WILAYA YA CHEMBA YAPATA BARAZA LA ARDHI TANGU KUANZISHWA KWAKE

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 27 มิ.ย. 2024
  • Wananchi wa Wilaya ya Chemba wanakwenda kutatuliwa kero yao ya muda mrefu ya kukosekana kwa Baraza la ardhi la Wilaya ambalo hutumika kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi inayojitokeza kila wakati kabla ya kufikishwa kwenye ngazi ya Mahakama.
    Hayo yamebainishwa leo June 28, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary wakati akiwaapisha wajumbe wanne wa baraza hilo, hafla ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
    “Tangu kuanzishwa kwa Wilaya ya Chemba 2012, wananchi wake wamekua wakisafiri umbali mrefu kwenda Kondoa kutafuta haki zao za ardhi. Sasa wamepata baraza lao na kufanya Dodoma kuwa na jumla ya mabaraza 6 hivyo, kero ya wananchi wa Chemba kutokua na Baraza la ardhi inakwenda kutatuliwa” Mhe. Senyamule
    Mbali na hilo, Mkuu wa Mkoa, amemtaka Katibu tawala Mkoa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Mkoa, kusimamia mchakato wa kuhakikisha Wilaya ya Chamwino nayo inapata baraza la ardhi na kukamilisha mabaraza yote saba ya Mkoa wa Dodoma kwani ndiyo pekee imesalia bila kuwa na baraza hilo
    Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Gerald Mongella, ameishukuru Serikali kwa kuifanyia kazi kero hiyo. “Tumekua tukipambana na migogoro mingi ya ardhi hivyo baraza hili litatusaidia kupunguza kero hizo si chini ya asilimia 75. Kupitia Baraza hili, haki itapatikana na amani itatamalaki kama ilivyo matamanio ya Mhe. Rais kumaliza migogoro yote ya ardhi”.
    Naye Mwenyekiti wa Baraza la ardhi na nyumba Mkoa wa Dodoma Bw. Omary Mbega, amesema jukumu kubwa la wajumbe hao ni kusaidia haki itendeke na kuwasihi kufuata maadili, kanuni na taratibu zinazoliongoza Baraza kwani ukiukwaji wake unaweza kupelekea kutenguliwa kwenye nafasi hiyo inayodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
    &&&
    #keroyakowajibuwangu
    #dodomafahariyawatanzania

ความคิดเห็น •