Salama Na MSIGWA SE6 EP01 FULL SHOW | SEMA PART 1 | SendTip Through MPESA LIPA NO 5578460

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ย. 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSCRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    #SalamaNaMsigwa ndo kifungua pazia cha msimu mpya wa kipindi chetu hiki baada ya kukaa nje kwa takriban miezi mitano, ndani ya hiyo miezi mitano tulipata kujifunza mengi yalojaa baraka na mengi pia yametokea ambayo yananifanya binafsi niendelee kujifunza kwa kadiri siku zinavyoenda na kwa hilo sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu alojaa Rehema nyingi sana.
    Ukiachana na yangu na ya wenzangu, kwenye maisha ya huyu mgeni wetu nambari moja naye pia mengi yametokea kwa upande wake, kwenye maisha yake, haswa kwa upande wa kazi. Kwa mtu ambaye alikua Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, mpaka kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali kwa kipindi kisichozidi miezi mitano nacho pia si kitu kidogo, na pengine kwa kipindi kile ambacho tulisema nasi tunachukua breki yeye pia hakuwahi kufikiria kama angekua kwenye nafasi hii alonayo sasa. Kweli jambo usilolijua ni kama usiku.
    Gerson Partinus Msigwa, kutoka Songea kwenye familia ya kawaida tu ambaye mapenzi yake makubwa ya kazi yake na kujitolea kwingi ndo kumemfanya afike hapo alipo. Haikua kazi rahisi wala, au ya siku moja, au pengine aliona haya yataweza kuja kutimia siku moja, at least kutoka kwenye khadithi aliyonipa kweye meza yetu.
    Kabla ya TBC Songea Mr Msigwa kazi yake ilikua ni kilimo tu kama kijana wa kawaida ambaye anakua na kuona wazazi wake wako shambani, hakua na ndoto kubwa, hakua malengo ya siku moja kuwa ndani ya Land Cruiser au kuwa na ukaribu na marais kadhaa wa nchi hii. Kazi yenyewe aliipata baada ya kuambiwa na mtu kwenye familia yao kwamba kuna tangazo la kazi ya Radio. Hakufanya ajizi akaenda, alikutana na watu kadhaa katika usaili ila mwisho wa siku yeye na ambaye ndo mke wake wa sasa ndo walibahatika kuchukua nafasi hizo mbili na mengine yamebaki historia.
    Aliwahi kufanya kazi ya kujitolea kwa muda tu, na huo pia ndo wito wake wa vijana ambao ndo wanatafuta kazi kwa sasa, wimbo huu anasema amekua akiuimba kwa kipindi sasa, kutaka wawe wanajitolea baada ya kutaka kupata ajira za moja kwa moja huku wakiwa pengine hata uzoefu hawana. Anaamini (hata mimi pia) kwamba kwa mmoja kujitolea huko kutaweza kufungua nafasi ya kupata elimu, kuonekana na pengine kuaminiwa na mwisho wa siku kuipata hiyo ajira moja kwa moja. Kitu ambacho vijana wengi wa leo wamekua wazito kukifanya.
    Safari yake ilianzia kwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kipindi kile yeye ndo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama mas’hara tu baada ya kukutana nae kwenye kazi, Mkuu alitoa agizo la yeye kuvutwa Ikulu na aanze kufanyia kazi pale. Hakurudi tena Songea, hata familia yake ilibidi ije yenyewe hapa Dar es Salaam, just like that mambo yote yakabadilika. Kutoka kwa JK, kuja kwa Marehemu Rais John Pombe Magufuli na mpaka kwa Rais wa sasa Ndugu Samia Suluhu Hassan ambaye alimbadilishia nafasi yake aliyokua akiishika kipindi ya JPM na kumpa hii alonayo sasa ambayo yeye ndo bosi wa baadhi ya walokua mabosi zake kipindi kile anaanza. Look at God 😄
    Haya mazungumzo hasa yalikua ya kutaka kumfahamu yeye na vitu vinavyomsukuma, na kutaka kujua barabara ambayo alipita ilikua na mashimo kiasi gani, na hata ‘ajali’ ambazo ameshawahi kukutana nazo na jinsi gani alikua ‘anapona’ nazo. Kweli maisha ni milima na mabonde na kwa discipline hii ambayo mwenzetu ameionyesha toka siku ya kwanza mpaka hapa alipo, bila ya shaka mimi na wewe tuna jambo la KUJIFUNZA.
    I hope you’ll enjoy the conversation like I did.
    Love,
    Salama.
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

ความคิดเห็น • 43