WASIOJULIKANA WANANASWA NA POLISI, WAMEUA WATU 10 NA KUWAZIKA WAMEKAA, WATOTO 2 WAZIKWA WAKIWA HAI.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ก.ย. 2024
  • Jeshi la Polisi Nchini Tanzania wamenasa genge la wauaji katika mkoa wa Singida ambao wamekuwa wakiwaua watu na kuwazika wakiwa wamekaa huku watoto wawili walizikwa wakiwa hai.
    Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania David Misime amesema kuwa Polisi waliwabaini watu hao baada ya kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa raia wema na tayari miili ya watu hao imeshafukuliwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
    Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe aliyefika eneo la tukio, amesema Serikali haitamwacha mtu yeyote aliyehusika katika vitendo hivyo kwani ni unyama uliopitiliza.

ความคิดเห็น •