Nitwae Hivi Nilivyo [NzK Namba 140]

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 26 ก.ค. 2020
  • Wimbo huu uliimbwa na kurekodiwa mubashara (Live) katika mkutano wa Ibada Kuu, tarehe 04.07.2020. Kanisa zima liliongozwa kuimba na Susan Ngussa, waimbaji wenza kutoka kushoto ni Gibons Mwakyusa, Olipa Tungaraza.
    Katika Ibada hiyo Mchungaji Petro Mganda alitoa somo lililosema:
    Wimbo Namba: 140 (NzK): Hivi Nilivyo Unitwae
    1. Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.
    2. Hivi nilivyo; si langu kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.
    3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni, Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.
    4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.
    5. Hivi nilivyo, mimi tu, Siwezi kujiokoa; Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.
    6. Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.
    Kwa nyimbo zaidi za kitabuni pamoja na historia ya nyimbo hizo ingia katika kusanyo (playlist) ya WIMBO WANGU katika channel hii: bit.ly/Wimbo-Wangu-Playlist.
    Ukiwa na swali, uhitaji wa maombi, ubatizo wasiliana na Mchungaji kwa namba +255 677 048 069 au +255 784 458 957.
    Kama una ushauri usisite kutuma kwa namba +255 713 343 939 au barua pepe live@mwengesdachurch.or.tz.
    Tunapenda kukujulisha kupitia channel hii, kuna vipindi mubashara mbalimbali kila siku jioni kama; Ongeza Ujuzi, Afya ni Mtaji, Kona ya Watoto, Lijue Kanisa na Ibada mbalimbali na maombi. Karibu ku-SUBSCRIBE ili uwe sehemu ya wengi wanaobarikiwa: bit.ly/SUBSCRIBE-Now, watumie na marafiki pia.
    Karibu pia kutembelea tovuti yetu: www.mwengesdachurch.or.tz
    Mungu akubariki.

ความคิดเห็น • 1