RAIS DKT. MAGUFULI AWASIMAMISHA TBA KUJENGA NYUMBA ZA MAGEREZA UKONGA
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 15 มี.ค. 2019
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Machi, 2019 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuagiza mradi huo ukabidhiwe kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kubaini kuwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeshindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati, licha ya Serikali kutoa shilingi Bilioni 10 za ujenzi.
Ametaka wataalamu wa TBA waliokuwa wakisimamia mradi huo pamoja na Askari Magereza waondoke na kuwapisha JWTZ.
“Kwa hiyo hapa nisimuone mtu wa TBA, nisimuone mtu wa Magereza kuja kusimamia, muwaache Jeshi la Wananchi wafanye kazi zao, siku watakapokuja kunikabidhi na mimi nitawakabidhi Magereza, kwa hiyo watu wa TBA kuanzia leo nimewafukuza hapa” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika mradio huo ambao ulianza zaidi ya miaka 2 iliyopita kwa kushirikisha Jeshi la Magereza ambalo lilikuwa linaisadia TBA katika kazi za ujenzi, na ametaka TBA na Jeshi la Magereza wabadilike katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Nataka kila mlipo watu wa Magereza mfanye kazi, msimamie watu, kama ni ng’ombe muwafuge vizuri wazalishe vizuri hadi muuze mazao nje, kama ni kilimo mlime kwelikweli, muwe ni jeshi la kuzalisha, hii ni aibu kuleta jeshi jingine la wananchi kuja kuwajengea nyumba nyinyi, wakati nyumba mnakaa nyinyi, mlitakiwa muwe mmeshapanga mkakati kwamba TBA wamesuasua, ngoja tufyatue matofari, tuanze kujenga” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Charles Mbuge amesema JKT itakamilisha ujenzi huo ndani ya kipindi cha miezi 2 na nusu kuanzia kesho na kwamba kazi zitafanywa usiku na mchana.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka TBA kutoa maelezo ya namna fedha zilizotolewa na Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 10 zilivyotumika, na ameonya kuwa endapo itabainika matumizi ya fedha hizo hayaendani na kazi zilizofanyika hatua kali zitachukuliwa.
Katika mradi huo, ujenzi wa majengo 12 ya makazi ya Askari Magereza yaliyopangwa kuwa na ghorofa 4 kila moja ulioanza Desemba 2016 umefikia asilimia 45 tu na unaendelea kwa kusuasua.
Jembeeee#watakubalitu..........your a good leader never met before
Outstanding mkuu na waje walale na wafungwa wao 😂😂😂😂
😂😂
Faraja iliyoje kubahatika amirijeshi anayeona mbalisana watanzania ni jambo la kujivunia sana ni mipango ya mungu Tumeteseka sana Tubadirike twende na wakati.
KMBIZA HAO COMMANDO WANGUUU, WAMEZOEA UJINGA UJINGA HAO
Waoh. Love you Mr. President Dr. John Pombe Magufuli
I salute you Mr president!
Safe Sana mheshimia Rais Kaz yako inaonekana.
Safi sana
Hata Umchukie vipi Uncle Magu, Kuna mambo mengine lazima umkubali tu! labda uwe Chizi.!? Hizi nyumba nazikumbuka ni miaka mingi kweli. Kumbe walishapewa na Pesa zote.!!??
Watapike
Na Tanzania ndo ilishafikia hapo. Alitakiwa aje mtu ka Magufuli.
Safi saan mkuu
Sifa ya kiongozi bora ni kuchukua hatua katika muda mwafaka.
hongera J.P.M kwa hatua hii uliyochukua.hakika wewe ni mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo.
aina ya uongozi wako ni wito na kujitoa kweli kweli.nchi yetu inauozo kila sehemu.
Viva C.C.M,viva J.P.M
Saf Sana mhe Rais
Neema Joshuaer ,mambo!!uko poa neema wng
God give me a vision like this Father, Ee Mungu nipe maono kama uyu Baba
I'm a congolaise but 😢😢😢
Nikikupa maono watakuua mapema...pambanatuu na hali yako kwa maendeleo ya ukoo wenu.
Haaaaahaaaaa lazima wazitapike #JeshiHalishindwi #TanzaniaMpyaYaJPM
Uko ulipo Mungu azidi kukulinda
Tanzania kwanza
Hapa kazi tu, 10% watazitapika..!😀
Victus temba Shemeji Nafurahi sana hatua anazochukua Mh Rais zinatia sana Faraja, Lakini Kuna wachache wanataka kuzingua tu .
Watashindwa tu
Piga kazi baba
Safi sana duh kura yangu mimi ni yakoo mjombaa
Wooh
Sipata ona...!!
Huyu ni zaidi ya Rais.
Washa moto haya ndio mabadiliko ...
Walishazoea ubwenyenye....
Jembe
Ukimuona mh Raisi amevaa hiyo kofia na yuko kwe ziara ujue kuna jambo litatokea nani anakubali hii
Chuma hakika mungu alituzawadia Ila hatukuona umuhimu wake pumzika kwa amani jpm
Safi sana jembe
🙌🏾🙌🏾🙌🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾
Real life
Rest in peace kipenzi cha watanzania
R.I.P MKUU DAHH
Mungu mlinde Rais wa 🇹🇿 namwombea afya nzuri
Huwa nakuelewaga Sana naomba Mungu anipe nifanye kama wewe President
Hii ndio maana halisi kiongozi, kuwa na maamuzi magumu mambo yanapoenda sivyo
....NA WATAITAPIKA...!
JESHI halishindwi Mh Rais...!
Ukinuna UWE NA SABABU MJOMBA MAGU BADO WANAJUSAHAU TBA WANALALA TU
2:50
Pumzika kwa amani na baraka Kamanda mkuu JPM
Hahahaha et ntawakabidhi 😂😂 walale na magereza wao😂😂 Rest in peace 🕊️ rais wetu
Aisee huyu jamaa alikua ni MWAMBA kabisa..!
Magu kazini
Vizur sana baba etu magu
Napenda sana mamuz ya rais anataka wachapa kaz
raha sana
Nakukubali sana rais wetu
kwa kauli hii kuna watu wanaenda kufungwa.....
Fukuza tu
Twahitaji kiongozi Kama huyu huku Kenya.
Hawa wanajikosha kwa kina mbowe eti serikali iwape magodolo wafungwa,hivi uende gerezani utoke hujakelwa sasa hereza au umeenda kutalii ,jengeni makazi yenu
That my president I salute you
jwtz safi
Inawezekana Raisi wa awamu hii akaweka historia ya pekee ,kwa kuwa nchini bila kwenda ughaibuni kwa miaka minne.
Vincent Masanja tuseme asante kwakua nakiongozi mwenye mtizamo chanya namsimamo kama uncle
Hakika Fadher More.
Hadi raha ...bravo Mr President... Hao wa kuzitapika itabidi watapike mpaka nyongo
hahahahahah
Jaman ludi kigambon uvukaji feery tunateseka panton kla sku zinaalibika tunateseka
Kazi usiku na mchana.... 😀😀😀😀😀😀
A cleansheet president!
Ewe mwenyez MUNGU ewe mwenyez MUNGU tunakuomba na tunazidi kukuomba enderea kumuongoz kumsimamia kumrinda na kuzidi kuimarisha afya yake raisi wetu ewe mwenyez MUNGU mkuu
RIP
N viongoz wachache wanaoweza kichukua maamuzi kama haya
Hapo ndipo waga Nasema 2020 Kura yangu Kwakoooooo
Jeshi halishindwi huko Vizuri Kanali
kusema ukweli toka moyoni jeshi la magereza lijitathinini upya yani ni sawa na baba tkt nyumba anatoa maagizo ktk familia yake na hayatekelezeki kwa wakati, hata mm nimechukia hii ni aibu, kama pesa zipo tatizo ni nn?? 😄😄😄😄😄😄
Canal jenga Bila shida Ila hao MAGEREZA watapike hela hizo
chuma cha pua ukizingua anakuumbua
Elelo yeye.
Mungu unatisha.Unajua kuwaleta watu wako kwa saa zako, kuliponya taifa lako.
President JPM nadhani bado hawajakuelewa hao wanafanya wajuavyo ni pingu tu huko ni kuhujumu mali ya watanzania walipa kodi usiku na mchana.
Dr magufuli safi sana
Kura yangu
Zmzm