FULL HIGHLIGHTS: SIMBA SC 2-2 AL MASRY (CAF Confederation Cup - 07/03/2018)

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 7 มี.ค. 2018
  • Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Al Masry kutoka nchini Misri katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
    Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2, umeshuhudia mabao matatu kati ya manne yakifungwa kwa penati.
    Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 10 na Emmanuel Okwi dakika ya 74, yote yakiwa ya penati, huku mabao ya Al Masry yakifungwa na Mohamed Gomaa dakika ya 11 na Ahmed Abdalraof dakika ya 26.
    Hata hivyo mchezo huo ulisimama kwa takriban dakika 25 baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha umeme katika dimba la Taifa kukatika huku uwanja ukijaa maji.
    Mchezo huo uliendelea baada ya mvua kupungua, lakini matokeo hayakubadilika na sasa Simba itahitaji ushindi wowote au sare ya kuanzia 3-3 katika mchezo wa ugenini utakaopigwa nchini Misri

ความคิดเห็น • 178