliwa nanani?

  • @manenombuma3987
    @manenombuma3987 2 ปีที่แล้ว

    Mbeleko election.hii ni hatari.

  • @rahmarahma920
    @rahmarahma920 2 ปีที่แล้ว

    Huchaguliwitena kwanini usipokee hunasababuya msingi

  • @mugemainyas5241
    @mugemainyas5241 ปีที่แล้ว

    Wabunge ni kama watumwa. Labda mwambieni wachague watu wawili ndo wawe wawakilishe kero zao.

  • @reganmartin5485
    @reganmartin5485 2 ปีที่แล้ว +4

    Simu 200 kwa siku na Kila mtu atumie dakika 3 kuongea hapo ni dakika 600 ina maana ataongea saa moja asubuhi Hadi saa 10 yaani masaa 10 Bila kupumzika je Nani anaweza?

    • @Sangaadam
      @Sangaadam 2 ปีที่แล้ว

      Ndio maana Wabunge wanatakiwa kua na ofisi ili kuwe na simu maarumu kwa ajili ya Mambo yanayohusu Ubunge ,So sio lazima simu apokee yeye Ila ofisi itapokea simu za wananchi wako na kupangilia jinsi ya kutatua kero au maombi ya wananchi wako...... Hao ndo wale wa vikaratasi km Steve Nyerere alivyo waita hawajui hata wajibu wao ni nn

  • @benardthomas8347
    @benardthomas8347 2 ปีที่แล้ว

    Huyo mmemchagua akalete maendeleo yake siyo ya wananchi, kwan hakuna njia nyingine ya kusikiliza kero za wananchi.

  • @jumannentimizi9000
    @jumannentimizi9000 2 ปีที่แล้ว

    WEWE SIYO MBUGE WAWANANCHI WEWE NI MBUGE WA MWENDAZAKE KWANI HUO MWAKA 2020 ULITEULIWA TU SIYO KWAMBA ULICHANGULIWA WEWE USIWADANGANYE WATU

  • @Mbingu77
    @Mbingu77 2 ปีที่แล้ว

    😄😄😄😄 subiri utaona mh mbunge😄😄🛌

  • @siashao169
    @siashao169 2 ปีที่แล้ว +1

    Pokea sim za wananchi wako! ujue matatizo yao ili ukawakilishe huko kwenye vikao.

  • @kalengashoppingcenter1108
    @kalengashoppingcenter1108 2 ปีที่แล้ว

    Tunakupiga chini tu, no kujitetea huna Dili kazi rushwa tu

  • @ramadhanimtetu7246
    @ramadhanimtetu7246 2 ปีที่แล้ว

    Mbunge niajili niwe mpokea simu wako jamani nakuhakikishia hiyo shida itakwisha

  • @simbarajabu4157
    @simbarajabu4157 2 ปีที่แล้ว

    Ndio zao hao wabunge

  • @MyName-wd8cp
    @MyName-wd8cp 2 ปีที่แล้ว +2

    Huna kazi zingine zakufanya?? Kwani hizo unazofanya ni kazi za nani?
    Siasa! Siasa! Siasa! SIASA NI URONGO, SIASA NI KUPAKANA MATOPE, hizi ndizo kauli za wana siasa! Je, kwa mwananchi unategemea nini kwa mwana siasa?
    Unampigia mtu kura kisha yeye anapata Kula vizuri na familia yake. And then wew unabaki kuomba omba. WANASIASA MUOGOPENI MUNGU hakuna cheo chakudumu hapa duniani!

  • @heritier5119
    @heritier5119 2 ปีที่แล้ว +4

    Huyu mbunge kafanya Sana maendeleo kwa pesa zake za mfukoni, kajenga vituo vya afya, kajenga mashule, zaidi mcheki youtube

    • @makongorowassira6593
      @makongorowassira6593 2 ปีที่แล้ว +4

      Sio hela zake bali za ofisi ya mbunge. Ambazo ni nyingi tu

  • @hamidmweusiii35
    @hamidmweusiii35 2 ปีที่แล้ว

    Huyu mbunge kiufup 25 hana chake kw hyo saiv achkue chake mapema afany mambo yake aachane na wananchi wapmbn na hali zao huwez kila mtu ukamrizisha kwiy broo ushapta shavu jipange kivyako ule shavu na familia yako maisha yaende

  • @shabansalee4924
    @shabansalee4924 2 ปีที่แล้ว +1

    Kwa mm sijakuerewa 😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😭😭😭😭😭😭😭😭

  • @robbierobin3094
    @robbierobin3094 2 ปีที่แล้ว

    Hahaha nitoe na 20k mheshimiwa

  • @boscomfundo7953
    @boscomfundo7953 2 ปีที่แล้ว

    Boya kwel huyu, ndio shida ya wabunge wa michongo hawa

  • @africakaka7217
    @africakaka7217 2 ปีที่แล้ว

    Pokea simu ili ujue changamoto zawananchi wako ama tenga muda wakuwasikiliza wananchi wako bila wao usingekua hapo, wape muda ili uweze kuongea nao nasio kusema umechaguliwa Kupokea simu ama shida zao, kumbuka wao ndio wanaojua changamoto wanazo zipata kwahiyo kawaida kukupigia . Hivyo tu kiongozi

  • @omarytexesunauwababa4587
    @omarytexesunauwababa4587 2 ปีที่แล้ว

    Mbunge ni watu

  • @otianasanga9106
    @otianasanga9106 2 ปีที่แล้ว

    Nikweli mtajua niwapi mmekosea kama umechoka kupokea bas waachie watakaoweza kupokea

  • @muhidiniabass4385
    @muhidiniabass4385 2 ปีที่แล้ว

    Acha ujinga ujue nafac uliyopo waliyokuweka ndo hao usiyopokea cm zao

  • @thomaschengena6369
    @thomaschengena6369 2 ปีที่แล้ว

    ukiamua unaweza kwann usiwape wasaidizi wako

  • @xingho3990
    @xingho3990 ปีที่แล้ว

    Wewe acha ubabe

  • @jacksongidion5170
    @jacksongidion5170 2 ปีที่แล้ว

    6

  • @heritier5119
    @heritier5119 2 ปีที่แล้ว

    Salimu ajiri mtu wa kupokea simu

  • @Hamy1109
    @Hamy1109 2 ปีที่แล้ว

    Acha kulia lia....si ulitaka mwenyewe Ubunge. Wewe 2025 hutoboi! Huwajui wananchi wewe.

  • @mzeemtopa1086
    @mzeemtopa1086 2 ปีที่แล้ว

    Mbona wakati wa kampeni unapokeabkucha nzima

  • @amiribakari2528
    @amiribakari2528 2 ปีที่แล้ว +1

    mbona wakati unatafuta kura ulikua unapokea ..na ukawaahudi piga sim wote me nitapokea ..na mpo wengi sio wewe tu 25 mtatujua

  • @saidhassan7779
    @saidhassan7779 2 ปีที่แล้ว

    KWANI UMELAZIMISWA UGOMBANIE AU??

  • @makongorowassira6593
    @makongorowassira6593 2 ปีที่แล้ว

    Huyu mbunge hajitambui, kwani hana ofisi ya mbunge? Direct calls kwenye ofisi.

  • @sagandamalechampullo659
    @sagandamalechampullo659 2 ปีที่แล้ว +3

    HIZO NI DHARAU SANA, FALA WEWE YAANI, UNAKATIBU, SECRETARY, NA MSAIDIZI WAKO HALAFU WOTE WASHINDWE KUPOKEA SIMU OFISI NZIMA, SI DHARAU HIZO!

    • @modestmzumbwe588
      @modestmzumbwe588 2 ปีที่แล้ว

      Mtu ambaye hakuchaguliwa hawezi kujua hayo hao walibebwa

  • @venancerichard920
    @venancerichard920 2 ปีที่แล้ว

    Anajitetea huyo kashapata

  • @boniphacewambura1427
    @boniphacewambura1427 2 ปีที่แล้ว +2

    Kama huwez kupangilia ratiba na kupokea simu achia ngazi na hii ni dalili ya kuferi
    Kutuambia màmbo ya makatibi hizo ni siasa

    • @christianhussein5128
      @christianhussein5128 2 ปีที่แล้ว +1

      Sasa unapiga cm za mizinga wewe mwananchi nenda kalime

    • @fatmafaki6163
      @fatmafaki6163 2 ปีที่แล้ว

      @@christianhussein5128 huyo mbunge hasemi kweli, anaona Kila simu ataombwa, basi bora divert simu zote bakisha ya mama Samia tu akitegemea uteuzi, si hapendi kutoa yeye apewe tu

  • @Worldunite
    @Worldunite 2 ปีที่แล้ว +1

    Ila kusema ukweli kupokea simu 200 kwa siku inabidi uwe na kichwa km gorofa, sio mchezo

  • @AfwilileNisaidie
    @AfwilileNisaidie 2 หลายเดือนก่อน

    Wewe mbunge mshamba hujui majukumu yako ulivyo omba kazi

  • @jumakapola419
    @jumakapola419 2 ปีที่แล้ว

    Wanaichi muwe makini kuchukua elfu 10000 zao

  • @awadhrajabu1403
    @awadhrajabu1403 2 ปีที่แล้ว

    Uchaguzi Ujao Utakua Mkali Kuliko Muazavo Kwasababu Moja Uchaguzi Uliopita Wengi Wameteleza Lakini Ndio Ivo Sema Yajayo Yanapendeza Sema Upinzani Wanachowaza Madalaka Badala Ya Kujipanga Mbunge Wewe Wacha Uongo Wewe Wakati Wa Uchaguzi Ungepokea Simu Zote Na Iyo Elfu20 Ungetoa Bila Kerere Zozote Au Sisi Kujua

  • @yusufmohamed8874
    @yusufmohamed8874 2 ปีที่แล้ว +1

    Kwanini ufunge vioo wakati wa kutafuta kura unavifungua.

  • @simbarajabu4157
    @simbarajabu4157 2 ปีที่แล้ว +1

    Mm napokea cm Mia 3 kwa cku ,sasa ww unashindwa nn

  • @elicanageorge1319
    @elicanageorge1319 2 ปีที่แล้ว

    USIYAONGEE HAYO MKUU HAPO UNATENGENEZA MATATIZO 2025 ACHANA NA HIO HABARI

  • @fadhilikazingo1261
    @fadhilikazingo1261 2 ปีที่แล้ว

    Natamani kujenga hoja na kusema kitu ila acha ninyamanze tu🥺🥺

  • @otianasanga9106
    @otianasanga9106 2 ปีที่แล้ว

    Kwani unafanya Bure

  • @muhambwetvonline
    @muhambwetvonline 2 ปีที่แล้ว

    Mkishiba ndio zenu sasa 20 tu unashindwa hata ku songesha

  • @burudikanamaruma8950
    @burudikanamaruma8950 2 ปีที่แล้ว

    Huyu jamaa huyu ongea tu imebeba dharau

  • @MasterOil-qm6vw
    @MasterOil-qm6vw 4 หลายเดือนก่อน

    Kwan wanakupigia simu kila siku umekua nani wao tu kwakua hawajui kwan mbunge analeta maendeleo gani kwenye taifa mm najua kazi yako ni kuwakilisha kero za wananchi bungeni lakin hela hutoi wewe

  • @saryajoseph6642
    @saryajoseph6642 2 ปีที่แล้ว

    Pokea simu za watu wewe Acha janja janja

  • @salumjumaruhaga2513
    @salumjumaruhaga2513 2 ปีที่แล้ว

    Wewe si mbunge ,mbona Una chemka ,ilA wewe hukuchaguluiwa uliwekwa Tu kama boya

  • @husseinhumbi6373
    @husseinhumbi6373 2 ปีที่แล้ว +1

    Acha uwongo Kama ulikuwa na kazi nyingine ya kufanya way ukwenda kufanya hizo kazi acha uongo kwa watz

  • @bahatikazungu7657
    @bahatikazungu7657 2 ปีที่แล้ว +1

    Kweli wewe mbunge kubwa jinga kwa hiyo kila simu niyakukuomba hera kama ni changamoto ya shule

  • @husseinkhaji895
    @husseinkhaji895 2 ปีที่แล้ว

    Mwongo tu wewe kwani ukipokea ukamwambia huna atakufanyaje ukipigiwa simu na mkeo au mama yako hutapokea? Acha kujiteea

  • @Worldunite
    @Worldunite 2 ปีที่แล้ว

    Vikao mnalipwa lkn wewe, sio kwamba hamlipwi

  • @odilomagungu8803
    @odilomagungu8803 2 ปีที่แล้ว

    Huchaguliwi Tena wewe

  • @bulikidittu3361
    @bulikidittu3361 2 ปีที่แล้ว +1

    "Sio kwamba Sina shughuli zngne za kufanya" WTF kwahiyo hyo siyo kazi yake kwenda kwenye vikao juu ya wananchi wake au n ya nan

    • @johnlembo2955
      @johnlembo2955 2 ปีที่แล้ว

      Yeah wtf! Hataki kusumbuliwa, ana kazi zake zingine za kufanya. Anakosaje kuwa na secretary kwa mfano

    • @bulikidittu3361
      @bulikidittu3361 2 ปีที่แล้ว

      @@johnlembo2955 nan kaongelea kuhusu kusumbuliwa kwenye simu, I talked about meetings only kwann aseme ameenda kwenye vikao kwaajili yao siyo kua hana mambo mengne ya kufanya bt aliamua kwenda kwaajili yao. Hio dharau, vikao n majukumu yake.

    • @johnlembo2955
      @johnlembo2955 2 ปีที่แล้ว +1

      @@bulikidittu3361 I think there is some misunderstanding here on my comment. I started with "yeah"(yes) meaning nakuunga mkono. Why would he say in public that he have some parsonal things to do when he wanted this kind of job? It's arrogant and incompetent of him. He supposed to have a secretary kumsaidia kuchukua simu zingine. He do not deserve a job as mbunge

  • @boniphacewambura1427
    @boniphacewambura1427 2 ปีที่แล้ว +2

    Umepata ubunge unaringa acha dharau

    • @j.c.maxima816
      @j.c.maxima816 2 ปีที่แล้ว +1

      Huyu ni la 7, lakini baada ya kupata Ubunge, dharau imezidi ! Jamaa hakumbuki kuwa Wananchi hawa ndio walimpa heshima alionayo! 2025 atajifunza kitu !

    • @heritier5119
      @heritier5119 2 ปีที่แล้ว

      Ana pesa kuliko hata huo ubunge, wananchi ndio waliomlazimisha awe mbunge. Ni tajiri wa migodi ya madini

    • @j.c.maxima816
      @j.c.maxima816 2 ปีที่แล้ว +1

      Ni kweli, alikuwa na pesa, lakini alikuwa anahitaji heshima... Kukaa na Wasomi wakati yeye hata kuandika ni shida, kuwa karibu na Wakubwa wa Nchi hii, kuheshimika katika Jamii! Na hii ameipata kupitia Wananchi... Kwa hiyo, ajishushe na kuacha dharau!

    • @boniphacewambura1427
      @boniphacewambura1427 2 ปีที่แล้ว

      Eti anapesa kuliko ubunge acheni uongo

    • @hafidhcalavoice9295
      @hafidhcalavoice9295 2 ปีที่แล้ว

      Hujitambui wewe umekosra sana

  • @saadmbaraqa5272
    @saadmbaraqa5272 2 ปีที่แล้ว

    Wajinga ndio waliwao

  • @haniffa9024
    @haniffa9024 2 ปีที่แล้ว

    MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI UPONE KANSA...DAWA YA KANSA
    *#.
    th-cam.com/video/ZgfBwGAJlrQ/w-d-xo.html

  • @haniffa9024
    @haniffa9024 2 ปีที่แล้ว

    MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI UPONE KANSA...DAWA YA KANSA
    *#.
    th-cam.com/video/ZgfBwGAJlrQ/w-d-xo.html